Edrian akatulia kidogo na macho yake yakaelekea kwenye upande ambao aliketi Aretha kisha akaendelea na uwasiliashaji huku akigusia changamoto ambazo wamekutana nazo na namna walivyozitatua na zile ambazo bado hazijatatuliwa hatua gani zinachukuliwa.
Alipofika mwisho, akaruhusu maswali, watu watatu waliuliza maswali na yote yakajibiwa ipasavyo,
"Thank you everyone for your time, I am so grateful to Global Mining Institute for organizing this Conference. To my fellow SGC global team, thank you Craig and my amazing staff.
And lastly, to my lovely fiancee and future wife Aretha Thomas, thank you for being here with me. Have a wonderful day everyone!"
Akatoka mahali aliposimama na kuelekea kwenye kiti chake huku makofi yakifuata.
Ratiba iliyofuata Ed hakutaka kushiriki, akaomba udhuru huku akimwachia Craig na Britney kuendelea na yeye akaondoka na Aretha kurudi hotelini ambapo walibadilisha nguo na kuvaa kawaida.
"Rian tunaenda wapi?" Akauliza Aretha mara baada ya kutoka akiwa amevalia nguo ambazo Ed mwenyewe alimtolea kutoka kwenye kabati lake...
"Tunaenda mahali ambapo tutazungumza mipango yetu ya ndoa hahaha" Ed akamtania wakati akiweka nguo zake chache kwenye begi moja na Aretha ambaye naye alimwambia aandae nguo za siku mbili.
Walipomaliza wakatoka kuelekea kwenye mgahawa wa hoteli hii kwa ajili ya chakula cha mchana kabla ya kupanda basi la abiria ambalo liliwapeleka kwenye mojawapo ya milima nje kidogo na Sydney mjini. Milima ya Bluu (Blue Mountains).
Walipofika mwisho wa safari yao ya saa moja waliingia hoteli nyingine iliyojengwa pembezoni mwa mlima. Mahali ambapo walipokelewa vyema na wahudumu kisha baada ya kujaza taarifa zao, mhudumu mwingine akapewa kazi ya kuwapeleka hadi nyumba ambayo wangetumia kwa malazi.
Eneo lote la mlima kulikuwa na theluji iliyofunika, matawi ya miti yaliyoning'inia yalidondosha theluji huku paa za nyumba zikifunikwa pia.
Walitumia gari maalum kupita kwenye barafu hata walipofika kwenye nyumba hiyo ambayo nje iliionekana kuwa ndogo lakini mara walipoingia ndani mandhari yake ilimfanya Aretha kutoa macho ya mshangao kwani vitu vilivyokuwepo vilitosheleza vilipangiliwa vyema.
"Rian I really love this place" Aretha akamvuta mkono mara tu mhudumu alipomaliza kuweka mizigo yao na kuwapa maelekezo.
Nyumba ilikuwa na sebule ndogo lakini ilipangiliwa vyema kwa kuwekwa kochi mbili huku moja ikiwa karibu na sehemu ya moto na jingine lilitazama mahali runinga iliwekwa. Kulikuwa na zuria dogo lililowekwa kati na meza ndogo ya duara. Chumba cha kulala kilikuwa cha wastani chenye kitanda kikubwa kiasi, huku pembeni meza na kiti viliwekwa karibu na kabati la nguo. Dirisha lake lilitazama sehemu ambapo kulikuwa na mwonekano mzuri msitu ambao ulifunikwa na theluji..
Kulikuwa na sehemu ya jiko ambayo ukubwa wake ulikuwa sawa na nusu ya ukubwa wa sebule yake.
"Nafurahi kama umepapenda" akamjibu kisha akamketisha kwenye kochi lililokuwa karibu na tanuru ya moto ili kupata joto sababu hali ya hewa na kuanguka kwa theluji kulileta baridi katika upande huu wa kaskazini.
Aretha akatoa glovu ambazo alivaa mkononi kujikinga na baridi. Wakaketi pamoja khuku mikono yao ikiwa imeshikana kwa kupishana. Wakaamua kumpigia simu mama yake Aretha lakini eneo hilo lilionekana kuwa na usumbufu wa kimawasiliano.
"Njaa princess?" Ed akamuuliza huku akiinuka kuelekea jikoni
"Sina njaa sana, nadhani nilikuwa nahitaji maji" Aretha akamjibu huku akinyoosha mikono yake kuelekea kwenye moto.
Edrian hakuwa na shaka sababu aliwaandaa siku moja kabla kuweka vyote vilivyohitajika kwa chakula....
Edrian akaelekea jikoni na baada ya dakika tano alikuja akiwa amebeba vikombe 2 vilivyokuwa na maziwa akaviweka mezani. Kisha akarudi kuchukua sukari na kahawa kwenye sinia dogo. Akachanganya vyote kisha akamkabidhi Aretha naye alibaki na kimoja,
"Blue Mountains wanasifiwa kwa kuwa na kahawa nzuri sana. Karibu uijaribu" Ed akamwambia, naye Aretha akashukuru na kuinua
Akashukuru "Asante sana Rian, unajua naona kama niko ndotoni, natamani maisha haya yangekuwa yetu siku zote"
"Tukioana utapendelea wapi tuishi?"