Chereads / penzi la bahati / Chapter 10 - chapter 9

Chapter 10 - chapter 9

"Umepatwa na nini tulya" anajiuliza mwenyewe akiweka mkono wake kifuani kufuatilia mapigo ya moyo wake."simuachi mjinga huyu"kilinge anataka kuamka kwenda kugombana na manumbu kwa kutaka kumdhalilisha nzagamba,lakini nzagamba anamzuia "achana nae unataka uanzishe fujo" nzagamba anamkemea kilinge huku amemshika mkono asinyanyuke alipokuwa amekaa.

"kwa nini tusiwapatie wakati wameitaka wenyewe" mkita ananyanyuka pamoja na ntula "ndio,huwa tunanyamza sana ndio maana hutafuta sababu ya kutuchokoza Kila wakipata nafasi" ntula anaongezea akijiandaa kupigana "nimewambia mkae mtulie"nzagamba anaongea kwa sauti ya ukali lakini ya chini watu wengine wasisikie "mnataka muanzishe fujo hapa habari zikiwafikia wazee na mtemi mtaonekana hamna adabu mmdharau sherehe,sitaki muadhibiwe kwa ajili yangu" anasisitiza nzagamba akiwaangalia marafiki zake,hakuwa nao kundi Moja tena lakini alishukuru kwa mara Moja Moja walipokutana hawakumfanya awe mpweke licha ya matatizo yake "tuko radhi kwa hilo,wanazoea sana wewe ni rafiki yetu hata iweje" anasisitiza mkita akionekana kutokukubaliana na nzagamba hata kidogo.

"Mimi siko sawa mkita,nashukuru kwa kuwa na Mimi, lakini sitaki muharibikiwe kwa ajili yangu,kama kweli unataka kumshikisha adabu kwa nini usimpige mshale wa kalio ukiwa porini" anatania nzagamba akinyanyuka na kumshika bega mkita "usijali,sio mbaya sana tofauti na angeniambia niende porini kuwinda,kwanza nimekumbuka sana kupiga mziki ngoja nikatoe jashi kidogo" nzagamba anawaacha marafiki zake akiwapatia tabasamu la kuwahakikishia kuwa Yuko sawa na kuelekea sehemu zilipokuwa ngoma huku minong'ono ya watu ikiendelea.

"siku Moja nitampiga mshale wa kalio kweli" mkita anaongea akikunja ngumi yake kwa hasira "subiri mpaka mawindo yaje tutapanga mashambulizi,kwa Sasa tulieni hamjamsikia nzagamba alivyosema" kilinge anawapoza wenzake na wote wanasimama na macho yao kuelekeza anakoelekea nzagamba"ndio,tumwache nzagamba alishughulikie hili,wote tunamjua nzagamba sio mtu wa kukata tamaa kirahisi wala mtu wa kuangushwa na kisiki Cha mti,huyo tumsubirie porini" lingo anaongea huku akitoa tabasamu la kisasi usoni kwake na wote wanaitikia kukubaliana kwa "mmh".Licha ya nzagamba kutokuwa katika kundi la kuwinda Hawa wa nne bado walikuwa wanamheshimu na kumchukulia kama kiongozi wao kabla ya rafiki hivyo ilikuwa ni rahisi kumsikiliza kwani muda wote walikuwa upande wake na walielewa maumivu aliyokuwa anayapitia.

Tulya anajikaza na kugeuza shingo pale alipokuwa amesimama nakuelekeza macho yake kule watu wanaokoangalia,mapigo ya moyo wake yanaongezeka zaidi pale anapomuona nzagamba akipita katikati ya watu waliokuwa wakimwachia njia Ili apite macho yake yanatua kwenye uso wake na kuona ni kijana Mmoja mzuri,aliyetoboa masikio yake nakuacha shimo kubwa katikati na kufanya yaning'inie kidogo na kumkaa vizuri, nywele zake ndefu zilizojisokota,usoni kwake jicho lake la kushoto likiwa limechanjwa mstari Mmoja wa duara kuzunguka jicho lake na kuwekwa vidoti vidogo vidogo juu yake, na shingoni akiwa amevaa kidani kifupi kilichokaribia kumkaba shingo yake,kifua chake kilichojazia misuli kikiwa na bombe mbalimbali na kumfanya tulya ajue Kila mchoro ulikuwa na maana yake anaangalia vizuri na kuona vidani viwili vilivyokaba misuli ya mikono yake na kumpendeza kama alimwona manumbu kapendeza basi alikosea nzagamba ndiye aliyependeza kuvaa vidani na michoro mbalimbali mwilini kwake kuliko vijana wote aliowaona hapa Kijijini hapana sio Kijijini hapa tu aliowahi kuwaona tangu azaliwe.

Nzagamba anafika sehemu ya wapiga mziki anaenda na kumfuata Mmoja wa wapigaji anaongea nae maneno ambayo tulya hakuyasikia kwani alikuwa Yuko mbali na makini kumkagua na kumuona akitabasamu kitendo kilichofanya mapigo ya moyo wake kuzima kwa sekunde chache mpaka kurudi,meno yake makubwa yaliyopangana vizuri yalipendezesha tabasamu lake.

Nzagamba anashika vijiti viwili mikononi mwake na Moja kwa Moja tulya akajua anaenda kupiga ngoma au malimba anatembea Mbele kidogo na kwenda kusimama sehemu ya malimba anapiga kidogo kama anajaribu au kuwapa ishara wenzake kuwa watapiga mlio huu ananyanyua mkono wake juu na kupiga kwa nguvu zaidi ile malimba kufanya mziki wa malimba kusikia vizuri kuliko mwanzo,tulya anaangalia mkono wake wa kushoto na kuona ulikuwa na mchoro mzuri wa mshale.

nzangamba anaanza kupiga malimba peke yake kwa muda wa dakika kama Moja na baada ya hapo mtu wa ngoma nae anaanza kupiga na wengine wote wanaanza kumfuata kitendo kilichofanya mziki uwe mzuri na watu wote kuanza kucheza isipokuwa tulya.

Sinde anaiona hali ya tulya na kumfuata alipo "uko sawa" anamuuliza akimshika tulya "nasikia kifua kinabana nashindwa kupumua" anaeleza tulya akijishika kifuani "eeeh! basi twende huku tukatafute maji na sehemu yenye upepo"

Sinde anamtoa tulya sehemu ya kucheza na kumpeleka pembeni kidogo mbali na walipo watu anamsaidia kukaa chini ya gogo "subiri nikuletee maji" sinde anaondoka na baada ya mda anarudi akiwa na kipeo Cha maji anampa tulya anakunywa "unajisikiaje"anauliza uso ukimjaa wasiwasi."Niko vizuri wewe nenda kacheze Mimi nitakuwa sawa" anaongea tulya akiegemea ukuta na kufumba macho yake " una hakika" tulya anaitikia kwa kichwa "sawa ukijisikia vibaya zaidi uniite tuondoke" tulya hamjibu anamtupia mkono kumwashiria aondoke na sinde anaondoka.Tulya anaendelea kukaa pale huku akiwa bado amefumba macho na masikio yake yakisikiliza mziki.

Kwenye ukumbi wa kucheza watu wote wakiwa wanatimua vumbi wakisahau lengo la mziki huo,manumbu akiwa pembeni na marafiki zake wakiangalia watu wakicheza na nzagamba akiwa na uso wa furaha na kumfanya manumbu akunje ngumi kwa hasira zinge aliyekuwa ameegemea mti na mikono yake ikiwa imepishanishwa kifuni kwake anaiona vizuri Hali ya manumbu na kutabasamu "hongera kwa kuwa kumbusha watu kuwa Kuna mziki mzuri,umefanya sherehe ifane" manumbu anamwangalia kwa hasira lakini zinge hakujali "unaongeza Kuni kwenye moto unaowaka unajua hilo" nsio anamjibu zinge,zinge anamwangalia na kuangalia wanakocheza watu anakunjua mikono yake na kuanza kuondoka "unaenda wapi?" anauliza nsio "nyumbani,hapapendezi tena hapa" anajibu zinge akiondoka "usijali sana unajua huyo Kila akiongea huwa ni kukera watu tu tumeshamzoea" nsio anamfariji manumbu aliyekuwa amekerwa na tabia ya zinge kutokuwa upande wake.

zinge ambaye siku zote huwa hapendezwi na tabia ya marafiki zake anaamua kuondoka eneo hilo kwani alikuwa hana la kufanya na vilevile huwa sio mtu wa makelele hivyo alipata nafasi nzuri ya kuondoka.

manumbu anaangalia na kuona mke wake lindiwe akiwa katikati ya watu akicheza anakunja sura na kutaka kuingia kwenda kumvuta lakini nsio anamkataza "acha unataka kufanya fujo Mbele za watu Hawa wote utamshughulikia ukifika nyumbani,na umesahau kuwa wewe ndio uliyemkaribisha nzagamba Ili umdhihaki watu watakuelewaje ukilianzisha Sasa hivi"

manumbu anaamua kusikiliza ushauri wa rafiki yake na kutulia pembeni huku pipa la hasira likiendelea kuchemka,tulya aliyekuwa anarudi anasikia mazungumzo ya nsio na manumbu "ni mtu gani huyu anayefurahia mateso ya wenzake na kuyafanyia mzaha" anajisemea tulya akirudi kule alikotoka asije manumbu akamuona na kumkasirikia kwa kusikiliza mazungumzo Yao moyoni akizidi kumchukia manumbu.

Baada ya muda mziki aliokuwa anapiga nzagamba unaisha na kuanza kupigwa mwingine tulya anaamka na kusimama alipokuwa amekaa na kushika kifua chake "Niko sawa Sasa"anajisemea nakuanza kutembea kurudi ukumbini njiani anamuona nzagamba akiwa anaondoka sababu Giza tayari lilianza kuingia mapigo ya moyo yanaanza kumwenda mbiao tena anapomwangalia nzagamba akiondoka bila kumuona yeye aliyekuwa akimwangalia " kama unataka kulala njaa nenda huko" anasikia sauti ya mtu nyuma yake.

Anashtuka na kugeuka anamuona manumbu akimfuata pale alipo,tulya hakutaka kuongeza chumvi kwenye kidonda tayari alishajua kuwa manumbu alifanya makusudi kumwambia nzagamba apige malimba Ili amwaibishe na mpango wake kuangukia pua anajua fika kuwa manumbu atakuwa anahasira na hakutaka kuwa kiroba Cha mchanga Cha kumalizia hasira hivyo anaamua kutulia na kutokusema kitu hata kama mdomo Wake ulikuwa unawasha kumlipukia manumbu na kumpa ya moyoni mwake "habari yako kiongozi"anasalimia tulya kwa heshima lakini manumbu hajaitikia na kubaki akimwangalia tulya kwa kumtathimini kuanzia kichwani mpaka miguuni kitendo kinachomfanya tulya apate msisimko wa woga Kila siku akimwangalia hivyo kitendo alichokuwa hakipendi kabisa.

kwa manumbu Leo hii alikuwa anamuona tulya ni mrembo sana tangu mchana alipokuwa anacheza na Sasa kutokana na mwanga hafifu wa mwezi anaonekana mrembo zaidi anamkagua kuanzia usoni anakuja kifuani anamwangalia saa sita zake mbili zilizofungwa vizuri na kuona kitambaa chake Cha kifuani hakiyatendei haki kwani kinayakaba na kupoteza mvuto wake anamwangalia tumbo lake dogo lililokuwa wazi linalofanya mpaka kiuno kiwe kidogo akija umbo la hipsi zake zinazofanya kiuno kiseme kinaonewa kuzibeba na mguu wake mnene uliopendeza kwenye kiatu Cha kuzungusha kamba iliyokuwa na njuga hakuwa mnene wala mwembamba, anamfanya ashindwe kujizuia kama mwanaume rijali.

Tulya anaamua kuongea Ili kumfanya manumbu aache kumwangalia "unamaanisha nini nitalala njaa" manumbu anashtuliwa na sauti ya tulya ambayo nayo aliisikia ikipenya masikioni kwake kama sauti ya ndege mzuri wa asubuhi.Anayapotezea mbali mawazo hayo nakurudi duniani "nimekuona unavyomwangalia nzagamba kwa sababu wewe ni mgeni hapa Kijijini utakuwa hujasikia habari zake" anaeleza manumbu "nimeshasikia habari zake" tulya anajibu akijitahidi kutokujibu kwa nyodo na kumuudhi manumbu habari zake tayari alikuwa Nazo "kweli lazima usikie kwani hata mpita njia tu huwa lazima asikie akipita,na Mimi je?" anamalizia kwa kumtupia swali,tulya anamwangalia kwa uso wa kutokuamini rohoni akiwaza 'huyu anataka nini?' lakini hakutaka kumuuliza kwa sauti "zako pia nimezisikia" anajibu na kumfanya manumbu asimame kibabe "kama hauna kingine Cha kuongea Mimi naondoka" tulya anaanza kuondoka lakini manumbu anamshika mkono na kumfanya tulya atake kumrukia kwa jazba iliyomjaa anapeleka macho yake Mahali alipomshika manumbu na kabla hajamwachia wanashtuliwa na hatua za mtu akija "nilikuwa nakutafuta kumbe upo huku"