Download Chereads APP
Chereads App StoreGoogle Play
Chereads

Malaika Battletech

MALAIKA WA UPENDO

Hapo mwanzo Mungu aliumba ulimwengu, akaumba mimea, wanyama, mito, mabonde akavibariki. Akamuumba mwanadamu kwa mfano na sura yake, aliwaumba mwanamke na mwanaume. Mungu akawabariki na kuwaambia "Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki" Mwanzo 1: 1 - 28. Katika amri ya kuujaza ulimwengu, Akamuumba malaika, Malaika wa Upendo. Yeye akaweka hisia ndani ya wanadamu, jukumu amepewa na mwenyezi Mungu. Malaika wa Upendo akawa ndiye kiongozi na msimamizi mkuu aliyepewa jukumu la kuhakikisha kila mmoja anampata amsitahilie, ili kulitimiza agizo la mwenyezi Mungu, "Zaeni muongezeke mkaijaze nchi na kuimiliki," Mwanzo 1: 1- 28. Hii Ni wazi kwamba, awali kabla hujampata akustahilie, utapitia misuko suko na changamoto nyingi za ujana, hasa pindi upambanapo kumupata akupendaye / umupendaye. Hivyo usipokuwa makini, utajikuta ukiingia kwenye mahusiano na mtu asiye wako. Na hapo utalipata jibu Ni kwanini..? Robo tatu ya wasanii wanaimba mapenzi. Hivyo Kama kijana, kwa Imani yako, fanya Dua na Sala ili Malaika huyu wa Upendo, aweze kukuongoza na kukuonyesha, Alie chaguo lako sahihi maana ndiye aliyepewa jukumu hilo na Muumba wetu. La hasha.!, Usipoweza kuwa mvumilivu na kuzishinda tamaa, ukaamua kufanya maamuzi yako binafsi, pasipo kumshirikisha Malaika huyu wa upendo, utajikuta ukiingia kwenye mahusiano na mtu asiye sahihi Yani asiye chaguo lako. Hapo tarajia dhambi ya uzinzi, kutendwa, Na maumivu makali moyoni mwako, havita hepa, maisha yako yote, maana umejitwika gunia la misuri, ungali umenyoa kipara. Fatilia kisa hiki Cha MALAIKA WA UPENDO upate kujifunza, chaguo sahihi pasipo Makosa.....
Salvatory · 24.5K Views
Related Topics
More