Chereads / The queen of Alchoraz:NDOTO YA UHURU WANGU / Chapter 1 - Sehemu ya 1:Mbali na maisha yangu

The queen of Alchoraz:NDOTO YA UHURU WANGU

Author_Bahati
  • --
    chs / week
  • --
    NOT RATINGS
  • 21.4k
    Views
Synopsis

Chapter 1 - Sehemu ya 1:Mbali na maisha yangu

Ni usiku mnene ndani ya mji wa Dar es salaam,mdada mrembo Asteria alikuwa akikimbizwa na wanawake kama wanne Hivi.Miongoni mwao alikuwa dada yake wa kambo aitwae Fahyma mwenye asili ya kiarabu.

Asteria akiwa anakimbia akajikuta akijikwaa na kudondoka chini kama mzigo.Fahyma na wenzake wakamfikia na kumzunguka.

"Wewe si unajitia mjeuri siyo.Unataka kuwa ndugu yangu ushee baba na mimi eeh.Sasa adhabu yako ni kifo pekee "Akasema Fahyma kwa sauti ya kikatili mno.

"Kwanini unanifanyia hivi Fahyma?Nimekukosea kitu gani hasa?"Asteria akauliza akilia vibaya mno.

"Hujui kosa lako eeh...wala usijali utalijua tu mtoto mzuri Sawa eeh"Fahyma akamkejeli na kumpiga kofi zito Asteria.

"Sasa leo umeisha ujue."Akasema na kumnyanyua Asteria ili amuue vizuri.

"Nataka nikuue kwa risasi kwa hiyo kimbia!"Fahyma akasema na kumfanya Asteria akimbie kujaribu kama atatoboa ama la.

Akiwa anakimbia, ghafla akajikuta akidondoka baada ya kupita Sehemu asiyoielewa.Akahisi kama anaondoka kwenye korongo vile.Hapana!Au alikuwa anadondoka kutoka kwenye mbingu nini?

"Pwaaa!"Akajikuta akidondoka kwenye mto mkubwa na kuzama chini kwa kasi mpaka akajibamiza Kichwa kwenye jiwe na kujikuta akipoteza fahamu kwa muda mfupi kabla hajagundua yupo nchi kavu.

"Atakuwa sawa kweli huyu?"Watu walikuwa wakiulizana na kumfanya Asteria ashtuke kujua ni kina nani.

Hapo akawaona watu waliovalia mavazi ya kale sana.

"Kina nani nyie?"Asteria akauliza akirudi nyuma taratibu.Watu wote walikuwa na asili ya kiarabu.Asteria akatazama kando na kuona watu wakiwa juu ya farasi.Oh Mungu wangu inamaana yuko ufalmeni eeh....

"Binti mrembo kweli.Utanifaa sana.Nitakuuza kwa sarafu za dhahabu nyingi kwa urembo wako."Akasema mwanaume mmoja mtu mzima na maarufu kwa biashara ya kuuza wanawake.Du!Kaingia pabaya.Mbona haelewi elewi.