Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 60 - CHAGUO LAKO

Chapter 60 - CHAGUO LAKO

Akainuka na kutoa ile sinia iliyobeba kifungua kinywa na kuiweka kwenye meza iliyokuwa pembeni. Akarudi kukaa.

"What is this.....nimepaliwa kusoma ujumbe tu"

Tik Tik...macho yakarudi kwenye simu kuona nini Retha alitaka kumuuliza..

"Rian nisamehe lakini naomba kuuliza, yule dada niliyepanda nae gari ndio mwanamke ulimuongelea kwenye kipindi cha siku ile?"

Mkono wa Ed ulikufa ganzi ghafla... akaiangalia ile simu akijiuliza, ni kwa namna gani ajibu hili swali. Akisema hapana atakuwa amedanganya.... akakumbuka swali la Rodgers na majibu aliyoyatoa...

"Rodgers, macho ya mwanaume huvutiwa na vitu vizuri hasa tunapoongelea jinsi ya kike, hata mimi nilivutwa katika uzuri huo huo, lakini ni binti mwenye kujituma, hivyo naamini tuna sehemu tutafika pamoja"

"Aaaaaargh....nilijifunga mwenyewe" Edrian akajilaumu. Kiukweli ni kuwa jibu lile lilidhihirisha kuwa alikuwa amempata mwanamke. Akajikaza kuweza kumjibu huku akijua lazima Lyn alimwambia kitu Aretha na kusababisha swali hili leo...

"Naomba nikujibu ndio kwa sasa, ila nitaomba kukuelezea hali ilivyo kati yetu tutakapoonana jumapili Retha."

Akashusha pumzi kwa nguvu kisha akaendelea kuchambua ripoti pasipo kuruhusu hisia zake zizinge kazi yake.

Tik Tik...

"Sawa Rian.Kuhusu ile picha naomba niimalizie ilichukuliwa kabla sijamaliza"

Aretha aliandika..

Uso wa Edrian walau ukafunikwa tena na tabasamu, akajipongeza kwa kuwa hakuwa amekosea tangu mwanzo alipodhani mchoraji wa ile picha ni Aretha. Akaandika...

"Nimeshaitundika mahali pake Retha labda uje mahali ilipo,utaimalizia hapa hapa"

Edrian huu ujanja wa kupindisha mambo kwa faida yako usiutumie kwa Retha....she is so innocent.....Ha ha akacheka taratibu alipojisemesha mwenyewe..

Tik Tik. ....

"Sijui kama naweza kufanya vizuri. Nimezoea studio yangu" Aretha akaandika

"Nitaweka mazingira kama ya studio yako ili uweze kuimalizia, hapo unaonaje?" Ed akamjibu

"Okay. Asante kwa muda ulionipa Rian" akaandika Aretha

Akaandika 'anything for you Retha' lakini kabla hajautuma akashtuka na kufuta

Asije akaniona kama nina ajenda ya siri akajionya mwenyewe kisha akaandika

"Asante pia kunipa muda wako Retha"

Akabaki anaiangalia simu yake kwa muda kisha akaendelea na kusoma ripoti zake

Tik Tik....

"Sawa. Kesho nitamtembelea mama kama alivyoniomba" Aretha akaandika

Ed akatabasamu kwa kuwa alishangaa kwa jinsi Aretha alivyokuwa na uhuru kuandika tofauti na wakionana. Labda ni aibu sijui...ngoja nifanye kile kilicho rahisi kwake. Aretha ni mwepesi kwenye ujumbe wa maandishi tofauti na mazungumzo ya ana kwa ana...

'

"Sitakuwepo, ila relax, au utajisikia vizuri Derrick awapo? Naweza kumuomba."

Aishhhhh, Derrick anaelewana na Aretha tangu mwanzo...je kwani lazima Ed amuombe mdogo wake ampe kampani? Anaweza kumwambia mwenyewe. Akalitupia mbali wazo lile baada ya kuona anavyomjali...

Tik. .Tik

"Asante sana, nitamuomba leo baadae..kazi njema" Aretha akajibu

Haikupita muda Ed akawa amemaliza kumjibu.

*************

Mida ya mchana Ed alipata chakula akiwa ofisini kwake mpaka Derrick alipofika kama walivyokubaliana.. Baada ya salamu Derrick akaelekea moja kwa moja kukabiliana na kile kilichomleta ofisini kwa kaka yake mchana huu

"Kaka najua ni muda umepita lakini naomba ujue tu sina nia mbaya na Lyn. Inawezekana anakupenda lakini sidhani kama amejitoa kwako asilimia 100 kama wewe ulivyojitoa kwake"

"Lyn ni mwanamke mzuri, hata mimi mara nilipomuona nilifurahi kuwa unajua kuchagua"

"Mmmmmm" Ed akaguna huku akimuangalia mdogo wake kwa jicho la 'unasemaje'

"Kuna vitu vidogo vilinitia mashaka hasa anapokuwa nawe ni mtu tofauti na anapokuwa na mtu mwingine. Tena sipendi mtu asiyeheshimu utu wa mtu wa kipato cha chini"

"Nilivumilia nikajua ni chaguo lako... lakini siku moja baada ga mizunguko yangu, kilipita katika mgahawa mmoja na bahari mbaya tukagongana nae" Derrick akaanza kumsimulia tukio lilivyokuwa baada ya kukutana na Lyn na hata kupelekea sintofahamu iliyopelekea yeye kuondoka nyumbani kwa amri ya kaka yake Edrian..

Mazungumzo yao yaliendelea huku Loy akiwa amewaandalia juisi nzuri ya nanasi...

Derrick akamsimulia ilivyokuwa wiki tano kabla...