Chereads / penzi la bahati / Chapter 53 - chapter 52

Chapter 53 - chapter 52

Tulya anamwangalia Lindiwe machozi yakimlenga machoni." we si unamarafiki?" anamuuliza huku akijua kabisa kilichotokea lakini Lindiwe kazaliwa na kukulia hapahapa kwa hiyo hawezi kuwa na marafiki wachache.

" si uliwaona na kuwasikia wewe mwenyewe siku ile" anaongea Lindiwe uvumilivu ukimshinda na machozi aliyokuwa akiyazuia yana anguka na kutengeneza mfereji kutoka kwenye macho yake yanapita kidevuni na mwisho chini ananyanyua mkononi wake haraka na kuyafuta.

Tulya anaona uchuro gani huyu anamfanyia mchana kweupe namna hii." kwa hiyo ukaona Mimi ndio nakuwa chaguo mbadala?" anamuuliza kwa sauti ya kutokuamini kinachotokea hajawahi kufikiria kuwa katika maisha yake Kuna siku mtu atakuja kumlilia anataka kuwa rafiki yake.

" ndio,kwa sababu wewe ni muwazi unaweza kumwambia mtu ukweli kuliko walichokuwa wananifanyia kina Mbula,nawaeleza shida zangu lakini kumbe walikuwa wananichukulia vingine" anaongea Lindiwe sauti yake ikionyesha ni jinsi gani kitendo Cha marafiki zake kilivyomvunja moyo na ni namna gani alivyokuwa mpweke.Watu wanaweza wakadhani unacho Kila kitu kumbe una mateso yako moyoni na wakati mwingine wanatia chumvi kwenye kidonda chako wafurahi wakikuona ukifurukuta kwa maumivu.

" wewe pekee ndio,umewahi kunipa maneno ya faraja ya kutoka moyoni na wengine wote walikuwa wanafiki tu,ingekuwa mtu mwingine angetangaza kilichotokea lakini wewe hukusema"

" unajuaje kama nilikuwa nakuonea huruma tu kwa hali yako na nilikuwa simaanishi" Tulya anamjibu.

" sio siku zote mtu humtetea adui yake,siku ile nilijua wewe ni mtu mzuri,ni samehe sana kwa niliyokufanyia siku za nyuma,nilikuwa na ogopa na nikakuona kama wewe ni sehemu ya kupunguzia mawazo yangu" Lindiwe anaendelea kufuta machozi yake ambayo Kila akijaribu yanatoka mengine.Upweke ulikuwa unamua taratibu,hapati faraja kwa wazazi,majirani na wanakijijj wanaangalia Kila kinachomtokea kama kivutio na marafiki aliowaona ni sehemu ya kupunguzia uchungu wanamcheka nyuma ya mgogo wake na kufurahia kinachompata,mume wake anaona yeye ni kituo Cha kuja kupunguzia aibu yake ya kutokuwa baba kwa kutumia mwili wake.

Kitendo Cha Tulya kumtetea mbele ya marafiki zake kilimpa faraja ambayo hajaipata kwa mda mrefu.Tangu aachane na Nzagamba maisha yake hayakuwa sawa tena wengi walidhani anafurahia ndoa na Manumbu lakini moyoni alikuwa anateseka sana na hakutaka mtu yeyote ajue kwani ukweli ni kuwa alimpenda sana Nzagamba licha ya yote yaliyompata na aliamua kuvaa kinyago Cha kujifanya Kila kitu kipo sawa.

" ingia ndani" Tulya anamwambia akiinama na kuchukua kibuyu chake maana kwa msiba wa Lindiwe anaweza pita mtu akawaona yakazuka mengine.

"Asante" Lindiwe anaitikia haraka akimfuata Tulya macho yakicheza kwa furaha kama kamuona mama katoka shambani na mkungu wa ndizi.

" na hii " anaongea,Tulya anageuka na kumwangalia anamuona akimwonyesha mfuko wa shanga.

" Haina haja,kaa nayo" Tulya anaongea akiendelea kutembea.

" usifanye hivyo nimetumia siku tatu kutengeneza" anabembeleza Lindiwe.

Tulya anavuta pumzi na kuchukua mfuko kitendo Cha kumfanya Lindiwe atabasam.

"kiuno changu na chako nimeona hakitofautiani sana,ila nimeacha nafasi kama ikiwa ndogo utaongeza na kama ni kubwa utapunguza" anaongea Lindiwe akiendelea kumfuata Tulya uani ghafla Tulya anasimama na yeye anasimama.

" atakuwa kaenda wapi?" anajiuliza Tulya kwa sauti ya chini akiangalia chini ya mti alipokaa mama mkwe wake akiyapuuzia maneno ya Lindiwe.

" nimekutana nae kule karibu na mbuyu mkubwa wakati nakuja" anaongea Lindiwe baada ya kumsikia.Tulya anageuka na kumwangalia.

" mama mkwe wako,halafu alikuwa kama hayuko sawa hivi" anaongezea.

" ulimuuliza akasema anaenda wapi?" anamuuliza.

" hapana,nilimsalimia tu" anamjibu.

Tulya anaingia na kukaa kwenye kibanda Chake na kuanza kujiandaa kutengeneza udongo kwa ajili ya kufinyanga vyungu moyoni anawaza akirudi itabidi aongee na Bibi sumbo apunguze kutembea kitu ambacho amesharudia mara nyingi lakini Bibi huyu hasikij hata kidogo.Lindiwe nae anakaa kwenye kigodo baada ya kuona Tulya hamkaribishi kukaa.

Anaingia ndani kwa Bibi sumbo na kumsikia akikoroma chumbani kwake anachungulia na kumuona akiwa amelala fofofo." mmmh sijui karudi mda gani?" anajiuliza akitoka na kumwacha apumzuke.

Nje anamuona Lindiwe anayemsubiri hiyo ni baada ya kukaa na kumwangalia akifinyanga vyungu huku akimwongelesha hiki na kile Tulya nae anamjibu tu kwa sababu anamwonea huruma kumfukuza.Lindiwe alipoaga na kutaka kuondoka Tulya anamwambia amsubiri waondoke wote kwani anaenda nyumbani kwa mjomba wake kuangalia maandalizi ya harusi ya binamu yake Sinde ikiwa ni siku mbili kabla.

" unaweza kwenda mwenyewe,mama karudi yupo ndani na siwezi kumuacha mwenyewe" Tulya anamwambia.

" Haina shida,tutaonana kesho" anamjibu na kuanza kuondoka Tulya akimwangalia " kesho?" anajiuliza baada ya akili yake kutafakari alichomalizia Lindiwe.

" siamini kama anataka kuja tena!" anaongea kwa sauti akijiuliza kama Lindiwe atakuwa mgeni wake Kila siku siku zijazo huku akitafakari urafiki wao utakuwaje ukilinganisha uhusiano wa waume zao na wao wenyewe." tafarani"anajisemea Tulya lakini inaonekana Lindiwe hawazi kabisa hilo.Hajui Nzagamba atasemaje akirudi kwamba kaondoka siku chache na mke wake amekuwa rafiki na mpenzi wake wa zamani waliokuwa maadui kabla hajaondoka.

Anarudi ndani na kwa kuwa imekuwa jioni anaamua kuanza kuandaa chakula Cha jioni.baada ya kumaliza anafunika na kwa kuwa mama mkwe wake alikuwa amelala anaamua kukaa nje amsubiri aamke waje kula wote.

" harusi ya Sinde itakuwa giza" anaongea kwa sauti ya chini akijilaza kitandani macho yake yakienda juu kutazama anga lililojaa nyota pasipo na mwezi.

Akili yake inazunguka mambo mengi ikiwemo kumbukumbu za kijijini kwao na mwisho kurudi kwa Nzagamba akijiuliza sijui atakuwa anaendeleaje huko aliko.

Kitendo Cha kukosa mnyama na wenzake kumcheka tena kinamuumiza kichwa na kinachomuumiza moyo zaidi ni kuwa hatakuwepo mbembeni yake kumfariji kitu ambacho hataki kukifikiria kabisa.

" wamechukua mda mrefu kuliko tulivyofikiria"

anasikia sauti ya Bibi sumbo anaamka alipolala na kukaa akimwangalia mama mkwe wake akijikongoja na kuja kukaa pale alipo.

" umeamka?" anamuuliza akikaza macho yake gizani apate kumuona vizuri.

" uko sawa mama" anamuuliza na kumfanya Bibi sumbo kucheka kidogo.

" mmmh,usijali mwanangu sitakufa kwa ugonjwa" anamjibu macho yake yakienda juu angani.

" usiwe na wasiwasi Nzagamba Yuko sawa kuliko siku zote"

" ni vigumu kusema hivyo mama" anamjibu akiangalia njia utadhani atamuona akirudi na kichane Cha ndege mkononi kama siku zote.Umbali kati Yao ulikuwa unamuua Tulya.

" Siku sio nyingi mambo yatabadilika ni vibaya nitakuwa naangalia nikiwa upande mwingine" anaongea Bibi sumbo kama anafikiria.Tulya anamsikia pasipokujua anamaanisha nini.

" unadhani watarudi kabla ya sikukuu ya vijana ya lindo maana Wana siku ya kesho tu" anauliza Tulya.

" watarudi usijali,Hali ya hewa ya Leo jioni ilikuwa ya tofauti sana,Kuna ngome imevunjika na sio Mimi tu nilioiona mmmmh" anaongea Bibi sumbo akivuta pumzi.mbona anaongea kama Kuna tatizo linakuja na sio watu kurudi mawindoni anawaza Tulya lakini anaamua kupotezea.

" nisikilize nikwambie mwanangu" anaongea na kufanya mapigo ya moyo ya Tulya kwenda mbio kwa woga.

" hakikisha muda utakapofika unapambanua wakati wa kutenda kwa moyo na kutenda kwa akili kwani sidhani kama nitapata nafasi nyingine ya kukwambia"

" unanitisha mama,Kuna nini Leo unaonekana hauko sawa" anamuuliza .

" kwa nini?"

" kwa sababu unaongea kwa mafumbo" anamjibu na Bibi sumbo kucheka kwa nguvu.

" twende tukale" ananyanyuka Bibi sumbo na kuelekea ndani akiendelea kucheka akimfanya Tulya asimuelewe zaidi.

Leo kukiwa kumekucha kama siku zingine lakini katika Kijiji Cha Ntungu wasiwasi umetanda wanakijiji wakijiandaa na sherehe ilihali vyakula vikiwa bado viko maili mia,imekuwa asubuhi,imekuwa mchana na Sasa jua linaelekea kuzama lakini bado mashujaa wao walioenda kuwinda hawajarudi.Mgawanyiko wa makundi ya kufikiri unatokea kwa wanakijiji wengine wakifikiri kwa Mara ya kwanza kula sikukuu zao za Mila pasipo chakula,wengine wakiwaonea huruma vijana waliotoka lindo msimu huku na kuvutwa mawindoni kwa Mara ya kwanza ilihali kukiwa hamna wanyama wakihofia uwezekano wa kuwa na Nzagamba wengi zaidi na wengine wakiweka matumaini kwa mizimu na mashujaa wao kuwa watawasili hata kama iwe ni kwa kuchelewa.

Maombi ya wenye Imani yanajibiwa kwani jua likiwa bado halijamaliza mwanga wake mbiu ya kutangaza wawindaji kurejea inasikika.Vigeregele vinasikika kijijini na wanawake wakitoka na vibuyu vya maji pamoja na vyakula na kukimbilia makusanyiko ya Kijiji kwenda kuwalaki.Wanaume waliobakia kijijini nao wakifuata njia kwenda kuwapokea.

Tulya aliyekuwa kwa mjomba wake akiongea na Bibi harusi mtarajiwa ni miongoni mwa watu waliosikia mbiu hiyo anajikuta akitoka mbio Sinde anayemwita nyuma yake asimsikie hata kidogo.

Njiani anakutana na mama yake Runde anayefanikiwa kupunguza breki za miguu yake.

" utampokea mikono mitupu?" anamsikia Runde akimwambia baada ya kumpita kama hajamuona anasimama na kurudi alipo akihema,na mapigo ya moyo wake yakienda mbio kama kakimbizwa na simba.

" njoo uchukue chakula na maji uwapelekee,ukienda mikono mitupu hautaeleweka" anaongea Runde akianza kutembea kuelekea nyumba kubwa naye akimfuata miguuni akiwa mwepesi akihisi mama yake anamchelewesha.

" polepole usije ukamwaga" anamsikia mama yake akimwambia baada ya kuona mwendo anaondoka nao Tulya baada ya kuchukua kibuyu Cha maziwa.Lakini maneno yake yanaingia sikio la kulia na kupita kushoto yasiguse kabisa kwenye ubongo.

kabla hajafika mbali anakutana na wifi zake mke wa Kilinge na mke wa Zinge.

" wifi tusubiri" anaongea mke wa Kilinge.

" nyie mnatembea polepole mtanikuta" anajibu kwa sauti ya juu akiendelea kutembea huku akihakikisha kibuyu Cha maziwa kinakaa vizuri mkononi.

" anamaanisha nini? wakati tunaenda wote huko,au sisi tunaelea wapi Ntali?" anauliza mke wa Kilinge ambaye jina lake ni Malimbe akimwangalia mke mwenzake mwenye mimba ya miezi mnne.

" mtoto wako mgongoni anakuchelewesha na Mimi na tumbo langu hapa linanifanya nitembee taratibu hapo alipo anatamani angekuwa na mabawa" Ntali mke wa kizinge anamjibu na wote wanamcheka.