Download Chereads APP
Chereads App StoreGoogle Play
Chereads

Hatai

Health and wellness

MADHARA YA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO Vidonge vya Uzazi wa Mpango, ni moja ya njia inayopendekezwa na Wataalamu wa Mpango wa Uzazi katika kuzuia mimba. Hata hivyo, vidonge hivyo Vinaweza kutimiza malengo hayo ya mpango huo ikiwa tu vitatumiwa vizuri na kwa usahihi, kwa sababu tafiti zilizopo, zinaonyesha kwamba asilimia nane (8%) ya wanawake hupata mimba zisitarajiwa kila mwaka, huku wakiwa katika mpango huo kutokana na baadhi yao kujisahau kumeza vidonge hivyo. Kwa mujibu wa tafiti hizo ambazo FikraPevu inazo, vidonge hivyo vya mpango wa uzazi vikitumiwa vizuri, kwa kuhakikisha muda wa matumizi yake unakuwa ule ule, ni mwanamke mmoja pekee kati ya 100 anayeweza kupata mimba isiyotarajiwa ndani ya mwaka wa kwanza wa matumizi ya dawa hizo. Hadi sasa kuna aina kuu mbili tu za vidonge vya uzazi vinavyotumiwa na wanawake katika wa mpango huo, ingawa aina zote hizo zina vichocheo (hormons). Aina hizo kitaalamu zinaitwa Estrogen na Progesteron. Estrogen ni aina ya kichocheo kinachotengenezwa na uterasi/ kizazi, kinachosaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi, kwa kuongoza ukuaji wa kuta za uterasi kwenye sehemu ya kwanza ya mzunguko wa hedhi. Kwa upande wake, Progesterone, hiki ni kichocheo cha kopasi luteamu ya ovari, kinachosaidia kuanzisha mabadiliko katika endometriumu baada ya ovulesheni. Ingawa katika aina hiyo mbili ya vidonge, kuna vingine vina kichocheo cha aina moja tu, kwa maana ya ama Estrogen au Progesterone, huku vingine vikiwa na vichocheo vyote viwili hivyo, lakini vidonge vyote hivyo ni salama, na vinafanya kazi kwa kufanya ute mzito kwenye shingo ya mji wa mimba na kuzuia kupevuka kwa yai, hivyo kuzuia mimba kwa kiwango cha asilimia 99. Vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza pia kutumika kama tiba ya kuweka sawa mzunguko wa hedhi, kuzuia maumivu makali wakati wa hedhi, kutibu chunusi pamoja na kupunguzamaambukizi ya magonjwa ya zinaa.
DaoistKHDcJO · 4.5K Views

Melody of Time: Epic ya Kim Dan

Muhtasari: Melodi ya Wakati: Hadithi ya Epic ya Kim Dan Utangulizi Mwaka 2024, Kim Dan, msanii wa K-pop na mtunzi wa miaka 21, anajitengenezea njia yake mwenyewe ya muziki. Usiku mmoja, wakati akicheza piano aliyoachiwa na babu yake, alilala na akaota juu ya tai mkubwa. Tai huyo anamfunulia melodi ya kale inayojulikana kama "Sauti ya Mbingu," na Kim Dan anatambua kwamba melodi hii imeunganishwa kwa undani na hatima yake. Sehemu ya 1: Kim Dan wa Zamani Maelfu ya miaka iliyopita, katika jamii inayoshi kwa ushirikiano na asili, Kim Dan wa Zamani alizaliwa. Anakua na uhusiano wa kina na tai na anajitahidi kukamilisha "Sauti ya Mbingu" ili kulinda kabila lake. Hata hivyo, lazima akabiliane na vitisho vya nje na akubali hatima yake ya kupigania maisha ya watu wake. Sehemu ya 2: Kim Dan wa Zama za Kati Wakati wa kipindi cha falme tatu, Kim Dan wa Zama za Kati anaibuka kama shujaa wa hadithi ambaye ana uwezo wa ajabu wa kudhibiti dhahabu. Anatumia nguvu hii kupigana na maadui zake na anaanza safari ya kugundua uhusiano wa siri kati ya "Sauti ya Mbingu" na nguvu ya dhahabu. Sehemu ya 3: Kim Dan wa Kisasa Katika Korea Kusini ya kisasa, Kim Dan wa Kisasa ni msanii wa K-pop ambaye anatafuta kutafsiri upya "Sauti ya Mbingu" kupitia sanaa ya kisasa. Anajitahidi kutatua migogoro yake ya kisanii kwa kuunganisha zamani na sasa kupitia nguvu ya melodi hiyo. Sehemu ya 4: Kim Dan wa Baadaye Katika jamii ya baadaye yenye dystopia, Kim Dan wa Baadaye anakuwa mpainia wa muziki wa mtandaoni na sanaa ya kijeshi ya hologramu. Anajitahidi kurejesha ubinadamu uliopotea kupitia "Sauti ya Mbingu," lakini melodi hii ina nguvu hatari inayoweza kubadilisha jamii, na kumwongoza kwenye vita vya mwisho. Hitimisho Kila Kim Dan katika vipindi tofauti anatimiza misheni yake, na "Sauti ya Mbingu" inafanya kazi kama ufunguo unaopita muda na kuamua hatima ya wanadamu.
Daniemuta · 663 Views