Asubuhi Moja tulivu jua likiwa lishachomoza sauti ya ndege mbalimbali zikiwa zinasikika, mji ukiwa umechangamka kwa pirikapirika za hapa na pale watu wakiendelea kutafuta mkate wa siku.
Mlio wa simu unamkurupusha bibie Mayrah usingizini, kiuchovu akachukua simu na kupokea huku akiweka loud speaker "Good mooorning baby" Sauti ya mwanaume iliyochangamka ilisikika "Morning honey" Alijibu kwa kwa sauti ya uchovu "Usinambie bado umelala mpaka muda huu Mayrah" "Aah nilichelewa kulala usiku ndo maana nime-overslept, you know that I'm not this lazy mpaka nichelewe kuamka" "Mmh!! ulikuwa unafanya Nini mpaka uchelewe kulala " "Hakina umuhimu wowote ule just potezea" "Mayrah..." "Yes babe" "Hivi ni kwamba ujui kama Kila kitu kinachohusiana na wewe kina umuhimu mkubwa sana kwangu" " Aidan please over thousand pleases naomba unielewe ninavyokwambia it's not important" kulikuwa na ukimya kidogo baada ya Mayrah kuongea maneno hayo "Ooh, it's not important sio, great then have a nice day" Aidan alijibu kwa sauti iliyoonyesha amekerekwa na maneno aliyoyaongea Mayrah "Aidan naomba usini....." kabla hajamaliza kuongea simu ikakatwa "Aidan.....Aidan" Akiangalia simu machozi yakawa yanamlengalenga kudondoka muda wowote ule "Laiti ungejua ni kitu gani hicho ambacho sitaki kukuhisisha usingetaka kukifahamu" Alijisemea huku chozi likimporonyoka kwenye jicho lake la kushoto na kuangukia kwenye kioo Cha simu yake.
*********************************************
Nyumbani kwa kina Apollo, Mama yake akiwa na Mumewe chumbani wakawa wanajadili jambo "Unahisi atakubali kirahisi tu" Aliuliza mama huyo huku akijivuta kitandan ili akae vizuri "Tunajua itakuwa ni ngumu mpaka akubaliane na sisi but no matter what lazima tumfanye akubaliane na sisi ebu jaribu kufikiria faida tutakazopata kupitia hii ndoa" "Najua faida zake, ntakuwa business woman gani alaf nisijue importance zake?" "Kwa njia yoyote Ile this has to happen".
Pindi wao wakiwa wanaongea mambo Yao chumbani, mtu wanaemuongelea ndo kwanza alikuwa anamalizia kujiandaa ili atoke na Zeus (mbwa) kwaajili ya matembezi, alipomaliza akashuka zake mpaka chini ambako akamkuta mdog wake Vera akiwa nae anataka kutoka aelekee kwenye safari zake "Morning bro" alisalimia baada ya kumuona kaka ake akiwa ameongozana na Zeus "Morning lil sis, heading chuo?" "Bruh, it's Sunday okay Yani Hadi Leo untaka niende chuo, fosho this elimu will kill me one day anyway I'm just going shopping with my friends" "Ooh, good luck then" Alijibu huku akismile "Thanks kaka, mnaenda matembezi" "Yeah it's been a while since nitoke na Zeus, ain't it boy?" Aliuliza huku akimuangalia Zeus "Woof" Zeus Alijibu kama vile kusema ndio "Haha si unaona Hadi yeye kakubali" "Huh Kila nikijaribu kuelewa chemistry yenu nashindwa, anyway later and take care" "Okay, You should take care too".
*********************************************
Raquel akiwa yupo Kitandani bado amejilaza kwa kuwa siku hiyo ilikuwa ni Sunday hivyo ilikuwa ni free day isiyomlazimu aende kazini, alionekana akiwa anawaza kitu flani, more specifically alikuwa anamuwaza mtu flani maana mara ajigeuzegeuze mara achekecheke mwenyew then akiwa bado kwenye ulimwengu wa mawazo simu yake inaita na kumtoa kwenye fikra zake "My charming Apollo" alianza kuongea mara baada ya kupokea simu "My beautiful Raquel, za wewe mpenz" "Mimi mzima baba angu sijui wewe" "Hata kama nilikuwa naumwa, baada ya kusikia sauti yako tu Kila ugonjwa umepotea" "Haha Apollo bhana" "Sijui umesomea chuo gani mambo haya maana hata nikiwa na msongo wa mawazo nikikusikia tu akili yangu yote inakuwa as clear as the sky on a sunny day" "Kwan jaman Apollo umeamka na Nini Leo haha" "Yani leo nmeamka alaf Kila nikifanya hiki au kile akili inasema Raquel Raquel" "Ndo maana, that explains why nilikuwa najing'ata asubuh hii"
*********************************************
Kipindi wawili hao wakiwa wanaendelea kuongea na simu, upande mwengine linaonekana gari Moja aina ya BMW inasimama katika parking lot ya hotel Moja kubwa hapo mjini, Ndani yake anashuka mbaba mmoja mnene kiasi na ukimuangalia kwa mara ya kwanza tu akili yako itakutuma useme 'pedeshee' maana muonekano wake tu ulikuwa unanukia pesa.
Akaingia Moja kwa moja mpaka kweny restaurant VIP na kwenda Moja kwa moja kwenye chumba kimoja na kuingia humo Ndani ambako Ndani yake alimkuta mwanamke ambae yupo kwenye miaka arobaini hivi akiwa amekaa zake akijinywea kinywaji chake mdogomdogo "Nilidhan we ndo nitakukuta umeshafika hapa wa kwanza" aliongea mwanamke huyo huku akiendelea kunywa kinywaji chake "Aah Kuna mambo yalinchelewesha siunamjua Tena yule mwanamke?" Aliketi upande wa pili wa meza hiyo akiwa anaangaliana na mwanamke huyo "Yeah yeah yeah, Apollo mmeshampa taarifa?" "I'm afraid bado kijana ndo kwanza karudi Jana hatukuweza kumwambia on the spot" Mona, ambae ndio huyo mwanamke alimwangalia huyo mwanaume mbele yake kwa makini sana "This plan better work or else nahisi unanfahamu vizuri David, I don't have to tell you what I can do" baada ya maneno hayo akabonyeza kiswitch kidog kilichopo mezani na baada ya muda Ndani ya chumba hiko akaingia waitress mmoja na kuchkua order zao Kisha akatoka.
*********************************************
Vera, anapark gari lake katika parking ya mlimani city na kushuka anatoka hapo direct anaelekea Ndani na kuingia KFC restaurant ambako anakutana na mabeshtie zake wawili wakiwa wametokelezea mmoja alikuwa ni mhindi aitwae Ishani na mwengn alikuwa ni mbongo mwenzake aitwae Lakisha sema wote walikuwa ni wakishua "Late as always" Aliongea Ishani baada ya kumuona Vera amefika kwenye meza Yao "Hihi nilipatwa na emergency bhana sio kwamba nmechelewa on purpose" alijitetea huku akiketi kwenye kiti kimojawapo "Whatever kwanza tushakuzoea" "Does that mean I'm forgiven" "Anyway Lakisha how's about Damian, still bado anakusumbua?" aliuliza Vera "Haha Yani that mwanaume, yeye ni kutwa anataka turudiane na Mimi Sina muda huo" "Wakati hajui kama stage uliofika huwezi hata kurudia nguo" aliongezea Ishani"Of course my gyal Isha Yan I just can't understand like why the fuck should I kurudiana with him, does he thinks that I'm that kind of a fool, he should forget about me"
"Ujue mwanzon I never thought kama yeye ndo angekufanyia vile, kumbe ni nyoka mmoja anaeng'ata na kupuliza" "Babes ebu let's change mada maana nahisi kichefuchefu Kila nikisikia jina lake" "Haha speaking of which, what you guys upto today night?" Ishani aliuliza "Well kwa upande wangu Niko free as a wild bird, what about you Vera" "Mmh bado Sina uhakika, you see Apollo karudi Jana so I think sitopata muda" baada ya kusikia jina la Apollo limetajwa alifurahi na kuona Kati ya taarifa alizosikia na atakazo sikia siku ya Leo, Ishani aliona hii peke yake ndo itakuwa top kabisa "Gyal wait wait wait first, unamaanisha Apollo as Apollo your si ndio?" Aliuliza harakaharaka macho yake yakiwa yanang'ara kwa furaha na tabasamu usoni mwake lililozidi kumfanya azidi kuonekana mzuri, pembeni Lakisha aliangalia juu Kisha akashika Tama kwa kumsikiliza rafiki yake "Oh my God, here we go again" aliongea huku akimuangalia Ishani ambae nae akamuangalia huku sura yake bado ikiwa imevalia tabasamu zuri "Hihihi ila Ishani bhana, anyway, yes it's Apollo kaka angu ndo amerudi" "Jaman Sasa mbona you never told me earlier about your brother" Ishani aliongea kwa sauti ya kudeka kama vile anataka kulia "Hehe, well somebody is obsessed with my brother" akionyesha kufurahishwa, Vera aliongea huku akimuangalia shoga ake huyo "Vera nakununia" Ishani Alijibu Kisha akageuga pembeni kuashiria kuwa amenuna "Khaaah jamani Ishani, haha ndo uninunue Sasa" "Yes, and I don't wanna talk to you, hmmph"
Lakisha akiwa kwa pembeni alimwangalia huku akicheka maana alikuwa akifurahishwa kwa vituko vinavyoendelea mbele yake baina ya Vera na Ishani akaamua achangie nae "So Vera since Apollo amerudi, what do you say if we have a sleepover at The Ferris Mansion so that our princess over here apate time with his Godsent man" baada ya kusikia hivyo tu Ishani aligeuka chap huku tabasamu lake likiongezeka maradufu, akawa anamwangalia Vera kwa macho yaliyokuwa na matarajio chanya, Vera nae akaendelea kusmile "Kwaio kama nikifanya hivyo utaacha kununa?" Aliuliza huku akimuangalia Ishani "As long as umekubali me hata sitoendelea kununa, kwanza nikinuna nakuwa mbaya akati I'm a hot Indian babe" "Haha ouwkeeeey request imekuwa approved" "That's my gyal, come here y'all" aliwavuta wote kwa pamoja na kuwapa a group hug "I love you guys" alimalizia kwa kuwapa kiss Kila mmoja wao
"Anyway guys my sis Priya anaolewa next month I know that hamuwez kukosa in this" "Ooh that's great news kwakweli" "Ndo itakuwa New Delhi" "Hapana wamesema itafanyika Singapore" "That's amazing" "Tuombee uzima tu" "Yeaah, hicho ndo muhimu" baada ya kumaliza story mbili tatu wakatoka na kuendelea na ratiba Yao iliyowapeleka hapo Mliman City ya kufanya shopping na baada ya kumaliza shopping wote wakarudi mpaka parking kweny magari Yao "I'll come pick you all badae" "Aah usijipe tabu Vera tutakuja wenyewe tu" "Basi sawa later then." Wakaagana Kisha Kila mmoja akaondoka na gari lake kuelekea makwao.