Edrian alimwangalia Aretha ambaye alimezwa haswa na maelezo ya Yassin kuhusu onesho watakalomuandalia Beruya, alijisikia furaha kuona namna alivyotoa mawazo yake huku akiandika yale aliyoona muhimu.
"Kuhusu zile picha tayari BM ame_" kabla ya kumalizia Yassin akaangalia mkono wa Derrick uliomfinya pembeni kumzuia asiendelee na kile alichokuwa akizungumza
Aretha aliona hili na akabaki akitarajia Yassin ataendelea, lakini kwa mkono ule uliomfinya alibaki akimwangalia Derrick
"Aaaah picha zote zimeshachukulia na pesa imeingia kwenye akaunti ya Beruya wakati yako Aretha nimepewa hundi tayari"
Edrian akamwangalia Derrick aliyeongea kwa tahadhari huku macho yake yakihama kutoka kwake kwenda kwa Aretha, "Its okay Derrick" akamwambia huku akimwangalia Aretha ambaye hakujua nini chanzo cha kusita sita kwa Yassin.
Derrick akamuangalia kaka yake akishangaa kama ilikuwa sawa kumuongelea BM ikiwa jana yake alionesha wazi kutokubaliana nae. Akatoa ile hundi na kumkabidhi Aretha ambaye aliingalia na kisha akaweka kwenye mkoba.
Mazungumzo yaliendelea kati yao, mipango kuwekwa tayari. Walipomaliza, Edrian akamuuliza Yassin kuhusu jumbe ambazo Beruya alimtumia Aretha
"Ninachohofia ni kuwa kama Beruya ndiye aliyetuma ujumbe wa kumlaumu Aretha basi itabidi mtafute kuwapatanisha kwanza kabla ya kufanya chochote"
Yassin akashangaa kusikia taarifa ile na mara alipooneshwa meseji zile akashtuka, "B sidhani hata kidogo kama anaweza kuandika haya maneno, kwa sababu alipozinduka alikuwa akimuwazia Aretha namna anavyojisikia, haiwezekani!"
"Kwa hiyo itakuwa mtu mwingine ametumia simu ya Beruya kutuma ujumbe! Na huyo mtu atakuwa karibu naye" Derrick akatoa mawazo yake
"Nafikiri Yassin ungetusaidia kuchunguza, inawezekana mtu huyo akawa msaada kwetu kujua kinachoendelea" Edrian akaongea
"Sawa, nitafanya hivyo, ila mtu pekee aliyekuwepo na Beruya muda mwingi ni yule mchumba wake ambaye ni daktari"
Walipomaliza wakaagana, giza lilianza kutanda muda walipoingia kwenye gari. Edrian akamwangalia Aretha kisha akamwambia
"Hongera Retha, umekuwa mfanyabiashara kufumba na kufumbua"
Aretha akacheka kicheko chepesi, "Asante ni kwako ambaye umenifanya niwe hivi"
"Mimi aaah?" Akauliza kwa mshangao Ed
"Ndio wewe"
"How?" akauliza Ed huku akielekeza macho yake barabarani
"Aaaàaaah nafikiri kuna kitu ulinipa" Aretha akajibu huku akiangalia nje kwa aibu
"Nilikupa nini?" Akauliza akimtania
"Sijui" Aretha akajibu akiendelea kuyakaza macho yake kuangalia nje
"Retha" Ed akamuita huku akitafakari kile alitaka kumwambia
"Aaaahm" akaitika Aretha
"Unaweza kusafiri nami?" Ed akauliza akimtupia macho kwa haraka kisha akayauliza
"Aaah kusafiri?" Aretha akashtuka na akageuka kumtazama Ed
"Ndio, kusafiri pamoja nami.." akaongeza Ed
"Ahmmm...sijui Rian labda nimshirikishe mama" akajibu Aretha
"Sawa, naweza kusafiri hivi karibuni nitatamani kusafiri nawe. Una hati ya kusafiria?." Edrian akauliza
Aretha akashtuka "kusafiri nje ya nchi?" Akauliza
"Ndio Retha, kuna mahali natamani twende pamoja." Edrian akaangalia upande wake halafu akaendelea "lakini tutaangalia ratiba yako chuoni"
Aretha akabaki kimya akitafakari huku vidole vyake akivifinya
"Heeeee princess mbona umebaki kimya? Unaogopa kusafiri nami?" Ed akauliza
"Aaah mimi?" Akashtuka na kuuliza
"Retha, unaniogopa wakati tuko wote jamani"
"Hapana Rian sikuogopi" Aretha akajitetea
Ghafla gari ikapunguza mwendo na ikasimama pembeni ya barabara, Aretha akashtuka akamwangalia Ed.
Ed akapandisha vioo vya gari, mwanga hafifu ulipenya ndani ukitokea nje kwenye taa za barabarani. Akageuka na kumtazama Aretha huku akitabasamu
"Rian kuna shida yoyote, mbon_" Ed akamkatisha kwa kumwekea kidole mdomoni "ssshhhh"
Akainama na macho yao yakakutana "umesema huniogopi, kama kweli hauniogopi nataka unibusu mwenyewe" Ed akamuangalia akatabasamu
Aretha akajaribu kukaa vizuri, akimuangalia usoni Ed, "Rian aa...na_"
"Eshshhhs... Retha kiss please" Ed akamwambia kisha akafumba macho kumsubiri Aretha akamwangalia Ed asiamini kama ni yeye aliyeamua kuegesha gari pembeni ili apewe busu.