Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 62 - NAJUA KUZICHEZA KARATA ZANGU

Chapter 62 - NAJUA KUZICHEZA KARATA ZANGU

Baada kuelekea vyumbani kwao, Joselyn aliyekuwa amekaa muda wote akiangalia Tv, aliinuka na kuizima. Akavuta hatua kuelekea juu ambapo badala ya kwenda mpaka chumba cha wageni alichofikia akaelekea chumbani kwa Ed, ghafla akakunja kulia na kuingia korido iliyoelekea chumbani kwa Derrick, alijua kabisa kwa muda huo shemeji yake hatakuwa amefunga mlango.

Akausukuma taratibu bila kupiga hodi na wakati huu maji yalisikika bafuni. Akajua Derrick anaoga, akakaa kitandani akimsubiri.

Baada ya dakika chache mlango wa bafuni ulifunguliwa na Derrick alitokeza akiwa amefunga taulo kiunoni. Alishtuka kumkuta Joselyn amekaa kitandani kwake, akainua macho kumtazama kwa dharau,

"Unataka nini?" Aliuliza

"He he sitaki kitu nimekuja tu kukuonya shemeji" alijibu Joselyn huku akimuangalia sana Derrick macho yaliyonesha unafiki

"Ondoka chumbani kwangu" alisema Derrick huku akichukua shati na kuvaa.

"Sikia D, chochote kibaya unachopanga kumwambia Ed, ahirisha." Alisema kumtisha shemeji yake.

"Unachoogopa nini kama hakuna jambo baya unafanya Lyn?" Alimuuliza huku akishika kitasa cha mlango na kufungua akimpa ishara atoke.

"Sina kibaya nachofanya ila najua unanichukia na unaweza nitungia uongo" alijibu huku akisimama na kumfuata Derrick

"Huna la maana nipishe nilale"alimjibu

Joselyn alionesha kukerwa na jibu hilo, akafika alipokuwa na kumgusa mashavuni

"Najua kuzicheza karata zangu usidhani ni mjinga. Unajiona sana kwa kuwa kaka yako anakupenda. Watch out D"

Derrick aliusukuma mkono wa Joselyn kisha akamkaba shingo kwa hasira lakini alipoona Lyn anatabasamu tu akamwachia, akamsukuma nje ya chumba chake na kufunga mlango.

Joselyn akacheka na kushuka ngazi taratibu akielekea mlango wa kutokea. Alikutana na dada wa kazi akimalizia kuiweka vyema sebule.

"Dada Lyn unaondoka?" Aliuliza Zena

"Nibaki nafanya nini wakati Ed hayupo, mliobaki hamnihusu" alijibu Joselyn na kutoka nje na mlio wa geti ulisikika kuashiria anatoka na gari yake.

"Mpheew! Kuringa tu utadhani kashaolewa" alijisemea Zena na kumalizia kuzima taa za ndani na kuelekea chumba chake kilichokuwa nje pembeni na mlango wa kuingia jikoni.

Usiku huu Derrick hakuweza kulala vyema, aliwaza namna gani atamshawishi kaka yake kumuacha Joselyn. Tangu mwanzo alikuwa na hisia mbaya juu ya nia ya Joselyn. Sasa anahitaji ushahidi kumshawishi. Lakini wakati akiwaza hivyo hakujua shemeji yake ameshamzidi hatua kwa kumsingizia kuwa alimkaba shingoni sababu ya kuingia chumbani kwa Ed. Kaka yake alishaamini kile kilichosemwa na mpenzi wake. Derrick aliumia kwa namna ambavyo kaka yake ambaye anamheshimu kumhukumu pasipo kumsikiliza.

Derrick aliazimu kumfuatilia zaidi Joselyn na kuhakikisha pete ya kaka yake haitaingia katika kidole cha mwanamke yule.

Aliondoka katika nyumba ya kaka yake na kuelea Heaven Apartment moja ya nyumba zinazomilikiwa na familia yake, alishukuru kuwa pamoja na kile kilichotokea bado ana uhakika kuwa kaka yake ni mtu mwema.

Karata alizozitupa Joselyn aliamini kuwa atazilipa kwa mafungu, kwa msaada wa kaka yake Li.

************************************