SURA YA 1
"Naomba simameni!!!. Ilisikika sauti ya kiume iliyokuwa na mikwaruzo.
Watu wote waliokuwepo ndani ya chumba hicho kilichokuwa na walinzi zaidi ya kumi waliokuwa wamevalia mavazi ya rangi ya blue iliyokolea na katika kila walinzi hao wote walikuwa wameshika silaha nzito aina ya SMG, walisimama baada ya sauti hiyo kutoa amri.
Kulikuwa na baridi kali katika chumba hicho kilichokuwa kimefungwa AC zilizokuwa zikipunguza joto la mwezi huo wa kumi uliokuwa ukisumbua jiji la mbeya. Lakini mbele ya kizimba alikuwepo mfungwa aliyevalia nguo yenye rangi ya chungwa; rangi iliyokuwa ina maana kubwa sana kwa mtu atakayebahatika kuivaa, na watu wengi walijitahidi kwa kadri wanavyoweza kutenda haki kila siku za maisha yao kuepuka kuja kuivaa nguo yenye rangi ya hiyo.
Lakini kitu watu wasichokijua kuhusu rangi hiyo ni rangi ambayo ilikuwa ina maanisha kuwa japokuwa sio mfalme wala mtumwa mimi ni moja ya mtu ambaye si miongoni mwa wanaoteseka ama wanaokula matunda ya nchi kwa kivuli cha kujinyenyekeza chini ya wakuu wa nchi. Bali ni mtu ambaye nipo huru japo nipo kifungoni. Aliwaza mfungwa namba 2203 aliyekuwa ameinamisha kichwa huku akiwa kwenye kizimba nyuma yake kulikuwa na walinzi wawili walioshika silaha nzito ijapokuwa alifungwa pingu.
"Naomba tuketi". Ilisikika sauti ya kiume iliyotoka kwa mzee aliyekuwa amevalia vazi jeusi zito lenye mistari myekundu iliyopita kwenye mabega yake kuashiria kuwa yeye ndiye aliyekuwa na mamlaka ya kuisikiza kesi hiyo ya mfungwa aliyekuwa kwenye kizimba.
"Wakili wa upande wa utetezi jiandae kwa ajiri ya kutoa ushahidi kuhusu kesi namba 3002, iliyofunguliwa tarehe 15 mwezi wa nane mwaka 2090, kesi ya jinai juu ya mauaji ya waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mmoja wa karani aliyekuwa mbele karibu na meza kuu ya hakimu alisema na kisha kuketi chini.
Watu waliokuwemo ndani ya chumba hicho walianza kunon'gona na kupelekea kelele zilizosababisha mzee Yule ambaye alikuwa hakimu wa kesi hiyo kugonga meza kwa kutumia nyundo iliyotengenezwa kwa mbao aina ya mninga.
"Utulivu tafadhali". Alisema mzee Yule
"Wakili wa upande wa serikali jiandae pia kutoa ushahidi wako juu ya kesi hii". Aliongeza kusema mzee Yule.
Mwanamke mwenye rangi ya maji ya kunde alisimama na kuashiria uwepo wake kama wakili wa upande wa serikali na kisha kuketi.
"Wakili wa upande wa utetezi naomba sogea mbele kwenye kizimba uweze kuwasilisha ushahidi wako". Ilisikika tena sauti ya hakimu Yule ambaye alikuwa mzee sana.
Labda kutokana na uzee wake ndiyo maana alikabidhiwa kesi hiyo kubwa kuwahi kutokea katika nchi ya Tanzania na yeye ndiye aliyeshika mamlaka ya uhai wa mfungwa aliyekuwa kizimbani. Hivyo alikuwa tayari kuweza kumsogeza kijana huyo kwenye hukumu ambayo ilikuwa haikwepeki kwa namna moja ama nyingine.
Mfungwa yule aliinama chini na alikuwa akikumbuka siku hiyo yaliyotokea mauaji ya waziri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Huenda alitamani kurudisha muda nyuma na kufanya maamuzi yaliyokuwa sahihi kwake lakini kwa wakati huo maamuzi yalikwisha fanywa na matokeo ya kitendo alichokifanya ndiyo kilimuweka mbele ya kiti hicho cha hukumu.
Mawazo yake yalimpeleka mbali na kufanya kushindwa kufatilia kesi yake kwa sababu ya msongo wa mawazo.
Mawazo yake yalimpeleka siku ya ijumaa tarehe 12 mwezi wa kumi mwaka 2090.
"naomba nipigie haraka iwezekanavyo akipita mwanjelwa". Ilisikika sauti ya mwanaume simuni.
"Ondoa shaka juu ya hilo dravo, kwa sasa bado msafara wake upo uyole akianza safari tu nakutaarifu". Ilisikika sauti ya kike kutoka upande wa pili.
Dravo alikata simu kisha kufungua begi refu jeusi na kutoa silaha ya masafa marefu aina ya long range M113 rifle na kuhakiki uwepo wa vifaa vyote vya silaha hiyo kasha kufunga begi hilo na kupanda gari jeusi iliyokuwa ikimsubiri nje ya chuo cha biashara kilichopo maeneo ya barabara ya kuelekea chunya.
Gari ilishuka kwa kasi na kukunja kushoto kufata barabara inayoelekea kanisa katoriki lililo karibu na hospitali ya Ks. Na kufata barabara ya chuo cha mzumbe na kutokea katika njia ya meta. Na kuingia ndani ya hospitali hiyo ya wazazi. Kwa haraka dravo alipanda lifti illiyompeleka juu ya jingo lenye ghorofa zisizopungua ishirini. Na kutokana na ushirikiano aliopewa na wahudumu wa hospitali hiyo aliweza kupita bila kuulizwa maswali mengi kuonesha kuwa walikuwa wamepewa taarifa juu ya ujio wa mtu huyo.
"Msafara wa waziri mkuu unapita maeneo ya Soweto, jiandae kumaliza kazi dravo".uliingia ujumbe kwenye simu kutoka kwa mwanadada aliyeongea na dravo nusu saa lililopita.
"Kila kitu kipo tayari, andaa njia ya kuweza kuwachanganya walinzi wake wa karibu ili niweze pata nafasi ya kumaliza kazi". Aliandika dravo ujumbe huo na kuutuma kwa mwanamke Yule.
Haraka bila kupoteza muda alitoa silaha iliyokuwa ndani ya begi lile jeusi na kuiunganisha silaha hiyo iliyokuwa imefunguliwa. Ndani ya dakika chache aliweza ifunga silaha hiyo na kuwa silaha kamili kwa ajili ya kumaliza kazi iliyomtuma; alifunga kiwamba sauti mbele ya mdomo wa silaha hiyo na kutumia darubini iliyokuwa kwenye silaha hiyo.
Dravo aliweza kuona msafara huo uliokuwa ukipita katikati ya jiji la mbeya na kukaribia makutano ya barabara nne yaliyopo jijini mbeya.
Gari sita aina ya v8 zilizokuwa na rangi moja zilikuwa zikishuka kwa kasi na kutoa mlio wa kin'gora kilichoweza kusimamisha magari yaliyokuwa yakitoka pande zote na kuacha njia moja ya gari hizo sita.
"gari ya tatu kutoka mwisho ndiyo yupo waziri mkuu". Uliingia ujumbe mfupi kutoka kwa Yule mwanamke aliyekuwa akimpatia taarifa dravo.
Bila kupoteza muda aliusoma ujumbe ule na kwa kutumia darubini iliyokuwa kwenye silaha hiyo aliweza kuona gari la tatu toka mwisho lililokuwa likiongozwa na waendesha piki piki wanne na kuweka dhahiri kuwa humo ndimo alimo waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka huo 2090.
Dravo kijana mwenye umri wa miaka isiyopungua thelathini aliweza kuona sura ya waziri mkuu na bila kupoteza muda alifyatua risasi iliyopasua anga kwa kasi ya ajabu majira ya saa tisa alasiri na kuweza kupenya katika kioo cha dereva wa gari hilo na kumpata dereva wa gari lile ambaye alikufa palepale na kusabababisha kuvurugika kwa msafara huo na kuweka hali ya hatari katika eneo hilo la makutano ya barabara. Dravo baada ya kufyatua risasi hiyo moja iliyompata dereva huyo lengo lake la kwanza liliweza fanikiwa na kumfanya aweze ingiza hofu kwa mtu ambaye alikuwa muhimu kwa taifa.
"Zungukeni gari la mheshimiwa haraka". Ilisikika sauti kutoka moja ya walimzi waliokuwa wamevalia mavazi ya kijeshi. Polisi waliokuwa wakiongoza msafara na piki piki waliweka vyombo vyao vya usafiri pembeni na kutoa silaha zao aina ya bastora zilizokuwa zimeshikwa kikakamavu mikononi mwao.
Macho yao yalipepesa huku na huko kuangalia katika majengo marefu huenda ndipo silaha ilikotokea.
Lakini walishindwa kujua ni wapi mtu anayehusika na shambulio hilo wapi alipo. Majengo marefu yalikuwa mengi katika jiji hili lililoendelea kwa kasi ya ajabu na kulinganishwa na jiji la dar es salaam ambalo kila kona ilijaa majengo marefu ya kila aina.
"Hakikisha unamlinda mheshimiwa . kuna hatari ya shambulio la kigaidi". Alisema Yule mlinzi aliyekuwa amejazia mwili wake kutokana na mazoezi hasa ya kubebe vitu vizito.
Mambo yote yaliyokuwa yakiendelea dravo aliweza kuona na kutafuta upenyo wa kumaliza kazi iliyomleta.
Juu ya ghorofa ya hospitali kuu ya wazazi meta ndipo alipoketi jasusi huyo aliyekuwa tayari kubonyeza kifyatua risasi na kutokomea kusikojulikana. Alifyatua risasi hiyo tena baada ya utulivu wa dakika moja uliotokea katika jiji hilo na kutokana na kiwamba sauti kilichofungwa mbele ya silaha ile haikusikika sauti ya aina yoyote ila matokeo yalionesha kwamba risasi imefyatuliwa na kumpata waziri mkuu upande wake wa kushoto wa kifua chake.
Walinzi walifanya kosa kubwa sana kutaka kumhamisha gari waziri mkuu na kutokana na maamuzi hayo yaliacha upenyo wa jasusi huyo kufyatua risasi hiyo ya kuamua hatima ya uhai wa waziri mkuu.
Walinzi wale walichanganyikiwa na kuanza kufyatua risasi angani bila kuwa na mpangilio kwa lengo la kutaka kumtisha mtu huyo aliyejificha sehemu ambayo wao walishindwa kumuona. Lakini mwisho wa siku walizua taharuki na kusabababisha jiji hilo kuvurugika kwa amani katika maeneo hayo.
Watalii waliokuwa katika hoteli kubwa walishtushwa na tukio hilo pamoja na wageni mbali mbali katika jiji hilo lililokuwa kwa kasi ya ajabu katika kipindi cha miaka 70.
Waziri mkuu alianguka chini na damu zilianza kutoka kwa kasi katika kifua chake kuashiria kuwa muuaji alidhamilia kumtesa waziri huyo na kumpa muda wa kupata maumivu.
"Kazi imekamilika". Aliandika ujumbe baada ya kufunga silaha yake na kuweka ndani ya begi hilo jeusi na kushuka kutumia lifti za ghorofa hilo.
"Vizuri". Alijibu Yule mwanamke aliyekuwa akiwasiliana na dravo toka mwanzo.
Ndani ya dakika kumi alipanda gari lake alilokuja nalo na kukunja kushoto toka hospitali hiyo ya wazazi.
Gari ilishuka mlima huo wa meta na kutokomea kusikojulikana.
Simu ya dravo iliita baada ya ukimya aliokuwa nao katika gari hilo.
"Mbona umempiga risasi ya kifua?. Haujatimiza makubaliano yetu". Ilisikika sauti ya Yule mwanamke na kwa sauti ya upole dravo alijibu
"Kwa nini kumuharakisha kwa Israeli mtoa roho kabla hajajua kosa lake ni nini? Nimempatia muda mfupi wa kukumbuka jinsi alivyoishi hapa duniani na ondoa shaka kuhusu kummaliza hatofikisha nusu saa utasikia taarifa ya kifo chake. Najua nimekiuka maagizo yako ya kumpiga risasi ya kichwa lakini hii naona inafaa zaidi kutokana na jinsi alivyokutendea na kunitendea miaka kumi iliyopita." Alisema dravo kwa sauti ya chini huku akikanyaga mafuta ya gari hilo.
"Una hakika na unachokiongea? Aliuliza Yule mwanamke
"Ondoa shaka juu ya hilo kisasi chako na changu kimetimia baada ya miaka mingi. Agiza kinywaji sehemu yoyote nitakulipia." Aliongea dravo huku akionesha tabasamu
"Sawa dravo tukutane hoteli moja wapo tufurahie mafanikio ya kazi yetu na kisasi kilichochukua muda mrefu kukitimiza". Ilisikika sauti ile ya mwanamke Yule.
"Tukutane green city hotel…jitahidi uwahi mapema jiji liko katika hali ya hatari na hawa polisi wako tayari kumkamata yoyote kwa hili tukio lililotokea.
Kuwa makini Maria. Simu ilikata baada ya kumaliza mazungumzo hayo ya watu wawili.
Waziri mkuu alikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa mbeya haraka iwezekanavyo lakini safari yake iliweza kuishia ukingoni kama mawimbi ya bahari yanavyoishia ukingoni.
Ilikuwa saa kumi na nusu ndipo madaktari walithibitisha kifo cha waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania . vyombo vya habari vikuu Tanzania ikiwemo TBC kilithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kijasusi na kuweka hofu kwa wananchi Tanzania nzima.
Nchi nzima iliingia katika hali ya hatari na watu hawakuruhusiwa kutoka nje zaidi ya saa moja. Watu wote walijifungia majumbani mwao hasa katika jiji lilikotokea tukio hilo. Vikosi zaidi ya vine vya jeshi la wananchi wa Tanzania vilimwagwa kutoka vikosi mbali mbali nchini.
Ndani ya nusu saa hakukuwepo mtu yeyote aliyethubutu kutoa pua yake nje haikujarisha alikuwa ni wa rika gani wote walijifungia ndani kama kuku wa kienyeji.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alitangaza hali ya hatri baada ya kutokea kwa kifo cha waziri wake mkuu na kwa mujibu wa katiba haitachukua siku zaidi ya saba, itampasa raisi kupitisha jina ambalo wabunge watalipigia kula kuwa ndio waziri mkuu wa nchi ya Tanzania.
Taarifa zilisambaa lwa kasi katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Baadhiya watu walifurahishwa na kuuawa kwa waziri mkuu huyo na wengine wakitoa majonzi juu ya kifo cha waziri huyo. Waliojua maana halisi ya kifo cha waziri huyo walikuwa katika hoteli ya green city hotel wakiendelea kunywa vinyo nyekunde taratibu wakisindikizwa na mziki wa taratibu uliokuwa ukichochcotyea furaha ndani ya chumba kimoja katika hoteli hiyo. Chumba namba 107 ndiyo chumba pekee katika hotel hiyo kilichokuwa kinapiga mziki kwa sauti ya juu na kuwafanya wateja wengine kuwa na wasi wasi juu ya watu waliokuwamo ndani ya chumba hicho.
Mlango wa chumba hicho uligongwa na meneja alikuwa amesimama nje ya chumba hicho na kuwataka wapunguze sauti maana inasumbua wateja wengine.
"Nimelipia hiki chumba nina haki kufanya chochote katika chumba hiki. Au kuna sheria yoyote uliyoandika kuhusu kuburudika katika hotel hii ni sawa na kuvunja sheria? Aliuliza mwanamke aliyekuwa amelewa kutokana na mvinyo kumkorea sawa sawa.
"hatukatazi kuburudika ila kutokana na hali ya hewa ya siku ya leo sio vizuri kupiga mziki mkubwa kiasi hicho". Alisema Yule meneja aloyekuwa na kitambi
Hali ya hewa gani?
Kwani kuna kimbunga huko au mvua kubwa?
"Aliyekufa ni baba ako au babu yako acha tujimwage bana achana na sisi". Alijibu Yule mwanamke na kufunga mlango kwa kasi na kumuacha meneja wa hoteli hiyo akipigwa na bumbu wazi.
"Nani tena huyo anatuharibia starehe yetu? Aliuliza Dravo huku akinyanyuka kutoka kitandani na kumfata mwanamke huyo aliyekuwa akikata mauno kutokana na mziki uliokuwa ukipigwa toka kwenye spika za chumba hicho.
"achana naye nishampasha ya kwake. Kwani kifo cha huyo mpuuzi kinahusianaje na sisi kuburudika potelea pote acha tufurahi maana kifo cha filauni ni furaha kwa wana wa Israeli. Alisema mwanamke Yule huku akimsogelea dravo na kuanza kumbusu mdomoni. Ndimi zao ziliweza pambana na kuamsha hisia kali zilizopelekea wawili hao kuamisha mechi na kuamia kwenye kitanda kikubwa chenye tandiko la sufi.
Haraka bila kupoteza muda dravo aliweza tumia ujanja wake kama mwanaume na kuanza kuuchezea mwili wa mwanadada huyo ambaye alikuwa mweupe mwenye rangi ya kuvutia. Siku hiyo dravo aliweza kuvunja amri ya tano na ya sita bila kupepesa macho huku kitanda kikiwa shuhuda asiyeweza toa neno lolote wakati huo, kilikuwa hakina budi kusaidia kuvunja amri hiyo ya sita.
Usiku huo ulikuwa usiku wa furaha kwa wawili hao na dravo aliweza kuwa mmoja ya mtanzania aliyeweza kummaliza waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Jiji la mbeya kwa usiku huo liliweza kufanyiwa doria ya hali ya juu na utulivu wa hali juu ulikuwepo; hata mbwa waliokosa makazi hiyo siku huenda walipeana taarifa juu ya kilichotokea maana hakudhurula hata mmja.
Vikosi vinne vya kijeshi viliweza fatilia na kuandika ripoti kuwa kifo cha waziri mkuu kimesababishwa na kupigwa risasi ya kifua ambayo iliiingia kwenye moyo wake na kusababaisha mshipa mkuu wa kusambaza damu kwenye mwili kupasuka na kusababaisha kupoteza damu ya kutosha iliyochangia kifo chake.
"Tafiti zinaonesha kwamba risasi iiyo muua imetoka kwenye silaha za masafa marefu na jasusi aliyesababisha kifo hicho ni kikosi cha watu waliobobea katika matumizi ya silaha hizo za mbali zilizopelekea kifo cha waziri mkuu". Alilipoti kamanda wa polisi wa jiji la mbeya amabaye aliambatana na kikosi cha jeshi cha jeshi la wananchi wa Tanzania.
"Tutahakikisha hatutolala kuahakikisha tunamtia hatiani jasusi huyu anayehatarisha usalama wa nchi. Alisema kamanda wa jeshi a polisi kanda ya kusini katika vyombo vya habari mbali mbali vilivyofika eneo la tukio.
"anasema nini huyu? Aliuliza Yule mwanamke akiwa juu ya kifua cha dravo.
"Muache atomize wajibu ila sidhani kama wataweza nikamata kwa mafunzo niliyopitia labda nijikamatishe mwenyewe maana nishatimiza lengo langu na sidhani kama nina cha kupoteza". Alisem dravo na kubadili chaneli na kuweka mziki kwenye runinga iliyokuepo kwenye chumba hicho.
'Nadhani muda umefika wa kumtafuta franco".aliongea dravo
"ni simu moja tu kila kitu kitakuwa wazi juu ya uovu alioutenda waziri mkuu". Alisema Yule mwanamke.
"jitahidi baada ya kukamilika kwa zoezi la franco baada ya siku tatu nenda jikamatishe na useme wewe ndio unahusika na kifo cha waziri mkuu". Alionhgeza Yule mwanamke
"Mimi nitajitahidi kwa namna yoyote usipate adhabu ya kifo, bado kuna kazi nahitaji uende kuifanya huko gerezani."
"kuhusu gereza utakalo fungwa tutapeana taarifa, ila kumbuka lengo la wewe kwenda kujikamatisha sio kwenda kufa ni kwenda kutimiza kazi ya kumaliza wale wote waliohusika na tukio lile mwaka 2080". Aliongeza Yule mwanamke amabye alimaliza kutoa maelekezo na kunyanyuka kitandani taratibu kuingia bafuni.
"Nifate au umetosheka". Alitoa kauli iliyomfanya dravo atokwe na mate huku akiutazama mwili wa mwanamke huyo uliokuwa na kiuno chembamba kilichojengwa na makalio makubwa.
Waliweza tumia muda uliobaki usiku huo kuendelea kuvunja amri ya sita na taratibu kuifa nya miili nyao myepesi kwa ajiri ya siku nyingine. Sauti za nasibu zilisikika katika bafu la chumba hicho kuashiria mambo yalikuwa mazuri baina yao.
Je nini kitaendelea katika sura ya pili? vuta chini kuendelea kujisomea. maoni yako ni muhimu sana mpenzi msomaji, nawapenda.