Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 202 - MVINYO KIDOGO

Chapter 202 - MVINYO KIDOGO

"Retha kuna kitu amefanya?" Edrian akauliza

"Hapana Rian. Nimeuliza tu" Aretha akamwambia..

"Mbona umesema ni mkali, kwani amekukaripia?" Edrian akasisitiza ili Aretha amwambie ukweli

"Haa hapana, nadhani nimemuogopa tu kwa muonekano wake" Aretha akajaribu kuupunguza wasi wasi wa Edrian

"Haya kata simu wasije wakanisikia" akamuomba

"Hahaha unataka ukawasikilize mpenzi eeeh?" Ed akamtania

"Hapana Rian. Hebu kata mara moja" Aretha akamsihi.

"Utanipigia wakimaliza?" Akamuuliza

"Sawa Rian"

***************

Simu ya Allan ilimshtua Edrian ambaye alikuwa na furaha baada ya mama yake kumpigia na kumwambia ajiandae na safari ya wawili.

"Hello Allan" akapokea

Allan akamkumbusha juu ya chakula cha jioni na Renatha.

"Ooooh nilishasahau!, baada ya saa moja nitakuwa tayari. Nikukute hapo tayari." Akamjulisha kisha akachukua simu yake na kumpigia Aretha ambaye mara tu alipopokea mwitikio ule ule wa furaha ulikuwa upande wa pili.

Wakaongea kwa muda mfupi, akaingia bafuni kujiandaa kukutana na Allan, Golden Hotel kuonana na Renatha.

"Kwa ajili yako Allan, unasababisha nisiende kwa Retha wangu." Akawaza huku akielekea bafuni kuoga

Alipomaliza kuoga kwa takribani dakika kumi, alitumia muda uliobaki kujiweka nadhifu kwa mavazi yake safi. Akinitazama kwenye kioo

"Renatha" akashusha pumzi na kuchukua simu na funguo ya gari kisha akatoka..

**************

Aretha alipomaliza kuzungumza na Edrian, akaketi kwenye kitanda chake akitafakari kwa nini alishindwa kumwambia ukweli kuhusu BM na ofa aliyompatia. Kila alipojaribu kufungua kinywa chake kusema, alihisi hofu ya kutotaka kumkwaza Ed wakati alikuwa mwenye furaha baada ya kupewa taarifa ya safari yao. Akaadhimu kumwambia mara tu watakapokuwa safari.

Akajiandaa baada ya BM kumpigia simu kumuuliza kama bado anataka kuifanyia kazi ofa ile. Akampa taarifa mama yake kuhusu ofa lakini hakumtaja BM

"Retha huwezi kwenda huko peke yako, kwa nini hujamshirikisha Derrick. Unamwaminije mtu haraka hivyo wakati umesema haumfahamu?" Mama akamuuliza

Aretha akachukua simu yake na kumpigia Derrick lakini simu haikupokelewa.

"Mwanangu mwambie Edrian" mama akashauri, lakini Aretha akamkatalia

"Mama mwache apumzike maana aliingia alfajiri na hajapata hata muda wa kupumzika"

"Basi ongozana na Frans, atakuwa amesharudi. Frans!!!" Akamuita

"Mama nitachelewa na muda umeshaenda, huyu Frans hadi ajiandae atafanya tuondoke giza limeshaingia. Ananionesha hizo picha narudi" Aretha akamshawishi mama yake ambaye kwa shingo upande alimruhusu

Aretha akaondoka huku akitumia usafiri wa gari ya kukodi kuelekea mahali ambapo BM alimwambia atakuwepo akimsubiri.

***********

Edrian alipofika kwenye maegesho ya Golden Hotel alifuata maelekezo ya Allan ambaye alimsubiri ghorofa ya nne ambapo ndio kulikuwa na mgahawa mkubwa wa hoteli hii.

"Bro asante" Allan akamwambia mara tu alipokaribia kwenye mlango wa kuingilia

Edrian akatabasamu kisha wakaingia ndani wakaelekea mpaka mahali ambapo walimuona Renatha ameketi. Renatha alipomuona Edrian akifuatana na Allan, sura yake ilibadilika lakini akarudisha tabasamu. Akasimama na kuwasalimia kwa pamoja huku akishika na kubana kiganja cha Allan.

"Renatha nina shauku ya kujua nini maana ya wito huu. Lakini ngoja tupate mvinyo kidogo kabla hatujaendelea" Akasema Edrian wakati akiketi wakati mhudumu akiwasogelea ili kutoka huduma.

Baada ya kupokea oda zao, mhudumu aliwaacha. Allan alitabasamu wakati akimwangalia Renatha kumuonesha kuwa alifanya kama ambavyo walikubaliana.

Renatha alivalia gauni nyeusi fupi iliyokuwa na ufito wenye mng'ao wa dhahabu tumboni kisha ukashuka upande wa kushoto. Nywele zake zilifungwa vyema na kwa nyuma na kutengenezewa mawimbi huku nywele chache za mbele zikining'inia pande zote mbili. Alipendeza sana.

Kimya kilitawala kwa muda kati yao kila mmoja akiangalia simu yake hadi mhudumu alipokuja na vinywaji. Baada ya kuhakikisha kila glasi ina kinywaji, akatoka.

Edrian akamwangalia Renatha kisha akainua glasi yake iliyokuwa na mvinyo akanywa.

Allan akatoka kidogo baada ya kuona Renatha kama aliyeshikwa na kigugumizi