Health and wellness
MADHARA YA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO
Vidonge vya Uzazi wa Mpango, ni moja ya njia inayopendekezwa na Wataalamu wa Mpango wa Uzazi katika kuzuia mimba. Hata hivyo, vidonge hivyo Vinaweza kutimiza malengo hayo ya mpango huo ikiwa tu vitatumiwa vizuri na kwa usahihi, kwa sababu tafiti zilizopo, zinaonyesha kwamba asilimia nane (8%) ya wanawake hupata mimba zisitarajiwa kila mwaka, huku wakiwa katika mpango huo kutokana na baadhi yao kujisahau kumeza vidonge hivyo.
Kwa mujibu wa tafiti hizo ambazo FikraPevu inazo, vidonge hivyo vya mpango wa uzazi vikitumiwa vizuri, kwa kuhakikisha muda wa matumizi yake unakuwa ule ule, ni mwanamke mmoja pekee kati ya 100 anayeweza kupata mimba isiyotarajiwa ndani ya mwaka wa kwanza wa matumizi ya dawa hizo.
Hadi sasa kuna aina kuu mbili tu za vidonge vya uzazi vinavyotumiwa na wanawake katika wa mpango huo, ingawa aina zote hizo zina vichocheo (hormons). Aina hizo kitaalamu zinaitwa Estrogen na Progesteron. Estrogen ni aina ya kichocheo kinachotengenezwa na uterasi/
kizazi, kinachosaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi, kwa kuongoza ukuaji wa kuta za uterasi kwenye sehemu ya kwanza ya mzunguko wa hedhi.
Kwa upande wake, Progesterone, hiki ni kichocheo cha kopasi luteamu ya ovari, kinachosaidia kuanzisha mabadiliko katika endometriumu baada ya ovulesheni.
Ingawa katika aina hiyo mbili ya vidonge, kuna vingine vina kichocheo cha aina moja tu, kwa maana ya ama Estrogen au Progesterone, huku vingine vikiwa na vichocheo vyote viwili hivyo, lakini vidonge vyote hivyo ni salama, na vinafanya kazi kwa kufanya ute mzito kwenye shingo ya mji wa mimba na kuzuia kupevuka kwa yai, hivyo kuzuia mimba kwa kiwango cha asilimia 99.
Vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza pia kutumika kama tiba ya kuweka sawa mzunguko wa hedhi, kuzuia maumivu makali wakati wa hedhi, kutibu chunusi pamoja na kupunguzamaambukizi ya magonjwa ya zinaa.