Chereads / penzi la bahati / Chapter 66 - chapter 65

Chapter 66 - chapter 65

Mkusanyiko mkubwa wa watu ukiwa una mzunguka mwana wa mtemi vichwa vyao vikiwa vimeinamishwa chini kwa heshima lakini macho yao yakiwa yamejaa udadisi na maswali mengi.

Wengi wakijiuliza ni kitu gani kimemleta mwana wa mtemi kijijini kwao? kwani sio kawaida na wengine wakiwa na wasiwasi kuhusu usalama wao kwani pindi familia ya kitemi ikifika mahali damu lazima imwagike.

'Kuna mtu kakamatwa anaongea upumbavu tena au?'

' Kafuata nini hapa?'

'kwa nini hasemi kitu?'

Wakati maswali haya yakiendelea kupita miongoni mwa wanakijiji waliojaa wasiwasi Tulya aliyekuwa miongoni mwao anajaribu kuweka sura yake sawa kwani shingo yake na mgongo vimeanza kumuuma kutokana na namna alivyo kaa kwa mda mrefu.

kwani alikuwa amesimama nusu kuinama nusu kusimama shingo yake kichwa chake kikiwa kimeinamishwa chini kufanya misuli ya shingo yake kuanza kuchoka ikifuatiwa na uti wa mgongo.

' huyu mshenzi anapanga kutufanya vichuguu au?!' anajiuliza hasira zikoanza Kumpanda.

' kuwa mtoto wa mtemi ndio kumpe kiburi namna hii,haoni kama Kuna wazee hapa?'

Anaangalia huku na kule anaona sio yeye tu watu wengi waliozunguka eneo hili wamechoka kuinama kwani imekuwa ni dakika kumi tangu wakae namna hiyo pasipo mtoto wa mtemi kutoa amri ya wao kuinua vichwa vyao.

' anatuadhibu au?' wengi wanajiuliza.

Tulya anapata tatizo lingine tena kwani miguu yake inaungana na kiuno na uti wa mgongo na shingo kulalamika kubadilishiwa mkao.

' ningeendelea na mambo yangu haya yasinge nikuta' anajilaumu kwa kujitafutia mwaliko wa adhabu asiyojua kosa.

' labda atakuwa ameondoka na sisi tunaendelea kusimama hapa kama fisi aliye ahidiwa mfupa?' anajiuliza kwani kutokana na ukimya huu inaweza ikawa ni wao tu waliyeko maeneo haya.

' au atakuwa amelala?' anajiuliza na wazo linamjia kichwani,anaanza kunyua miguu yake na kukanyaga kwa kishindo Ili kumshtua mwana wa mtemi kama atakuwa amelala.Baada ya kujaribu kama mara tatu pasipo mafanikio anaamua kuja na wazo la kuchungulia.

Taratibu ananyanyua sura yake anahakikisha yuko makini asishtukiwe na mtu yeyote au hata hao walinzi wa mwana wa mtemi wasimuone.

' kama ameondoka nitawaepusha Hawa wazee na ganzi ya misuli'

Anaendelea kujiiba kunyanyua sura yake.' Niko huku mbali nikichungulia hakuna atakayeniona'

Ananyanyua kichwa taratibu akielekeza upande alikosimama mwana wa mtemi macho yake yakipita miguu ya watu wengine na kufika umbali aliko simama mwana wa mtemi ananyanyua uso wake kuangalia juu haraka Ili awahi kuficha sura yake pale atakapo kamatwa.

Lakini anarudisha kichwa kwa staili ileile aliyotoka nayo baada ya macho yake kukutana na mwanaume aliyekuwa anamwangalia tayari.

' amenikamata! nimekwisha!'

Jasho jembemba linaanza kumtoka baada ya kusikia hatua za mtu zikija mahali alipo.

' kwa nini usiache kusabibisha matatizo hata siku Moja Tulya?'

Anajifokea mwili ukimtetemeka ' Sasa Leo itakuwa ndio meisho wako,umekufa Tulya,umekufa leo'

Hatua za mtu zinazidi kusogea na mda sio mrefu anaona miguu ya mtu hapana sio mtu tu ni mtu aliyekuja kutoa hatima yake ya meisho akisimama mbele yake.

Anafumba macho yake aking'ata midomo yake kwa wasiwasi na kihoro, mapigo yake ya moyo yakipiga kama Ngoma ya harusi ya Sinde aliyokuwa anaicheza Jana na ana uhakika yasingekuwa yanapiga kwa kihoro cha kuashiria mwisho wa maisha ya mhusika wa huo moyo watu wange burudika mpaka mwisho wa sherehe.

Lakini kihoro cha mapigo ya moyo wake kina weza kufanya Kijiji kizima kukimbia pangoni na kujificha kwani kwa Sasa kinatumika kama baragumu ya kuashiria hatari na mtu yeyote asikiapo baragumu hiyo lazima ajiadhari.

" simameni"anasikia sauti nzito ya mwanaume karibu yake inayofanya mwili wake kuongezeka jasho na kuisha nguvu hapo alipo alikuwa anashikilia kamba iliyo oza wakati ana ning'inia kwenye korongo.

Maneno aliyokuwa anayasubiri kwa hamu hapo awali Sasa hayajampa hata ahuweni.

" nimesema simama" inasikika tena sauti lakini safari hii ikiwa imejaa madaraka zaidi.

Wana Kijiji Wana endelea kumwangalia Tulya akiendelea kuinama wakishangaa zaidi kwa nini mwana wa mtemi kamfuata.

Anasimama taratibu utadhani sio yeye aliyekuwa na haraka dakika kumi au kumi na tano zilizopita akilalamika misuli yake kukaza.

Ana nyanyua uso wake na macho yake yana gongana na mwanaume mrefu aliyesimama mbele yake.

Ubaridi mkubwa asijue umetoka wapi unapita na kuingia kwenye misuli ya mwili wake aliyokuwa analalamika kukakamaa .

Unapita kwenye,ngozi misuli hadi kwenye utumbo na kugandisha chakula chake Cha asubuhi alichokula na familia yake.

Lile jasho la awali la kihoro alilokuwa anahisi limeloanisha mpaka fizi zake linajikuta limekauka ghafla kama mto wa laana uliokauka ghfla wakati wa masika.

Nywele zake za kisogoni zinajikuta zikisimama na kumfanya Tulya kutamani kukimbia mbali milimani akajifiche.

" wewe ni nani?"

Anasikia mwanaume akimuuliza lakini Tulya alikuwa ameshafika mbali kuokoa uhai wake akiacha kiwiliwili chake pale alipo kuwa amesimama.

Masaa machache yaliyopita.

Tulya anaonekana akiondoka nyumbani kwake baada ya kupata kifungua kinywa na kufanya shughuli zingine za nyumbani mwendo wake ukiwa wa haraka.

' ohh, mizimu nisaidieni nimechelewa'

Nzagamba anasimama mlangoni akimwangalia mke wake akipepesuka haraka haraka kukimbizana na mda,takribani mgongo wake wote ukiwa wazi kutokana na kitambaa chake Cha kifuani alichofunga kilichokuwa na mikanda mwembamba ikining'inia.

makalio yake yakitupa sketi yake fupi kwenda kushoto na kulia kutokana na mwendo wake wa haraka.

Shanga zake kiunoni zikirushwa rushwa juu na chini anajikuta akitabasamu.

" anatamani angekuwa na mabawa" anaongea kwa sauti ya chini.

" nimekwambia Niko sawa nenda tu na mkeo" anaongea bibi sumbo aliyetoka ndani na kumwona kijana wake akimwangalia mkewe.

"hatuwezi kukuacha mwenyewe baada ya kilichotokea jana" anajibu Nzagamba macho yake yakiendelea kuwa kwa mke wake anayezidi kupiga hatua zaidi kuwa mbali na yeye ghafla hisia za upweke na hamu ya kuwa karibu nae ina mjia .

Anatikisa kichwa kujiweka sawa anageuka na kumwangalia mama yake.

" rundi ndani mama unatakiwa kupumzika" macho yake yanarudi kumwangalia mke wake anakuta ameshapotelea anageuka na kuingia ndani kwake.

" mhhh,uzee huu Sasa nimeanza kuchungwa kama mbuzi" anaongea Bibi sumbo macho yake yakienda juu kuangalia jua kama kulipima makali yake .

" haliumizi sana" anarudi na kuingia ndani kwake.

Tulya anafika nyumbani kwa ndugu yake Sinde anakuta ndugu wengine wa familia ya Tinde na Sinde wakiwa wamekusanyika nje ya nyumbani ya wanandoa wapya kwa utambulusho.

Anaenda na kukaa karibu na mama yake Runde pamoja na mjomba wake mzee Shana akiwasalimia kwa sauti ya chini.

Runde anaitikia kwa sauti ya chini huku mjomba wake akimwitikia kwa kichwa.Baada ya utambulisho ambao haujachukua mda mrefu kutokana na familia hizo kujuana kwa mda mrefu kwa kukaa Kijiji kimoja maisha yao yote watu wanatawanyika wakizidi kupeana pongezi za kuwa karibu zaidi baada ya ndoa ya watoto wao.

Tulya na Runde wanaenda kumsalimia Sinde Tulya na Sinde wanakumbatiana kwa furaha wanamsikia Runde akisema.

" hapa ndio nyumbani kwako Sasa Sinde,mambo ya kuja nyumbani kwangu Kila siku kwa sababu ni karibu siyataki" Runde anaongea na kumfanya Sinde kuzungusha macho yake juu kuchoshwa kukumbushwa mara kwa mara jambo Hilo na mama yake.Anamwachia Tulya na kumwangalia mama yake.

" anamaanisha wewe sio mtoto wake tena" Tulya anaongezea akicheka.

"nimekuwa nikisikia maneno hayo tangu nikiwa mwali,Jana karudia kama mara mia Moja na mpaka nayasikia yakijirudia akilini kama Ngoma ya mavuno" Sinde anajibu.

" ni vizuri tumeelewana binti,maana aibu sitaki ,binti mwenyewe wewe tu sitaki niambiwe nimeshindwa kukulea wakati sikuwa hata na mzigo mkubwa" Runde anamjibu macho yake na sura yake vikionyesha msisitizo.

" angalia wakwe zako mwenyewe" Sinde anamjibu akiwaangalia wifi zake wakija walipo , Tulya na Runde wanageuka kuangalia walipo." wakwe zangu wamefanya nini?" Runde anauliza akiwaangalia wakwe zake kwa macho ya kujivunia

" wako vizuri kabisa"

"mama mkwe wangu kasema hivyo hivyo" Sinde anajibu " hata wangu" Tulya anajibu wanatazamana na kucheka kwa nguvu na kufanya watu wote wawangalie.

" shhhh,hivi mtakuwa lini nyie" Runde anawakanya kwa sauti ya chini.

" kimewafurahisha nini?"anauliza Malimbe mke wa kilinge baada ya kufika walipo.

" Amna kitu,Hawa watoto sijui watakuwa lini?"Runde anatikisa kichwa kusikitika na kuanza kuondoka Sinde na Tulya wanaendelea kucheka kwa sauti ya chini.

" mmeolewa Sasa mbadilike jamani" Ntali anawaambia mkono wake ukiwa kwenye tumbo lake akili papasa.

" mbona sisi ni wakubwa,halafu sijamuona kaka Zinge?" anauliza Tulya

" sijui kaenda wapi asubuhi nimeamka simuoni" Ntali anamjibu.

" una uhakika kalala ndani?" Sinde anauliza macho yake yakionyesha utani.

" mume wangu ni mwaminifu"

" kwani Mimi nimesema kitu" Sinde anamjibu akinyanyua mabega yake.

" ni kweli kaka Zinge siku hizi simuelewi?" Tulya anaongea akikumbuka alipo onana na Zinge siku ya jana hakuwa sawa kabisa macho yake yakionyesha uchovu kama mtu ambaye hajalala .

***usiache ku comment mawazo yako kuhusu mwelekeo wa story ni muhimu na unanioatia mwanga wa kujua wasomaji wangu wanataka kitu gani,Asanteni*****