Anakumbuka alimuuliza kama yuko sawa lakini kabla hajamjibu Tulya akaitwa ndani.
' itakuwa kitu kina msumbua au kweli kapata mwanamke mwingine?' anajiuliza.
' lakini kupata mwanamke hakuwezi kumsumbua kwani ni jambo la kawaida mwanaume kuoa mitala hata mke wake hawezi kupinga,
lakini mbona bado wanapendana sana na mke wake? labda itakuwa uchovu tu Wakutoka mawindoni"
Anapotezea mawazo yake na kurudi kuongea na wenzake.
" na nyinyi mmeshaolewa tutawaona mtaweka wivu wenu kwenye ghala gani ili usitoke" Malimbe anawaambia.
" bado tuna mda sisi" Sinde anajibu.
" Mimi mnitoe" Tulya anajibu kichwa juu kwa majivuno ya ushindi kuwa hawezi olewa mitala.
Malimbe na Ntali wanaondoka wakimwacha Tulya na sinde.Tulya anatabasamu baada ya kuona mwendo wa rafiki yake hauko sawa ambao ameshauona kwa mda mrefu.
" mwanamke wa moto wewe?" anaongea akitabasamu.Sinde anamwangalia anamuona Tulya uso wake ukiwa umejaa utani na nyusi zake zote mbili akizichezesha.
" nini?" anamuuliza.Tulya anacheka " hapana nilitakiwa niseme mumeo wa moto,ninavyokumbuka jana alisema amechoka anaenda kupumzika lakini kwa mwendo wako unaonyesha tofauti"
Sinde anamuelewa ana maanisha nini." kwa nini usikae kimya tu Tulya jamani" anamjibu akiangalia huku na kule macho yake yanakutana na ya Tinde aliyekuwa anamwangalia anageuka haraka.
Tulya anangalia alikoangalia Sinde anamwona Tinde bado ana mwangalia ndugu yake anatabasamu na kumsogelea Sinde.
" Nina uhakika anatamani kutufukuza watu wote hapa ili akurukie tena" Tulya anajisikia raha kumtania rafiki yake na ndugu yake.
" niambie ilikuwaje?" anauliza kwa shauku.
" siku nyingine bwana Tulya huoni watu wote hawa"
" niambie bwana,unakuja hiki ndio kilichonileta hapa" anasisitiza Tulya macho yake yakionyesha uchu wa umbea.
Sinde anavuta pumzi ya kukata tamaa anajua rafiki yake king'ang'anizi hataondoka mpaka apate anachotaka.
Anaangalia kama Amna mtu karibu Yao anasema " tayari umeshasema mpaka Sasa anatamani kunirukia,utakuwa umeshajua nime mfanya nini"
" mwanamke mbaya kweli wewe,tayari ulishamchanganya mtoto wa watu,umeenda kumpa nini tena?" anauliza Tulya sauti yake ikiwa imejaa utani na umbea.
"ndio maana nimekwambia hii tunatakiwa kuwa wawili tu nikuonyeshe kwa vitendo halafu tucheke kwa nguvu pasipo kuonekana wa ajabu,mwenzako bado mwali ujue"
" sawa,nitakuja kesho Ili tuje tusimuliane vizuri" Tulya anamjibu akiamua kuacha umbea wake wa kutaka maelezo ya usiku wa ndoa ya mwenzake kwa Sasa.
" mhh,niambie nasikia jana ukaleta kizaa zaa mpaka mumeo akakuvurumusha ngomani" Sinde anamuuliza.
" umeshasikia tayari,mwali mmbea wewe"
" wifi yangu kaniambia asubuhi nasikia isingekuwa Nzagamba ungeshinda,hajakupiga kweli nasikia alikasika sana"
" ungeniona na ngeu hapa kama Lindiwe" anamjibu.
" kweli,niambie ikawaje?" Tulya anatabasamu akichezesha mabega yake na kusema.
" alikuwa na wivu"
" nini?" Sinde anabwatuka kwa nguvu watu wanawaangalia
" shhhh,kwa namna hii itabidi na hii tuongee kesho" Tulya anamjibu akiangalia huku na kule.
" hapana niambie Sasa hivi,siwezi kusubiria hiyo mpaka kesho itaniua" Sinde anamjibu akimvuta mkono na kuzunguka nae nyuma ya nyumbani mbali kidogo na watu.
" niambie, Nzagamba alikuwa na wivu?!" anauliza baada ya kuona mahali walipo ni salama.
" Sasa unaelewa kwa nini Mimi sikutaka kusubiria kesho?"
" achana na hilo elezea ilikuwaje mpaka Nzagamba akawa na wivu?"
" unajua Mimi nilikuwa nacheza nikiwa nimenogewa na ngoma nimeshtuka tu navutwa mkono kuangalia nikaona ni Nzagamba.."
Tulya anamuelezea Kila kitu mpaka walipofika nyumbani na kugombana mpaka Nzagamba alipokuja kumbembeleza.
"ooh mizimu ya mababu zangu! Tulya umefanikiwa kumtega Nzagamba,natamani ningemuona Nzagamba akiwa na wivu" Sinde anajibu macho yake yakionyesha kuota ndoto ya mchana.
" mwenyewe hakujua hata kama ana wivu alisema tu hataki kuona wanaume wengine wakiniangalia kama chakula Cha sherehe" wote wanacheka.
" na unajua Jana BB baada ya kugombana ilikuwa kidogo tufanye lakini.."
Sinde anadakia kimbea " lakini nini?"
" bibi sumbo akaharibu" Tulya anaongea akivuta pumzi ndefu utadhani kanyang'anywa tonge mdomoni.
" kivipi?!"
Tulya anamuelezea Kila kitu " nampenda mama mkwe wako lakini kwa Jana nahisi kumchukia" Sinde anasema baada ya kusikia maelezo ya Tulya.
" Mimi pia,kidogo lakini kwa sababu alitoka kujua kama tupo sawa sababu hiyo inanifanya kidogo nimvumilie" wote wanacheka.
" Sasa kuhu.." kabla Tulya hajaendelea anafika wifi yake Sinde mschana wa miaka kumi na nne akikimbia sura yake tu inaonyesha alivyo machachari lakini mwenye roho nzuri.
" wifi,wifi " anaita.
" pole pole Sia utaanguka" Sinde anamkanya,Sia anafika na kusimama walipo.
" wifi unajua mwana wa mtemi amefika kijini kwetu"
" nini?!" Sinde na Tulya wanauliza kwa pamoja.
" ndio na watu wote wanaekekea huko kumwangalia" Anajibu Sia
" unaongea ukweli?" Tulya anauliza.
" ndio twende na sisi tukamwangalie " Sia anamvuta mkono wifi yake tayari kuondoka.
" ndio twendeni,sijawahi ona msafara wa mwana wamtemi au mtemi" Tulya ansema.
" Mimi pia" Sia anajibu akimvuta mkono wifi yake lakini Sinde hasogei.
" Twende unashangaa nini?" Tulya anamuuliza." manjua leo siruhusiwi kutoka"Sinde anawajabu akitabasamu na Sia anamwachia mkono.
" ohh,nilisahau" Sia anasema.
" hata Mimi" Tulya nae anajibu.
" nendeni mtakuja kunisimulia" Sinde anawajibu kwa tabasamu.
" nitakuja kukwambia Kila kitu wifi" Sia anasema na kumshika mkono Tulya.
"tutaonana kesho" Tulya anamjibu akianza kuondoka na Sia kiherehere Cha kuangalia msafara wa mwana wa mtemi kikionekana usoni mwake.
Mbali na hapo katika boma ya Nzagamba na mama yake mlango wa nyumba ya Bibi sumbo unafunguliwa anatoka mwenye mji huo.
" naenda kuchukua tu ule ukindu nilioacha jana nawahi kurudi,nikiweka rangi nitabakiwa na kazi Moja tu ya kushona ule mkeka.
Anajitengeneza vizuri anaangalia mlango wa nyumbani ya kijana wake na kuvuta pumzi ndefu.
" akiniona huyu ataanza kuongea na atanizuia kutoka,wanataka kufanya wazee tuonekane hatuna kazi" Anaangalia njia na kuamua kuzunguka kupitia uwaani.
Baada ya mwendo wa kutembea na kupumzika Bibi sumbo anafanikiwa kuvuka mto na kupita ng'ambo ya pili.Anasimama kwenye kivuli cha mti mkono wake ukienda kiunoni baada ya kuhisi mfupa wa kiuno chake mkono wa kushoto ukianza kuvuta.
Anapeleka mkono wake na kuukandamiza kidogo sauti ya maumivu inamtoka.
" niliangukia huu mfupa Jana usiku,nikirudi nitapitia kwa mzee Ndumbe akanipe miti shaba ya kupaka hiyo itasaidia haraka.
Anatafuta mti mkavu na kufanya mkokonjo wake.Baada ya kupata mguu wa tatu mwendo wa Bibi sumbo unakuwa afadhali na maumivu yakipungua kidogo safari yake inaendelea.
Haikumchukua mda mrefu na kufika eneo liliojaa ukindu,anazunguka na kwenda kwenye kichaka kidogo anainamana na kutoa ukindu uliofungwa kwa katani.
" mmmmh,haujaharibika ungejikunja ingekuwa sawa na kazi bure" anajaribu kuubeba akilinganisha uzito wa mzigo.
" sio mzito sana" anaangalia shamba lililojaa ukindu na kujisemea " eneo lile kule halijakatiwa kwa mda mrefu na wa mama wa siku hizi wanakuja kukata wanavyojisikia na Mimi nikienda sidhani kama nitarudi hapa hivi karibuni,si utaharibika ule" anaongea akitikisa kichwa akiuonea huruma ukindu.
" sababu nimeshafika hapa ngoja tu nikate ule uliokomaa chini niuache ambao bado teke mpaka nitakaporudi huo utakuwa haujafikia hatua ya kuharibika,kuhusu kubeba nitauweka tu mgongoni kwangu na huu nitajitwisha kichwani"
Anainama na kuchukua kisu chake kidogo alichokificha chini ya kichaka anarudisha ule ukindu chini ya kivuli maana ukikaa juani na kukauka ukiwa umefungwa ungeharibika.
" subirini hapa nakuja"
Anapiga hatua na kuelekea mwisho kabisa wa shamba karibu na pori anainama na kuanza kukata ukindu akikusanya na kuuweka mahali pazuri.Kutokana na uzoefu wake mikono yake ilikuwa inakata haraka haraka.
Anaona ukindu mmoja ukiwa umeharibika anauufuata.
" Amna mtu atakayejua kama ulikuwa mzuri na ulikuwa wa thamani kwa Sababu umeoza na unanuka hufai kwa matumizi unatakiwa kwenda unakostaili"
anaongea na kuung'oa ukindu huo.
"unanizungumzia Mimi au?"
Anasikia sauti nyuma yake na kumfanya atulie mahali alipo.
**** usisahau kuacha comment yako kwani ni muhimu sana kwangu****