Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 164 - UKANIJIBU UTAWEZA

Chapter 164 - UKANIJIBU UTAWEZA

"Okay bro sitauliza. Ila nitamkabili Aretha mwenyewe aniambie kama amekuzuia usiingie ndani"

"Li! Usijaribu kumwambia chochote nakuomba" Ed akamwambia akimtazama usoni, lakini Li aliachia tabasamu na kuangalia mbele kwenye mlango..

"Sitamuuliza bro" akajibu taratibu, lakini kabla Ed hajasherehekea jibu lile Li akaongeza

"Ikiwa utaniambia nini kinaendelea. Nje ya hapo siwezi kuahidi chochote"

Edrian akainua mkono wake kisha akambinya kidogo Li begani akamwambia

"Asante mdogo wangu, najua unanijali, hata mimi sijui ukweli wa nini kinamsumbua Retha" akameza mate kisha akaendelea

"Ila nahisi tu kutokana na mazungumzo yangu na Dokta Brianna, Retha atakuwa na 'stress' ya matukio ambayo hajayazoea kwenye maisha yake." Akanyamaza kumruhusu Li kuelewa kile alichokizungumza.

Baada ya kimya cha sekunde chache Li akageuka na kumwangalia kaka yake kisha akamshika kaka yake begani na kumwambia,

"Sitamuuliza ila kuna kitu nataka niongee naye. Ni cha msingi, hivyo usinizuie bro" Li akamwambia kaka yake kwa msimamo thabiti.

"Sawa Li, najua unanijali. Nashukuru sana" akamaliza kumwambia na wakaendelea kuzungumza zile picha alizotumiwa na Captain.

**********

Baada ya mama na Frans kuingia, Aretha alikuwa amefumba macho, sio kwamba alikuwa amelala, la hasha bali aliogopa iwapo Ed angemkuta macho. Macho yake yalijaa machozi kila alipomuona Ed. Akiwa amefumba macho alisikia mlango ukifunguliwa lakini akasikia mama yake akijiuliza Ed kwa nini hakuingia ndani. Jibu la Edrian lilimfanya walau atabasamu,

"Afadhali Rian hakumwambia" akawaza

Mara aliposikia mlango umefungwa, akafungua macho taratibu na yakakutana na yale ya mama yake,

"Unaendeleaje Retha?" Mama akamuuliza huku akiketi kwenye kiti kilichokuwa pembeni ya kitanda...

"Naendelea vyema, nisamehe siku__" sauti ya Aretha ilikuwa na mkwaruzo sababu ya kulia muda mrefu.

"Usijali, binti yangu nimekuelewa" mama akamkatisha kisha akampa ishara Frans kuongea na dada yake.

Baada ya ndugu hawa kusalimiana, mama akamtoa Frans mle chumbani akamwambia amsubiri nje. Frans akaondoka na kuelekea nje.

"Retha, umemfanya nini kijana wa watu?" Mama akamuuliza mara tu Frans alipofunga mlango

Aretha ambaye hakujua kama mama yake alikuwa akimuwazia Edrian,

"Mama hamna kitu" Aretha akajaribu kuficha uso wake kumwangalia mama yake usoni

"Retha, yeye ndie anaonekana kuwa na hali si njema, unamlaumu eeeh?" Mama akauliza

"Hapana mama, na__"

Mama akamkatisha Aretha na kumwambia, "naomba uache Retha, unakumbuka nilikuuliza utaweza kupambana! Ukanijibu utaweza, sasa nakuomba usimuongezee uchungu kwenye maisha yake unanielewa Retha" mama akamwambia taratibu huku akitazama uso wa mwanae ulioonesha kukosa mng'ao sababu ya kulia..

"Mama, kama aliyefanya hivi ni Lyn, nitakuwaje na uhakika hataumiza mtu mwingine?" akameza mate taratibu kisha akaendelea

"Kumuona Rian kunaniumiza pia sababu maisha yanakosa raha kila nikiwaza nitayavumilia mangapi mama eeee! Machozi yakaanza kushuka kama bomba kwenye uso wa Aretha..

Mama akasogea na kujaribu kumuinua kwa tahadhari na kumkumbatia pasipo kutingisha mpira uliopitisha maji aliyowekewa na Dokta kumuongezea nguvu.

Aretha akalia mikononi mwa mama yake hadi alipoona hana tena machozi yaliyobaki. Na kwa sababu ya kulia akapitiwa taratibu na usingizi. Mama akamuacha alale pale pale mikoni mwake.

************

"Hellow boss" sauti nzito ilisikika nje hospitali hii ya City kwenye mojawapo ya magari yaliyoegeshwa kwenye eneo la maegesho.

"Boss mpango umefanikiwa, ila kuna dharura na wapo hosoitalii"

Sauti ya upande wa pili haikusikika vyema lakini aliyekuwa akitoa ripoti alielewana na bosi wake.

"Sawa, nimekuelewa. Narudi" alipomaliza akakata simu.

Akatabasamu, "Am sorry Aretha unaumia sababu ya mtu mwingine"

Akawasha gari na kuondoka.

*************

Usiku ulienda sana lakini Ed hakuondoka pale hospitali hata baada ya Li kumshawishi kuwa Aretha yuko salama na amelala pamoja na mama yake, lakini haikuwezekana.

Aliingia kwenye chumba alicholazwa Aretha kule kumuona amepumzika moyo wake ukatulia. Hakujua mama hakuwa amelala, alisikia hatua zake