"Aretha samahani naomba nikuone" Ed akajikakamua na kumuita Aretha ambaye aliona aibu baada ya kukutana na uso wa Ed akijaribu kuchungulia....
Ed alisimama pembeni mbele ya gari, hisia zake zilikuwa moto sasa na hakujua kwa nini akimuona Aretha anajisikia hivyo.
Alipenda macho yake, tabasamu la Aretha lilimfanya asikie raha kumwangalia.. bado alivutiwa na soni nyingi usoni kwa binti huyu, hasa alipojaribu kuyakwepesha macho yake....
"Oooh God nampenda tu hata sijui kwa nini" akajisemea moyoni...
"Ammhhm.... "Aretha alimshtua Ed ambaye alikuwa amehama mawazoni
"Nahitaji kukuona, please niwekee ratiba hii wiki" akajikaza kuyasema maneno haya... hakutaka kumpa sura tofauti binti huyu. Alitaka walau apate muda wa kuongea nae kwa ukaribu
Akiwa anaangalia pembeni Aretha akakwama tena..."ammhhh... lini?"
"Jumamosi?" Akauliza Ed
"Mama yenu aliomba nimtembelee jumamosi...sijui nitatoka saa ngapi?" Akajibu Aretha..
"Jumapili je, pleasee?" Ed akamsihi Aretha...kwa uungwana wake asingeweza mlazimisha.
"Aaamhhh... haya"
"Asante sana....nitakupigia kukujulisha muda" Ed kwa furaha akamwambia
Aretha akaitikia kwa kutikisa kichwa, uso wa Ed ukang'aa kwa tabasamu..
"Usiku mwema...Retha"
"Nawe pia" akajibu huku mshangao ukiwa wazi machoni pake kusikia Ed akilifupisha jina lake akabaki amesimama pale pale...
Sekunde 10 zikapita, sio Ed wala Aretha aliyeondoka..Ed akawa wa kwanza kushtuka
"Goodnight." Ed akaaga tena.. "aisee nina mpango kuaga mara ngapi" akajihoji Ed moyoni
Aretha akamwangalia alipoelekea kwenye gari na kuingia. Miguu ya Ed ilikuwa mizito akitamani kutokupoteza nafasi iliyokuwa mbele yake. Akawasha gari na kuondoka, bado akimpungia mkono Aretha... "Gosh, am too much... why am I acting like this" maswali yalikuwa mengi kichwani kwa Ed. Kila alipokutana na Aretha ni kama dunia yake iliporomoka na kujikuta anakuwa mtu mwingine kabisaaaa.
"Call Young Dereck" akatoa amri kwenye simu yake impigie Derrick... ikafanya vivyo hivyo na mara moja simu ikaita. Alikusudia kumshukuru ndugu yake kumtengenezea mazingira ya kuaminiwa na mama wa Aretha...lakini alitamani kujua nini Derrick na mama huyu walizungumza.
*********************
Jana yake......
Jumatatu usiku baada ya Aretha kurudishwa na Ed usiku........ Mama yake Aretha akiwa chumbani kwake alichungulia dirishani baada ya kusikia mlango mdogo wa geti ukifunguliwa. . Akataka kuhakikisha ni Aretha, alipomuona moyo wake ukafarijika lakini kabla ya kurudisha pazia, kuna jambo likavuta macho yake hata akasogea dirishani tena.
Aretha alipomaliza kufunga mlango mdogo wa geti, alisimama na wakati huo rasha rasha za mvua ziliendelea kumwagika. Mama yake alidhani binti yake angekimbia haraka ili asilowane.. lakini Aretha alisimama akalitoa lile koti ambalo Ed alimfunikia kichwani. Akaliangalia halafu akalikumbatia huku akivuta harufu kana kwamba alikosa hewa, macho yake akafumba kama mtu mwenye kutafakari kitu. . Alipoachia akatabasamu na kujiweka koti kifuani na kukimbia kuelekea ndani.
Mama yake akawa kama aliyepigwa na radi. ..mkono wake ukiwa kwenye pazia, maswali yakatiririka ndani yake...
"Ni nani mwenye koti hili, Derrick au kaka yake aliyemleta?"
"Binti yangu amempenda mwenye hili koti tangu lini, na mbona sikugundua mapema?"
Aliposhtuka Aretha alikuwa akigonga kwenye mlango wa mbele wa nyumba..akarudisha pazia na kuelekea mlangoni tayari kumfungulia.
Baada ya kufungua Aretha aliingia huku akilificha koti mama yake asilione. . Mama naye akaamua kumuacha binti yake apite bila kumhoji.. akatikisa kichwa na kucheka moyoni...
"Hivi binti yangu anajifichia nini wakati mimi walau napata furaha kumuona katika hatua hii ambayo nahisi amechelewa." Aliwaza mama huyu!
Akaamua kumgongea binti yake, akasikia purukushani kabla ya Aretha kufungua mlango
"Mama...." alijibu akihema kana kwamba alivamiwa..akiwa amesimama huku mlango kaufungua nusu. .
"Retha... naomba tuongee" mama alijibu kwa upole kiasi cha kumshtua binti yake ambaye sasa alisogea na kumruhusu mama yake apite...
Mama akaelekea hadi kitandani na hakuacha kuona koti alilokuja nalo binti yake