Chereads / penzi la bahati / Chapter 5 - chapter 4

Chapter 5 - chapter 4

Ni wiki mbili Sasa zimepita tangu tulya aachwe na mama yake katika himaya ya mpuli ,ameanza kuyazoea mazingira na kuwa mwenyeji."aje Mzee au kijana kaka naomba umwozeshe sijali awe mke wa sita au Saba mwozesheni tu" anaamka usingizini tulya akitokwa jasho,na anasikia sauti ya runde ikiwaita nje "tunakuja mama" anaitikia tulya nakuanza kumtikisa sinde aliyekuwa amelala fofofoo "Kuna nini asubuhi hii"anauliza sinde kiuvivu " amka mama anatuita" anaongea tulya akiwa tayari ameshasimama akivaa viatu vyake aina ya katambuga.

wanatoka nje na kuelekea nyumba kubwa aliko mama Yao runde huku waking'ang'ania kaniki zao kutokana na baridi ya asubuhi "Jana mmerudi saa ngapi "anauliza runde pindi tu walipofika,sinde na tulya wanatazamana "mapema tu mama"anajibu tulya, runde anawangalia kwa kuwatathmini "mmeanza kunidanganya mmeenda ngomani na kurudi usiku ukiwa umeenda mnadhani sikuwasikia" sinde na tulya wanatazamana tena wakikosa Cha kusema.

Jana walienda ngomani wakapitiwa na kuchelewa kurudi "shauri yenu wewe mwingine mchumba wa mtu lakini hujielewi fanya varangati uchumba uvunjike na wewe mwingine hata huyo mchumba hujapata bado na unahamu ya kucheza ngoma mpaka asubuhi, kwani Mimi Nina shida sina hata shida msipoolewa mtakaa hapa kwangu mfanye kazi kama punda" anaendelea kuongea runde "haya nendeni msombelee vile vyungu tulivyochoma na kuvitoa jana wateja wanaanza Kuja kuangalia Leo"

Runde ni mfinyanzi mzuri na watu wengi wanapenda vyungu vyake.sinde na tulya wanaondoka wakijivuta kwani miili Yao ilichoka kwa kucheza ngoma jana na kuchelewa kulala .

Baada ya tulya na sinde kuondoka anafika Mzee Shana anayeonekana hakulala hapa Leo "habari ya asubuhi mume wangu" runde anamsalimia akikunja mguu wa kushoto kidogo na kuinama kama ilivyo Mila na desturi kwa mwanamke kuonyesha adabu "nzuri,nimewaona sinde na tulya wanaelekea wapi asubuhi hii" anauliza Mzee Shana akitengeneza rubega ya kaniki yake vizuri,mkono wake wa kushoto ukichomoa sime yake kiononi na kumpa runde,naye anaipokea kwa adabu "nimewatuma wakasombelee vyungu wavilete nyumbani"Mzee Shana haongei kitu anaanza kuelekea ndani runde naye anamfuata nyuma anakohoa kidogo "baba kilinge"anaita runde na mumewe anageuka na kumwangalia anaendelea"vipi kuhusu posa ya tulya unashughulikia?" "ndio nalishughulikia, bado mapema sana nataka vijana wamuone hapa Kijijini kwanza nikianza kutangaza hivihivi tu wataanza kujiuliza labda binti anamatatizo hivyo sitaki kumuweka rehani,kwani Kuna tatizo" anauliza Mzee Shana akimwangalia mkewe kwa kumpima kama ana la kusema "hapana" anajibu runde akiweka sime juu ya kibao ukutani

"sitaki kuharakisha mambo tulya ni mpwa wangu na ni mrembo sana sitaki nimuwozeshe tu Ili mradi hata kama anavitimbi nataka nipate posa bora na kwa mwanaume mzuri"anamalizia Mzee Shana akiingia chumbani "naomba tu mizimu itusaidie wasije wakaleta janga lingine maana itakuwa aibu" ananong'ona runde wasiwasi wake juu ya tulya na sinde na tabia yao ya kwenda ngomani na kuchelewa kurudi wasije wakapata mimba.

waschana wengi wanaopata mimba kabla hawajaolewa hutengwa na jamii au kupewa adhabu nyingine nyingi kwa kushindwa kujiheshimu na lawama nyingi huenda kwa wazazi hasa mama kuambiwa hajamlea vizuri.

Njiani tulya na sinde wakiwa wanatembea sinde anasimama na kumwangalia tulya "kwani mama kajuaje kama sisi tulienda ngomani Jana" "Mimi ndio nilimuaga jana" anajibu tulya bila wasiwasi "ohh mizimu nisaidieni ndo maana, mwenzio huwaga siagi Sasa unaona kilichotukuta siku nyingine usiage" sinde anaongea akianza kutembea. "kwa hiyo alitusubiri" anauliza tulya "ndio maana yake ungekuwa wewe ungelala" sinde anasimama kidogo akimwangalia tulya ambaye hajamuelewa anachomaanisha "sikiliza" anamvuta tulya na kumshika bega wakiendelea kutembea "una watoto wawili wa kike wote hawajaolewa mwingine kachumbiwa na mwingine ni bibi matata hata hodi haijasikika mlangoni na wote wameenda kuzurura ngomani na wanachelewa kurudi ungelala usingizi ukaja" anamaliza sinde na kumwangalia tulya "huwezi kulala" anajibu tulya na kuendelea "lakini ndio uniite bibi matata" "ndio kumbe tukuite nani?kwa zile fujo ulizozifanya za kukataa wachumba unataka tukuiteje shangazi anahaki ya kukasirika na kusema uwozeshwe hata kwa Mzee" sinde anamtania wakiwa tayari wameshafika sehemu vilipo vyungu"usiseme kabisa hivyo maana tangu mama aongee vile nalala kwa shida Kila nikilala najiona nimeolewa na Mzee hata leo nimeota" anaongea tulya na kumfanya sinde acheke kwa nguvu "kumbe unaogopa kuolewa na Mzee" sinde anaendelea kucheka akimwangalia tulya aliyekosa furaha.

Tulya anainama na kubeba chungu na kujitwisha kichwani sinde nae anafanya hivyohivyo "ungekuwa wewe ungeweza kuolewa na Mzee"wanaanza kutembea kuelekea nyumbani "lakini niambie ukweli kwa nini hutaki kuolewa"sinde anamuuliza tulya huku akiendelea kutembea"sio kama sitaki kuolewa,sitaki kuolewa mitala"

Sinde anasimama akimshangaa tulya kwa sababu kitu alichokuwa anakitaka ni sawa na kutaka jua lichomozee magharibi,kwani wanaume wengi wanataka kuwa na mke zaidi ya Mmoja kwa ajili ya kujiburudisha wao na wengine wakichukulia kama ufahari,sio kama haijawahi kutokea mwanaume kuwa na mke Mmoja inakuwepo ila inakuwa ni kwa nadra sana,sinde anamshangaa tulya kwa wazo alilokuwa nalo ambalo wanawake wengi huwa hawana kichwani kabisa na hata kama mwanaume anaahidi kuwa atakuwa na mwanamke mmoja tu anaoa mke wa kwanza ikifika Mbele ya safari anabadili mawazo anaoa mke mwingine tena yule wa kwanza anakuwa Hana namna nyingine kwani kuondoka hawezi hivo humbidi kuvumilia na kukubaliana na hali halisi.

"utampata wapi huyo mwanaume wako mwenyewe" wanaendelea na safari wakitembea kwa makini wasíje wakaangusha vyungu "sijui ila Nina matumaini kuwa nikitafuta sana nitampata Yuko mahali" anaongea tulya macho yake yakiwa yamejaa ujasiri na matumaini "vipi usipompata utafanyeje umri wako utakuwa umeshaenda nani atakuoa kama sio Mzee" sinde anamuuliza akitengeneza chungu chake vizuri kichwani.

Tulya ananyamaza kwa mda akifikiria atafanyaje endapo akifikia huko "nikifika huko nitakubaliana na hali halisi ila sitaki kwenda haraka nataka nijaribu kwanza" anaongea tulya akili yake ikiwa katika mgogoro wa nini kitampata huko mbeleni.

Sinde anamwangalia kwa masikitiko akijua mwenzake anaota ndoto ya mchana akiamka atakutana na giza nene asijue aende wapi lakini anaamua kutomuingilia kwani anajua tulya ni mbishi kama alifanya vimbwanga vyote vile anajua hawezi kukata tamaa kirahisi alikofika ni mbali

" unajua sisi hatuna maamuzi juu ya hilo utakapofikia ukingo usije ukajilaumu,wanawake wengi tumekuwa hatujali kuhusu kuolewa mitala ila tunachokipa kipaumbele ni kuolewa wakwanza hata mume akioa mke mwingine wewe unakuwa na madaraka mkononi ya kuwaongoza wengine na baada ya hapo mashindano na majigambo ya nani apendwe zaidi yanaingia,hongera kwa kuwaza wewe kama wewe tulya" tulya anatabasamu kwa maneno ya sinde "itakuwaje mjomba akiniletea Mzee kama mama alivyosema" anauliza tulya akimwangalia sinde.

Sinde Anacheka kidogo "utakubali, Nina uhakika utaamsha kimbunga hicho haijawahi kutokea" wote wanacheka "haya yote makosa ya yule mchumbaako nani vile" anaongea sinde uso ukijaa kukereka huku akijaribu kulikumbuka jina la mchumba wa zamani wa tulya,"luila" anamaliza tulya "eee luila asingekuacha haya yote yasingekukuta mwanaume gani Hana uvumilivu hata nusu" tulya anaguna tu mara nyingi hapendi kukumbushwa habari za luila baada ya kimya kifupi anaongea "hapo mwanzo nilikuwa namlaumu sana lakini Sasa imeshapita kwani hata yeye hakujua kuwa alianguka kwenye mtego"

Luila aliyekuwa kijana maarufu sana na hodari katika jamii ya wafugaji mabinti wengi sana walitaka kuolewa nae na wazazi wengi walimpenda na kupeleka posa kwao lakini luila alizikataa zote kwani tayari alikuwa na mtu aliyempenda ambaye alikuwa ni tulya.Baada ya baba yake tulya kupeleka posa kwao alikubali na kumchumbia tulya lakini Kuna watu ambao hawakuridhika wakitaka watoto wao lazima waolewe na luila kwani hakuwa mtanashati tu kwao walikuwa ni matajiri wa mifugo, wengi wakijua mahari ingewatajirisha.

Mzee nkia aliyekuwa na binti yake aliyempenda sana luila na yeye mwenyewe mpenda mali walifanya figisu wakamhonga somo mbuzi wawili kumfanya amcheleweshe tulya kutoka mafunzo ya mwali na mpango wao ulifanikiwa tulya alisota ndani mwaka mzima baada ya somo wake kusema hajaguzu mafunzo hii ilimshtua tulya na wazazi wake kwani somo huyo mwanzo alikuwa akimsifia tulya kuwa anafanya vizuri lakini alibadilka ghafla lakini walikuwa hawana jinsi ila kukubaliana na Hali ilivyokuwa kwani kimila Binti ni lazima amalize mafunzo hayo kwa kufuzu ndo atafaa kuolewa, huku luila akashawishika na kumuoa mbula Binti wa Mzee nkia.

Tulya alipotoka alikuta mbula tayari akiwa na mimba ya luila.pengine luila angekuwa ameoa mwanamke mwingine ambaye hakuwa mbula tulya angekubali kuolewa mke wa pili lakini tulya na mbula walikuwa ni kama maji na moto hivo hakutaka kuwa katika vita mpaka anaingia kaburini kwani alijua yeye na mbula hawawezi kupatana hasirani,licha ya luila kuujua ukweli hakukubadili kitu kwani mbula tayari alikuwa mke wake na yeye ndo aliyeanguka kwenye mtego wa mbula na baba yake hakuwa na wakumlaumu hivyo alimpoteza tulya. "ndio maana na jina lake baya" tulya anaondokewa kwenye mawazo na sauti ya sinde iliyokuwa bado inamtukana luila anaanza kucheka "unaniambiaga Mimi sijui kuziba mdomo na wewe je imekuwaje Leo" sinde ambaye sio mwongeaje sana leo alikuwa anatukana ikamfanya tulya acheke "lakini ni hasara yake kakosa mwanamke mrembo kama wewe" anaongezea sinde na kuendelea

"hembu nambie shangazi alisema ni mzuri sana ni kweli" anauliza sinde akigeuka kumwangalia tulya macho yake yakiwa yamejaa shauku ya kujua "ndio,alikuwa moto wa kiangazi wa kuwasha Kijiji kizima lakini mbula ndio mshindi" anajibu tulya sauti yake ikikwaruza kidogo na anakohoa kusafisha koo

sinde anakuja sura kusikia tulya akisema mbula ndo mshindi"mshindi wapi?Nina uhakika atakuwa anaishi maisha ya taabu mpaka haamini kuishi na mwanaume asiekupenda ni sawa na kukalia Kaa la moto ni mbaya zaidi kwake uongo wake umegundulika najua luila atakuwa anamuona kama mzoga Sasa hivi" "watajuana wenyewe Mimi hayanihusu tena na nipo ulimwengu mwingine kabisa" anajibu tulya akitaka kuiacha maada hiyo "kwa nini wanaume wengi wazuri wanaishia vibaya hivo"

anaongea sinde wakiwa wamefika nyumbani wakitua vyungu vyao chini "wengi mwingine nani aliyetapeliwa" anauliza tulya akisimama "yeye hakutapeliwa yeye alinyang'anywa mchumba" "na nani? alikuwa haoni au?" anauliza tulya na kabla sinde hajajibu wanakatishwa na sauti ya runde akija "naona nikiwaacha mtamaliza kesho haya twendeni huko mwisho wateja waje wakute kweupe hapa" anaongea runde akiwapita na wao wakimfuata nyuma kwa mwendo wa haraka.

mwezi umeisha Sasa tangu tulya aje katika himaya ya mpuli hamna mchumba yeyote aliyeleta posa wala mjomba ake hajalizungumzia suala la posa na anashukuru kwa hilo maana yeye mwenyewe hayuko tayari kabisa kuanzisha varangati ugenini.

Inilikuwa ni mchana wa jua la utosini tulya na mama yake runde kama alivyopenda kumuita mke wa mjombaake walikuwa mtoni wakichota maji. tulya akiwa ameinama akijaza kibuyu chake maji anasikia sauti ya mziki mzuri sana,sauti ambayo ilikuwa ikisikaka vizuri kabisa kutokana na upepo tulivu wa mchana.

Sauti ilipenya masikioni kwake ikagusa mpaka moyo wake mapigo yakimwenda upesi,anajaribu kutega sikio lake vizuri ajue inatokea wapi pasipo mafanikio kwani sauti ilikuwa imesambaa eneo lote la mto."kalimba hiyo" anashtushwa na sauti ya mama yake runde aliyemuona ameduwaa akiisikiliza mziki "eeh! najua kama ni kalimba nani anapiga hiyo anapiga vizuri kweli" anauliza tulya akisogeza kibuyu chake pembeni huku masikio yake yakiendelea kusikiliza mziki "nzagamba" anajibu runde.