Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 243 - UFINYU WA AKILI

Chapter 243 - UFINYU WA AKILI

Akiwa ofisini kwake Li alipokea simu kutoka kwa Edrian akimtaarifu kuwa wangeingia na ndege ya alfajiri ya siku iliyofuata. Furaha ilikuwa wazi kwenye sauti ya Edrian alipokuwa akizungumza.

"Vipi lakini niliongea na mama naona anafurahia sana uwepo wa Beruya hapo nyumbani!"

"Aahm n- nadhani ni kawaida yake kufurahia akipata mtu anayefanya vitu apendavyo" Li akamjibu, na kama Edrian angekuwepo kushuhudia uso wake angelimcheka sana maana alikuwa alichora duara kwenye karatasi iliyokuwa mezani..

"Eeeeh, hebu nambie anamfanyia nini mama yangu"

"Eh!," Li akashtuka, "aaahm hahahaha m-mambo ya kupika bro unasahau tena"

"Mh, hivyo tu, haya! Ed akaguna kisha akamwambia "unajua sijamwambia mama kama narudi najua atasisitiza nije na Retha"

"Kwani kuna shida ukija naye nyumbani?" Li akauliza

"Hapana, mama yake Retha aliniomba nimpeleke nyumbani binti yake mara tutakapofika"

"Oooh mama kamkumbuka binti yake" Li akajibu

"Kama ambavyo mama Simunge amenikumbuka"

"Aaah, lakini kweli"

Wakaendelea na mazungumzo huku wakigusia mambo ya kiofisi. Li hakumwambia kilichotokea akiendelea kutunza ahadi yake kwa Allan.

*****************

Ķatika jumba la Martinez, mambo yalikuwa magumu kwa upande wa Joselyn. Alisimama pembeni ya kochi alipoketi baba yake huku miguu akiwa ameinyoosha juu ya meza.

"Baba kama sio sasa hivi nitampoteza Ed milele, naomba uniruhusu nifanye kitu, unajua siwezi kufanya chochote bila simu yangu?" Sauti ya Joselyn ilikuwa ya kumsihi Martinez kumruhusu walau arudishiwe simu yake

"Hapana mwanangu, sitaruhusu uharibu taswira ya familia hii kwa mara nyingine" Martinez akamjibu huku jicho lake likiwa kwenye kioo cha kompyuta mpakato iliyokuwa miguuni pake.

"Mmhhh" akashusha pumzi Joselyn, akataka kusema kitu lakini baba yake aliinua jicho na kumtazama kiasi cha kushindwa kuendelea kusema

"Sikia Lyn, ni aidha uchague kuniamini mimi na mipango yangu au uanzishe vita na mimi ambapo unajua matokeo yake." Martinez aliposema hivyo akarudisha macho yake kwenye kile alichokuwa akifanya

"Baba tafadhali" Joselyn akasogea na kupiga magoti karibu na kochi aliloketi baba yake. Macho yake yakapita kwa haraka kwenye kioo cha kompyuta aliyokuwa akifanyia kazi Martinez

Kile alichokiona kikamfanya ainuke na kumtazama baba yake kwa huku akikunja sura. .

"Baba unataka kufanya nini ah!!" Akauliza huku sauti yake ikibeba hasira na uchungu

Martinez hakujibu neno lolote zaidi kumtupia jicho la kumpuuzia kisha akaendelea kuzungusha kipanya kichokuwa mkono mwake

"Baba unajaribu kufanya nini na hizo picha za huyo mwanamke na Ed! Unataka kunizunguka sasa eeeh?" Sasa machozi yalikuwa yakilenga kwenye macho ya Joselyn

"Mhhh" akaguna Martinez kisha akaachia mkono wake uliokuwa kwenye kompyuta! Akamtazama Joselyn

"Unajua sipendelei mtu asiyekuwa na akili, sasa naona kukufungia ndani kumefanya ufinyu wa akili yako kuwa wazi. Nimeketi hapa kuhakikisha natengeneza njia ya wewe kumrudia Simunge na wewe unabwata tu kama bata...mtcchh" akasonya na kuendelea na kazi yake

"Lakini baba hizo picha ukizipeleka kwa watu watajua mimi sikuwahi kuwa naye"

"Nani kakwambia hivyo? Hebu tulia siku chache zijazo utashukuru kuwa nimefanya hivyo kwa faida yako. Au nikuache ukajibu maswali ya Inspekta Sunday?" Akamuuliza huku tabasamu lenye dhihaka likitoka upande mmoja

Joselyn akamwangalia baba yake kisha kwa sauti ya chini akamjibu "Hapana baba"

"Basi tulia, vumilia masaa machache ili usiharibu maelezo yangu niliyompa Inspekta. Kaniletee maji labda ukifanya majukumu ya wengine itakusaidia kutuliza hiyo akili yako" Martinez akaendelea kuchapa kwenye kompyuta yake..

Joselyn akageuka na kuelekea jikoni kwa unyonge akiwaza maneno aliyoambiwa na baba yake. Alishukuru kuwa ile kesi ya akina Bruno, baba yake alifanya awezalo kumnusuru. Hakika aliwatuma wale vijana kumfanyia vurugu na kumteka Aretha na Charlz. Inspekta Sunday mara tu alipowahoji na kuchunguza simu zao namba ya Joselyn ilikuwa kwenye orodha ya namba zilizopigwa mara ya mwisho.

Martinez akiwa na mtu wake ndani ya polisi aliweza kupata taarifa mapema na hivyo akaichukua simu ya Lyn.