Ilikuwa desturi na mila za jamii yetu ,kila baada ya miaka mitatu kungetolewa kafara katika msitu wa Kibiongo, mahali ambapo paliheshimiwa zaidi kutoka enzi za bibi zetu.wakasonokye akiwa kiaongozi wa hafla hizi na mlinzi wa Dhehebu hili alilowachiwa na babake kandamoja ,alijitolea kwa jino na ukucha kuakikisha kuwa hakuna siku ,mwezi ,mwaka wala sekunde maamuzi ya miungu wa mzimu huu yangekosa kutekelezwa.
mababu walikua wamekubaliana kuwa kila baada ya kipindi cha miaka mitatu "sadaka " iliyo hai ingetolewa ili kuzidi kukilinda kijiji na wanajamii wake. Ilikuwa kazi kuu ya wakasonokye kutimizia mababu wa mzimu haki yao, kwa ushirika kwa wanakijiji.
Walilazimika kutafuta kipusa aliye bikira binti bikira ndio sadaka ya wakuu !. Licha ya kuwa ilikuwa kibarua kingumu sana kubainisha binti bikira na asiye bikira kwani katika ajinabu hizi mabikira walikuwa wameadimika kama mkonjo wa nyoka.Mizimu ilikuwa imewaachia wanao mashariti mangumu ambayo yangegharimu maisha yao iwapo hayangefuatwa kikamilifu.
wakasonokye alitimiza majukumu yake kwa wepesi sana katika miaka ishirini ya kwanza kwani haikumwia vingumu kupata mwanamwali katika janibu zile, mabinti bikira walikuwa wengi na kutokana na hali duni ya elimu kijijini gazija na maeneo yaliyokizunguka ,wazee wangekubali kuwatoa binti zao moja baada ya mwingine ,waliamini ujaala ungeleta mtoto mwingine atakaye chukuwa nafasi ya yule aliye tolewa kama kafara.
Benito akiwa ghulama mtanashati ,kimo cha kati na mwenye misuli 'American height' kama wanavyoitwa na mabinti wa majira haya,Alitokea kusalitika kwa penzi la Farida.
usuhuba wao ulianza Benito akiwa na miaka kumi na misita naye farida akiwa na miaka kumi na minne.kipindi hiki wiote wakiwa wananfunzi wa shule ya upili ya Tandale.Farida alikuwa binti mwenye shingo ndefu iliyokishikilia kichwa chake chenye udo uliong'aa kila mara kama nyota usiku mpevu.macho yake yakitwaa rangi ya kipekee ya samawati.pua lake kama kisu kibutu.midimo yake ilikengakenga kwa tambasamu la kuunajisi ubikira wa ajuza wa miaka tisini ambaye mguu wake wa tatu ulisahau kutembea miaka hamsini iliyopita.
Yasemekana huyu aliumbwa wakati muumbaji ametambasamu,shingo yake ilikuwa ile ya kukata, masikio yake yalikuwa yamemkaa vyema pale kichwani.Meno meupe pe! yaliyopagwa yakaitikia wito pale kinywani.Ulimi wake wenye ncha na uliotoka inje akipitisha kwenye meno yake.Binti huyu alikuwa kamilifu.wengi wa mabinti wenzake na hata walimu wa kike walimuonea gere.Katika maisha ya binti huyu hakuwai vutiwa na mwanamme kiasi kile cha Benito, kweli benito na farida walikuwa wamesalitika katika mahaba ,ambayo kila mmoja alikuwa radhi kulipingania na kulikuza kadri ya uwezo wake ata ikigharimu uai wake.Benito kwa upande wake alikuwa mwenye sura ya jamali,misuli ilimtutumka katika baadhi ya viungo vya mwili wake .Alikuwa jamali aliyewatesa wengi kipindi kile cha ujana wake, pale shuleni na hata kijijini...
Mara kadhaa Farida alijikuta katika mgogoro na wanafunzi wenzake pale shule kwa sababu ya kijana huyu aliyeiteka nafsi yake na kuhushtaki moyo katika mahakama kuu nchini na kuhukumiwa kifungo cha maisha mle gerezani na kazi ngumu kila asubuhi na jioni.
Benito alikuwa bumbumbu masomoni kwani angeunga moja na moja apate kumi na moja,Angesoma hadi usiku wa manane angalau ili kuona kama alama zake masomoni zingeimarika lakini wapi ama kweli kupanda mchongoma ndio kazi kushuka si kazi.
Mzee katiki na bibiye Mutheu walimpenda Farida ,kweli huyu binti alikuwa boni la jicho lao,Hakuwa kifungua mimba tu bali alikuwa mtoto wa pekee kwa ile jamii.