Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 61 - SURA MBILI

Chapter 61 - SURA MBILI

Derrick Simunge akiwa katika harakati zake za kuangalia fursa katika sekta ya utalii, aliingia kwenye mgahawa maarufu hapa A-Town. Mahali ambapo watalii wengi hupenda kukaa kutokana na huduma yake ya vyakula tofauti kutoka mataifa mbali mbali. Watu maarufu pia walipenda kuja kukaa katika mgahawa huu, mandhari yake hasa wakati wa machweo ingekuvutia bila shaka. Seasonal Restaurant.

Derrick alikaa kwenye kona moja ya mgahawa huu, na mhudumu wa kike alimsogelea kuchukua oda yake. Ukweli ni kwamba Derrick ana handsome face, ambayo kwa msichana yeyote lazima amkubali kwa kumuangalia tu. Ndugu zake humtania kwa sababu ya kukaa tumboni na dada yake basi atakuwa aliiba sehemu ya uzuri wa dada yake. Tofauti ya Derrick hakuwa play boy, lakini kama angelitaka basi asingesumbuka kujitwalia yeyote amtakaye.

Oda ya chakula ilipokuja alimshukuru yule mhudumu ambaye alibaki amesimama akimwangalia Derrick huku akitabasamu.

Derrick hakumsemesha alitabasamu na kuendelea kula chakula chake mpaka aliposhtushwa na sauti ya kicheko laini ambacho alikifahamu. Aliinua uso kumuona mwenye kucheka, macho yake yaligongana na ya Joselyn aliyekuwa ameshika mkono wa kijana mmoja wa kiasia, walikuwa wakielekea kwenye eneo la VIP. Eneo hili lilikuwa ni vipande vilivyokatwa kama vyumba ili kuwaruhusu watu maalum kukaa peke yao bila kusumbuliwa na kuonekana na watu wengine.

Joselyn aliuachia mkono wa yule kijana na kumushiria atangulie atamfuata baada ya muda mfupi. Joselyn alipiga hatua hadi alipokuwa,

"Hellow shem D, what are you doin here?" Aliuliza Lyn

"Eating" alijibu kwa ufupi na kuendelea kula

"Ooh, that man ni class mate wangu tulisoma wote. Usifikiri vibaya sawa eeh?"

Derrick aliinua macho na kumuangalia Joselyn kisha akamjibu,

"Sifikiri chochote"

Akaendelea kula, Joselyn akasonya na kumwambia

"Unaringa sana Derrick, sitaki uanze kumjaza uongo Ed. Umeniona hapa yaishie hapa"

"Okay" alijibu Derrick na kuendelea kula.

Baada ya kuondoka Joselyn, Derrick aliinua macho kumuangalia hadi alipopotea kwenye kona. Akamalizia chakula chake na kumsubiri mhudumu amletee bili, haichukua muda mrefu yule binti akarejea na bili. Wakati akitoa pesa kwenye pochi yake yule mhudumu alimuuliza

"Samahani unafahamiana na Joselyn?"

Derrick akainua macho na kumjibu

"Kiasi tu.. wewe unamfahamu?"

Yule dada alitabasamu baada ya kuona Derrick kamuangalia kwa tabasamu, akamjibu kwa sauti ya kunong'ona

"Ni mteja wetu yeye na yule mtu wake"

Derrick aliposikia hivyo alijisikia vibaya lakini hakutaka kuonesha akampa ishara yule dada amsogelee kisha akamwambia

"Aahmmh huwa anakuja hapa mara nyingi?"

Yule dada akajibu kwa hofu

"Meneja hapendi tuseme taarifa za wateja."

Derrick akamuangalia kwa yale macho yake ya kubembeleza

"Please"

Yule mhudumu akaangalia alipokuwa meneja wake na kuona yuko busy akamjibu

"Mara nyingi huyo kaka anapokuwa mjini, maana nasikia anaishi SA ."

"Okay asante, keep the change". Alimshukuru na kuinuka kuelekea nje, akimuacha yule dada akitabasamu. Alichukua helmet yake na kuvaa kisha akaondoka na pikipiki yake.

Alielekea mpaka ofisini kwa Linus ambaye siku zote huchelewa kurudi sababu ya kusubiri hesabu ya maduka ya kubadili fedha.

Baada ya kusalimiana akamwambia

"Kaka Li, Big bro anahitaji kumjua vyema Joselyn, sina hakika lakini nimemuona akiingia sehemu na mtu mwingine"

Linus alishtuka kusikia hivyo, japokuwa siku zote alihisi Joselyn si innocent kama anavyojionesha bado aliamua kutoingilia sana. Sasa leo mdogo wake kalithibitisha.

Baada ya kumpa maelezo, Derrick akamwambia wampigie simu Ed, lakini Linus akamkumbusha kuwa mikutano aliyoenda Ed ni ya muhimu, akirudi watamwambia. Linus alijua kuwa itakuwa vigumu kumthibitishia Ed hizi habari lakini aliona vyema wamsubiri arudi. Ed angewasili alfajiri ya siku ya Ijumaa. Walikubaliana na wakaamua kuendelea kumpeleleza Joselyn.

Walipoelekea nyumbani siku hiyo ya Jumatano usiku walishangaa kumkuta Joselyn akiwa amekaa sebuleni. Wakamlaumu Ed kumpa ruhusa ya kuingia na kutoka atakavyo.. Baada ya salamu walielekea mezani kupata chakula kabla ya kila mtu kuelekea chumbani kwake.