"Na je kama ni sumu ya kuniua taratibu?" Ed akamuuliza akiinua jicho lake
Derrick akashtuka na akaonekana kusumbuka kwa maneno yale lakini akajiweka sawa kisha akamwangalia kaka yake... "kaka kila mwezi unafanya check up kuna kitu kiko tofauti mwilini mwako?"
Ed akamwangalia na hakujibu swali lake lakini akamwambia, "Ungeniambia"
"Ungeniamini bro?" Derrick akamuuliza huku akinua jicho lake..
Edrian akashusha pumzi, akakumbuka ile wiki nzima baada ya harusi ya Brian alishangaa jinsi ambavyo Derrick kila asubuhi alikuwa akimpelekea kikombe cha maziwa na jioni kabla ya kulala alikuta kikombe cha maziwa kwenye meza ya chumbani kwake. Na hii ilimfanya Ed kujisikia vizuri kwa kuona mdogo wake akimjali.
Akatabasamu kidogo, "basi sawa D, inawezekana nisingekuamini. Hii taarifa nani mwingine anaijua?"
"Ni mimi tu na Emmy. Niliogopa kumwambia stori nzima bro Li sababu yeye aliamini mnapendana sana na si vyema kuingilia. Kumbuka wewe kuwa pamoja na Lyn ilikuwa inampunguzia kupokea kelele nyingi kwa mama..lakini tulifurahi kuona walau umeamua kuishi maisha zaidi ya kazi yako"
"Oooooh sawa. Basi naomba ibaki hivyo hivyo asijue mwingine. Unamuamini Emmy?" Ed akauliza japokuwa anamfahamu Emmy ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa Derrick. Walikua pamoja japokuwa Derrick alimpita kidogo Emmy
"I trust her bro. Huyo ni benki yangu ya siri" Derrick akamjibu huku akiachia tabasamu lake laini..
"Okay. Unaweza kunisaidia kumwangalia Aretha? nataka kumfahamu zaidi. Naomba uendelee kuwa karibu nae.. lakini....."
Akasita kabla ya kuendelea na kumfanya Derrick atabasamu na kusema
"Usijali bro, ni rafiki yangu na hakuna cha zaidi.!"
"Ha ha ha kweli.... lakini usiibe picha zake tena kuniletea... msaidie aweze kupata soko la kazi zake" Ed alicheka maana hakutaka kumaanisha alichowaza mdogo wake japokuwa alitamani kumwambia hivyo
"Hakuna shaka bro, nitaona cha kufanya. Huko chuo nina mtu wangu hawezi niangusha kuhakikisha yuko salama" Derrick aliongea kwa msisitizo akionesha namna alivyofurahia kutajwa kwa Aretha kwenye mjadala wao...
"Mtu wako mwanaume?" Akauliza Edrian pasipo kuficha sura ya wivu iliyoonekana wazi usoni kwake...
"He he he bro usiwaze hata kidogo, huyo Charlz hana shida kabisaaa."
"Okay." Ed akajibu akijitahidi kutoonesha dhahiri kuwa ana wivu wa wazi!
Mazungumzo yao yalipoisha Derrick aliondoka na kumuacha Ed ambaye wakati huu alichukua simu na kumpigia Lyn..
"Hello babe" sauti ya Lyn upande wa pili ilisikika..
"Bado uko hapo?" Sauti ya Ed ilikuwa ya utulivu lakini iliashiria hasira
"Ed unanifukuza?" Lilikuwa swali la Lyn
"Jibu swali langu kwanza Lyn..nimekuagiza uondoke wakati natoka hukunisikia" Ed alijitahidi kuzungumza kwa utulivu kabisa
"Ed siondoki mpaka uje. ..ulisema jioni tutaongea...eeh. nakusubiri babe" Lyn alipomaliza hakusubiri Ed ajibu akakata simu..
"Mhhhhhh" Edrian akashusha pumzi huku vidole vyake vikichua paji la uso wake kabla simu yake ya mezani kuita, akabonyeza na kusikiliza
"Bosi kuna mgeni kutoka Wizarani.."sauti ya Loy ilisikika
"Okay ..mruhusu" Ed alipomaliza akajinyoosha na akaondoa zile glasi za juisi na kuziweka juu ya jokofu.
Mlango ukafunguliwa, akaingia mwanamke mmoja mzuri wa sura, akiwa amevalia nguo zilizoonesha kuwa ni sare ya ofisi; shati rangi ya njano na sketi fupi rangi ya kahawia. Na urefu wake wa wastani hakika viatu alivyovaa vilimuongeza hata kumfikia Ed. Nywele zake zilisukwa rasta ambazo zilikuja katikati na kufanya mkia wa farasi uonekane. Uso wake ulionekana kuongezewa vipodozi vilivyomfanya kuwa mrembo zaidi.Mkononi alishika mkoba pamoja na faili.
Ed akanyoosha mkono kumsalimia mwanamke yule ambaye nae alionekana kuwa kwenye bumbuwazi la kumtazama Ed hata kusahau kuwa hawajasalimia
"Aaah sorry, habari ya mchana!" Akashtuka yule dada na akamsalimia Ed
"Salama, karibu sana" Ed akamkaribisha huku akimuelekeza kiti cha kukakaa na yeye akaenda kukaa kiti chake nyuma ya meza huku wakiangaliana uso kwa uso na yule dada akisababisha yule mgeni wake akwepeshe macho yake mara kwa mara
"Karibu," Edrian alirudia makusudi ili kumshtua mgeni wake ambae alisahau kujitambulisha akimezwa na mazingira