Chereads / HUESOS / Chapter 1 - 1.KANIACHA

HUESOS

🇹🇿Mtuwa_Peter
  • --
    chs / week
  • --
    NOT RATINGS
  • 6.5k
    Views
Synopsis

Chapter 1 - 1.KANIACHA

"Waiter,hebu niongezee bia mbili." Ilikuwa ni sauti ya kijana Benson akimuagiza mhudumu wa baa.Benson alikuwa katika kipindi kigumu sana maishani mwake.Hii ilitokana na kuachwa na mpenzi wake,Ana.

Kuachwa kwake na Ana kulimpelekea awe mlevi wa kupindukia na hata kuchelewa kufika kazini na hilo lilipelekea Benson kufutwa kazi.Ana alikuwa ni mpenzi wa muda mrefu wa Benson lakini ghafla tu akaamua kuachana na Benson bila sababu maalum.

"Eey,eey amka saa hivi ni saa kumi na moja alfajiri" Sauti nyororo ya mhudumu ilisikika.Benson akajikongoja kunyanyuka huku bado akiyumbayumba, akaingia kwenye gari ili kuelekea nyumbani kwa wazazi wake.Alipofika nyumbani hapo alisita kidogo kugonga hodi lakini kabla ya kuanza kugonga hodi mara mlango ukafunguliwa.Alikuwa ni mama yake Benson.Alikuwa ni mnene kiasi,mrefu kwa kiasi chake na rangi yake ilikuwa ni maji ya kunde.

"Mwanangu, toka jana asubuhi ndo unarudi sasa hivi,usiniambie bado unakunywa pombe.Si nimekuzuia mie.Wasichana si wapo wengi tu kwani lazima Ana",mama Benson alilalama kwa hasira huku akitetemeka."Mama,habari za Ana tuachane nazo, mimi sasa hivi naangalia maisha yangu wala siangalii mtubaki",Benson alijibu."Sasa mbona bado unalewa?",mama huyo alihoji.

Benson hakujibu bali aliingia sebuleni moja kwa moja.Mara pap....Baba Benson huyo.Hakusita hata kujongea na kilichofuata ni kumpayukia Benson.Benson hakuwa na budi zaidi ya kumsikiliza baba yake na baada ya hapo alielekea chumbani kwake.

Benson hakuwa ni mtu aliyependa kuishi chini ya mwamvuli wa wazazi wake pindi atapokuwa katika ujana wake lakini hali iliyomtokea hivi karibuni hasa baada ya kufutwa kazi, hakuweza kulipia tena kodi ya ile nyumba aliyokuwa amepanga.Hivyo basi hakuwa na budi zaidi ya kurudi kuishi tena nyumbani kwa wazazi wake." Kaka utamwaza hadi lini Ana,achana naye we fanya maisha yako."Huyu alikuwa ni mdogo wake Benson aitwaye Boniface." Dogo ukikuwa utaelewa.", Hilo lilikuwa ni jibu la Benson kwa mdogowe.Benson akaingia chumbani kwake kwenda kupumzika.

**************************

"Hivi Ana, sababu ya kumuacha hasa Benson ni nini yaani? Anateseka sana mtoto wa watu.Nimekutana nae hapo juzi kati hapo amelewa chakari.We unaenjoy tu unakula raha.Utamtesa hadi lini?", ilikuwa ni sauti ya Rose moja ya marafiki zake Ana."Jamani,kila muda Bensoni Benson mara kafanya hili mara kafanya lile.Nimemuacha kwa maamuzi yangu lakini sio kwa kulazimishwa na mtu na kingine mkome kumuongelea huyo Benson kama vipi kaolewe naye wewe.",Povu lilimtoka Ana.

Ana ni mtoto ambaye alizaliwa katika mazingira ya kitajiri sana na hakuwahi kujua shida na umaskini ni kitu gani.Ukiachana na hilo Ana pia alikuwa ni mwenye akili darasani.Alikuwa amefanikiwa karibu kila kitu lakini hakufanikiwa jambo moja tu.Hakuwa maarufu.Ni kitu alichokiwaza sana na ndio maana alipopokea DM kutoka kwa moja ya wasanii maarufu nchini,Rico Brizzo kuwa anamkubali na kumpenda hakuweza kumkatalia. Hiyo ndio ilikuwa fursa yake,Ana ya kuwa maarufu.Hii ndio sababu hasa ya Ana kuachana na Benson.