Download Chereads APP
Chereads App StoreGoogle Play
Chereads

THE MONSTER INSIDE OF ME

🇹🇿Laivilani_tz
--
chs / week
--
NOT RATINGS
2.3k
Views
Synopsis
Amanda anajikuta akiingia kwenye mikono ya shetani aliemtengenezawenyewe na kuuonja moto wa kuzimu yake je atafanya nini?
VIEW MORE

Chapter 1 - shetani

"Amanda,mara ngapi unataka nikuambie namna navyojisikia juu yako..unapenda namna navyolia Lia juu yako?" Mike mkaka mtanashati na mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya kulevya alilalamika mbele ya mdada Amanda Clayson ambaye anashikilia rekodi ya kushinda taji la miss Tanzania na miss world mfululizo.Ni zaidi ya mwaka mmoja Sasa Mike anamfatilia Amanda akionesha nia ya dhati kabisa kutoka moyoni kwake.Licha ya juhudi zote Amanda alitoka na mwanaume tofauti na Mike na sasa walikuwa wanaenda kufunga ndoa siku ya kesho yake jambo ambalo lilimuumiza mno Mike.Kwanini asiwe yeye?Anakasoro gani.

"Sio moyoni tu bali hata machoni pangu hunivutii..Sikupendi na sitokupenda.Hufai hata kukaa mbele yangu.Nawezaje kutoka na shetani kama wewe?Muuwaji tu." Amanda akafoka na kumtazama kwa dharau.

"Babe!"Akaitwa Amanda na hapo akaja Strphan mumewe mtalajiwa.

"Yes babe."Amanda akijibu akisogea mbali zaidi na Mike ambaye alifura kwa hasira.Kumpata Amanda iliweka vita kubwa kati yao.Sasa moto uliwaka zaidi.Stephan akamsogelea Amanda na kumbusu shavuni kwa lengo la kumuumiza Mike.

"Mambo..Ushapata mwaliko wa harusi?" Steph akauliza na kumfanya Mike azidi kuchukia.

"Sishangai hata usipokuja mara zote unaleta chuki za kijinga."

"Chunga mdomo wako.Utaumia"Mike akaonya kwa sauti ya baridi yenye maumivu makali ya kupoteza.Hili penzi lilimchanganya akili.

"Steph tuondoke..tumpishe Shetani.." Amanda akaaga na kumshika kiuno Steph kutoka eneo la parking ya magari taratibu.Mike akawatazama na kutabasamu kiroho mbaya.

"Tumegombana kwa muda mrefu lakini Mimi naonekana kushindwa,sitokubali damu lazima imwagike.Amanda wewe ni wangu lwa nguvu maana amani imeshindikana."

Mike akajisemea na kutabasamu.Kichwani alishapanga jambo lake

*Mchana wa harusi*

Amanda alikuwa na tabasamu Pana akiwa njiani kuelekea kanisani.Alijua wazi anaenda kuwa mke halali wa Stephan,mwanaume wa ndoto yake.Ataachaje kufurahia hii nafasi.Basi mwisho akawasili kanisani ambapo watu wengi walijaaa.vigere Gere vikapigwa akapokelewa na kuingia ndani kumkabili Steph ambae alisimama kwa bashasha akimtazama.Amanda akatabasamu na kumsogelea.Ilikuwa ndoa ifike mwisho pale ambapo risasi ilipenya kwenye kifua Cha Steph na kuwaacha watu mdomo wazi.

"Steph!!!!!!"Amanda akapiga kelele baada ya Steph kudondoka chini.Hajakaa sawa shetani huyu mbele yake sio mwingine Bali ni Mike.Hata nguvu ya kuongea tu alikosa.Walinzi wa Mike wakaingia wakiwa na mabunduki yao na kuwamiminia risasi wageni waalikwa wote.

"Twende hukuuu!!!"Akamvutana Amanda kwenda nae nje.

"Niachee!!"Akataka kuleta fujo akapigwa ngumi Moja akaximia pale pale.Wakawasha gari zao na kuondoka haraka sana.

"Naenda mbali na maisha haya sababu yako Amanda..najua nitatafutwa baada ya Hilo ila sijali.cha msingi wewe nimekupata."Mike akajisemea na kutabasamu.Ndugu wa Stephan ni miongoni wa viongozi kwahy alijua watamtafuta tu.

Je kweli Stephan kafa?Nini hatima ya Amanda?