Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 237 - KICHWA KIGUMU

Chapter 237 - KICHWA KIGUMU

"Unamaanisha kulikuwa na kamera nyingine uliyoweka?"akauliza Allan huku akionekana kupatwa na mshtuko

Li akamshika begani " Sisi ni ndugu Allan, isikusumbue sana. Acha Captain aangalie halafu tutaona nini cha kufanya"

"Kuna kitu kinaendelea sikijui Comrade?" Akauliza Captain ambaye alikuwa ameketi kwenye kiti kilichopo ofisini kwa Ed huku akitumia kompyuta mpakato.

Watatu hawa waliporudi kutoka SR wakaelekea ofisini kwa Ed wakimuacha Alphonce ambaye alielekea ofisini kwake. Captain aliketi huku akipekua faili za picha kwenye kompyuta yake na wakati huo huo akiimarisha mfumo wa usalama kwenye ofisi hii ya Ed...

Allan akainama chini kisha akamtazama Li lakini Captain akaendelea "Renatha najua ana kazi ametumwa hapa ila sio hiyo inayosomeka kwenye barua yake"

Allan akameza mate kisha akafumbua kinywa kutaka kusema lakini kabla hajasema Captain akasema kwa ghafla

"What!!" akahamaki na kuwafanya Allan na Li wote wamtazame

Akaonekana kijana ambaye alivaa kofia nyeusi, suruali na shati yake navyo vilikuwa vyeusi. Alikuwa mfupi na mwenye mwili wa wastani.

"Huyu ni nani?" Allan akauliza kwa mshangao mara alipoona ile picha

Captain akamwangalia Allan kisha akaongeza ukubwa wa picha zile hata kukaribia kuuona uso wake lakini bado hawakuweza. Dakika chache baadae wakamuona Renatha akimfuatilia yule kaka wamekutana wote kwenye mlango wa kuingia kwenye ofisi ya Ed na Allan. Wakawa wakibishana huku Renatha akisimama mbele kumzuia kuushika mlango wa Ed, ikawa wote wakashtuka wakaelekeza macho kwenye mlango wa kuingia ambapo inaonesha walisikia hatua za mtu, Renatha akatoa funguo wa ofisi ya Allan akafungua na wakaingia ndani..

Allan hakuamini alichoona, "Renatha alipataje funguo za ofisi yangu?" akawaza, Li akamshika bega kumtia moyo

Mara walipoingia hawakuwaona wakitoka isipokuwa akaonekana Allan aliyefika na kushangaa kuona mlango wa ofisi yake ukiwa wazi

"Walipitia wapi hawa aiseee?, hapa tunahitaji kuwajulisha watu wa usa___" Akauliza Li lakini akakatisha maelezo yake pale alipoona sura ya Allan ikiwa na mashaka, akamwambia

"Tuko pamoja Comrade" kisha akamwambia Captain

"Comrade tunaweza kulitunza hili kwanza kabla ya kumwambia Bro?"

Captain akainua uso na mikono yake ikaacha kubonyeza kompyuta akamwangalia Li

"Bro atanitoa macho akigundua, tell me the truth, what's going on?"

Kabla Li hajampa jibu Allan akainuka na kuzunguka na kwenda kukaa kwenye kochi

"Captain" akamuita taratibu na kuwafanya Li na Captain wamwangalie wakiacha kutazama kompyuta

"Unawaza kunipa leo na kesho nipate ukweli wa jambo hili? Nataka nijue ni kwa namna gani waliweza kutoka ndani ya ofisi yangu. Nakuahidi nisipojua nitakuruhusu umwambie Bro"

Captain akamwangalia Li ambaye alitikisa kukumshawishi akubaliane na ombi la Allan

"Basi sawa, hata hivyo nitaingia kuhakikisha mwenyewe hakuna mlango wa siri au tundu walipita maana kwa dirishani haiwezekani!"

"Asante sana bro" Allan akamwambia

"H ahahha poa bro, ila kuwa makini na Renatha. Mimi sina kichwa kigumu kuelewa unachojisikia haha" akamwambia

"Oooh" Allan akajibu kisha wote wakainua na kuelekea ofisini kwa Allan..

*********

Dakika 45 kabla ya Captain kufika, ofisini kwa Beno.....!

Renatha alikuwa ameweka kifaa cha kusikilizia sikioni kwake huku akiendelea na kazi, ghafla akashtuka baada kusikia sauti za watu waliokuwa wakizungumza kupitia kifaa chake

Akaacha kubofya kwenye kompyuta yake akasikiliza huku sura yake ikibadilika kutoka kwenye heri na kwenda kwenye shari

"Huyu mpuuzi nilimwambia hawa watu wana uwezo mkubwa kiteknolojia hakunisikia" akawaza wakati akiendelea kusikiliza

"Huyu Captain ni nani?" Akajiuliza mara aliposikia akitajwa kwenye mazungumzo aliyokuwa akiyafuatilia. Ni wazi kuwa Renatha alikuwa akisikiliza mazungumzo kutoka ofisi ya Allan, yaani kulikuwa na kifaa kilichompa nafasi ya kufuatilia yote yanayoendelea ofisini ile.

Akachukua kalamu iliyokuwa pembeni akawa akiandika, ghafla akaacha,

"Shiiit...what, Allan what?" Akainuka kwa mshangao halafu akaketi taratibu

Kichwani akakumbuka maneno aliyomwambia BM siku ile alipoonana na Ed