Jamii nyingi kabla ya kuwepo kwa utandawazi wanaume ama mwanaume katika jamii alioneka ni kiumbe imara sana kuliko mwanamke.
Jitihada nyingi zilizofanywa na mwanamke hazikuonekana kama zilivokuwa za mwanaume, katika jamii nyingi za waafrika mwanamke alionekana kama chombo cha starehe na kuwa yeye alikua ni kiumbe dhaifu.
Wazazi kwa walezi walikuwa hawapi vipaumbele watoto wa jinsia za like katika masuala ya kupata Elimu, kutoa maamuzi ya familia, kutoa maamuzi yao wenyewe hata kurithi mali.
Watoto wadogo walikuwa wakiolewa angali wadogo na walianza majukumu ya ndoa wakiwa wadogo huku watoto wa kiume walikuwa wakiolewa vipaumbele kwenye mambo yao waliyoyapenda wao. Matabaka haya mawili yaliweza kuleta uwivu miongoni mwao, na waliibuka watu mbalimbali kupambana na halo hiyo iliyokuwa ikiikabili jamii za nyakati hizo.
Katika harakati zao za kujikomboa walihusisha na sekta mbalimbali
Katika nchi ya Tanzania serikali iliweza kuingilia Kati kutokana na wanawake kuonekana wananyanyaswa sana na wanaume. Harakati ziliweza kuzaa matunda lakini kulikua na makosa ambavyo serikali iliweza kutunga Sheria kandamizi dhidi ya watoto wakiume Ilhali dhumuni lilikua ni kuweka usawa lakini Sheria hizo zilimlenga sana mtoto wa kiume kuliko wa kike.
Jambo lililofanya kuwa kinyume chake wanawake wakawa wanaishi kwa uhuru huku wanaume wakiishi kwa taabu. Na hapo jamii haikuweza kihakikisha tena usalama wa watoto wakiume ama jinsia ya kiume. Jamii ziliona kama mwanaume ni mtu hatari na adui kwa jinsia ya kike.
Kutokana utandawazi kukua na kusambaa mwanaume alikutana na changamoto mbalimbali ambazo zilimshusha halo ya kujiamini na kujihisi mwanaume.
Watoto wa kiume waliingiliwa kinyume na maumbile, waligeuzwa kuwa vyombo vya starehe kwa wanawake na baadhi ya wanaume. Mahakama zilikutana na kesi kila kukicha za mwanaume au mtoto wa kiume kunyanyasa kijinsia lakini sauti haikufika mbali katika kupaza saut zao maana jamii nyingi zilimuona mwanaume katika taswira ya ambayo hatokuwa ya kweli.
Mwanaume hakuwa salama katika jamii jambo ambalo liliwaharibu kisaikolojia wanaume na hivo vitendo vya kuingiliwa kinyume na maumbile na wao waliruhusu hivo huku thamani ya mwanaume katika jamii ukawa inapungua maana hata kunabaadhi ya wanaume walibadilisha jinsia zao na kwenda upande wa jinsia ya kike Ili waweze kuishi KWA amani.
Itaendelea....