Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 66 - LET'S BREAK UP

Chapter 66 - LET'S BREAK UP

Jioni kwenye mgahawa maarufu Edrian alikaa akimsubiri Lyn ambaye alichelewa kwa dakika kumi na hakukasirika maana alimjua Lyn kwa kutunza muonekano wa uzuri wake hutumia muda mwingi!

Kwa kawaida The Royal Restaurant ina VIP cubes. . Ed alikaa akiangalia kwenye sehemu ya kuingilia huku akiwa na simu yake ya mkononi akiendelea kusoma mrejesho wa baadhi ya wafanyakazi ambao walikuwa kwenye orodha ya mwanasheria Ganeteu waliohisiwa kuwa na malengo mabaya na SGC.

"Sorry Edrian babe nimechelewa" sauti ya Lyn ilikuwa laini na ya taratibu huku akiwa ameegama kwa wepesi kwenye ukuta..

Edrian akainua macho yake huku akikutana na uzuri wa Lyn ambao jioni hii uling'arishwa na gauni refu la rangi ya bluu, likiwa na mkanda wa shaba uliopita kifuani hadi shingoni na kuangukia mgongoni. Alivutia kumwangalia. Uzuri wake ulikuwa hauwezi kufichika. Ed hakujibu chochote akainua jicho lake moja kabla ya kumuashiria akaribie kukaa. Lyn akatabasamu na kusogea akivuta kiti kuketi.

Akainama hadi karibu na uso wa Edrian na kusema

"Am sorry babe, umeona nilivyovaa kukuomba samahani" Lyn akaachia tabasamu lake la mahaba

Lyn tafadhali kaa. Akamjibu kwa sauti ya chini huku akimwangalia machoni..

"Okay.. ngoja tukae tuongee"

Akaketi, Edrian akabonyeza kitufe cha njano kilichokuwa kati kati ya meza ile...

"Lyn umependeza. Be at peace you are beautiful" Edrian akamwambia akijua bila hivyo Lyn hatotulia kumsikiliza, ataanza mbinu zake za kumkwamisha asiseme maazimio ya moyo wake.

"Thank you Edrian. I love you" kama ambavyo Edrian alimfahamu Lyn ni mtu anayependa kupata "attention" sura yake ilionekana kupata utulivu baada ya kusikia maneno aliyomwambia..

"Tuna mambo machache nataka tuongee lakini walau tusubiri mhudumu atuletee oda yetu. Nimeagiza chakula chako pendwa." Aliongea Edrian

Na kabla hajaendelea mhudumu alisimama mlangoni akiwa amebeba tray iliyobeba mvinyo na glasi akisubiri kupewa ishara ya kuingia, ambayo Ed alimuonesha...

Baada ya kuwamiminia kwenye glasi, akaondoka akiahidi kurudi baada ya dakika kumi na chakula..

"Babe kwa yale yaliyotokea asubuhi naomba unisamehe sikuwa na mahali pa kwenda" Lyn alisema baada ya kushusha glasi yake ya mvinyo akaweka mkono wake juu ya ule wa Ed ambao ulitulia mezani..

"Lyn kuna mengi ya kuzungumza kwa sasa tule chakula sababu mimi nina njaa" alisema Edrian huku akimwangalia Lyn ambaye uso ulikuwa uking'aa kwa raha

"Sawa Ed, ..nakupenda sana usinichukulie dhaifu" wakati maneno haya yalimtoka Lyn akiwa ametabasamu na kumfanya Ed kuona onyo nyuma ya alichozungumza..

Akamwangalia, hakuongeza neno akaachia tabasamu kisha akainua glasi yake na kumalizia mvinyo kidogo uliobaki. Chakula kikaletwa na kuandaliwa vyema kwenye meza. Mhudumu akatoka na kuwaacha, Lyn alifurahia kuona chakula akipendacho... "beef lasagne" wakaendelea kula taratibu.

Kimya kiliendelea wakati wa chakula, mpaka walipomaliza, mhudumu akatoa vyombo.

"Ed mpenzi, wakati nakuja nimewaza sana ulivyoniambia nije. Nikahisi unataka kuni suprise na ahadi yako" Lyn akaegama kwenye kiti macho yake yakimwangalia Ed kwa upole..

Ed akajisikia vibaya kwa sababu aliyasikia maneno yake mwenyewe aliyoahidi. Akameza mate na kumwambia

"Lyn.... kuna sababu mbili ambazo zinasimama kama kizuizi cha mimi kuendelea na kile nilichoahidi."

Lyn aliyekuwa ameegama kwenye kiti akasimama kwa mshangao

"Lyn kaa chini unisikilize tafadhali" Ed akainua macho na kumwambia Lyn ambaye alikaa kwa hasira na kubaki amemwangalia usoni

"Najua tumekuwa pamoja karibu miezi sita, nimekufahamu kiasi nawe pia." Ed akameza mate kisha akaendelea...

"Mpaka hapa tulipofika siwezi kuficha kuwa kuna mengi pia sikuyapenda kati yetu. Na kwa sababu hiyo sitaki tuwe na maisha ya majuto kwa kushindwa kuukabili ukweli" Ed akatulia akimwangalia Lyn ambaye kifua chake kilipanda na kushuka akionesha kukasirika..

"Edrian unelekea wapi na haya mazungumzo?" Lyn akamuuliza kwa haraka akimwangalia kwa jicho la ukali

"Let's give each other a break for now" Ed akasema huku akiinua glasi ya maji na kunywa.

"No" jibu la Lyn lilifuata kwa haraka huku akimwangalia Ed