Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 162 - CHUMBA CHA DHARURA

Chapter 162 - CHUMBA CHA DHARURA

Frans alipokata simu akamrudishia mama yake, ambaye alimuangalia usoni na kisha akamuuliza taratibu, "nini kinaendelea?"

"Mama hakuna kinachoendelea, ila kuna kitu nilitaka dada akwambie mwenyewe lakini naona amepata dharura na wamerudi na Edrian hospitali" sauti tulivu ya Frans ilimfanya mama yake aamini kile alichomwambia lakini akashtuka aliposikia hospitali

"Nani yuko hospitali" akauliza kwa wasiwasi

Frans akakohoa kulainisha koo kisha akamwelezea yote yaliyotokea kama Ed alivyomwelekeza. Akajitahidi kumwambia taratibu akiangalia upokeaji wake wa taarifa. Mpaka alipomaliza kumwambia kilichotokea, hakukuwa na mabadiliko yoyote kwenye hali ya mama yake.

"Frans, kuna kitu hauniambii eeeh?" Akauliza mama

"Kitu gani tena mama" Frans akauliza akijifanya kushangaa!

"Hospitali wameenda kufanya nini?" Akauliza mama huku akiinua jicho kumtazama kijana wake..kisha akaongeza swali kabla ya Frans kujibu!

"Umesema kuwa mlienda kumuona Beruya kabla ya kuja hapa, kwa nini wanarudi tena huko?"

Frans akasita kidogo kumjibu mama yake, ilikuwa vigumu sana kwake kujaribu kuficha kinachoendelea..

"Mama kwani kuna shida kama wakirudi huko? Labda wameambiwa hali imebadilika ghafla na__"

"Frans" mama akamkatisha

"Niambie, Edrian amekwambia nini ambacho hataki mimi nijue?" mama akaendelea huku akiinuka na kusimama sambamba na kijana wake

Frans akapiga hatua moja nyuma akamuangalia mama yake, akashusha pumzi "Mama unajua tukio la leo limemhuzunisha dada Retha na__"

Simu ya mama ikaita, ikamkatisha Frans aliyekuwa karibu na kumwambia ukweli mama yake, akashukuru mlio wa simu uligeuza macho ya mama yake yaliyomwangalia kuelekea kwenye kioo cha simu.

Akapokea, "Hello mwanangu" mama akaitika kwa haraka baada ya kuona aliyempigia

"Mama naomba ujiandae kuna mdogo wangu nimemuagiza anakuja kukuchukua na Frans dakika chache zijazo" Edrian akaongea kwa sauti ya utulivu japokuwa kulikuwa na dalili za huzuni ndani yake

"Anatuchukua kutupeleka wapi mwanangu, ni usiku sasa" akauliza mama

"Mama yangu najua una maswali mengi ila naomba uniamini, ni Retha mwenyewe ameomba mje" akamsihi

Sauti ya Ed ilikuwa tulivu kiasi cha kumfanya mama aamue kukubaliana na Ed kuwa atakwenda.

"Mwanangu kama kuna jambo unanificha naomba utambue sipendi kushtuliwa"

Edrian akashusha pumzi kwa uzito hata kumfanya mama ahisi vibaya

"Mama kama jambo sijakwambia nitakuwa na sababu njema tu lakini ukija huku itakuwa rahisi kukuelewesha"

"Haya nitakuja"

****************

Baada ya kumfikisha Aretha kwenye chumba cha dharura kwa ajili ya kupatiwa huduma ya haraka, Edrian hakuondoka mle ndani. Kwa kuwa Dr Ivan na Dr Brianna ni watu aliowafahamu walimpa kiti akae pembeni wakati wakishughulika na matibabu ya awali.

Pamoja na kupewa kiti Ed hakuweza kukaa, aliinuka mara kwa mara na kuzunguka. Akakumbuka alichomwambia Dokta Brianna "Tafadhali fanya unachoweza kumsaidia, siwezi kumpoteza ninayempenda?"

Dokta Brianna na dokta Ivan ni madaktari viongozi kwenye hospitali hii ya City. Ni mara chache sana ungewakuta Chumba cha dharura wakihudumia wagonjwa. Walihusika hasa na upasuaji, lakini leo rafiki na mshirika wa hospitali hii aliwaleta kwenye chumba cha dharura.

"Ed come down, she is okay. Ni mshtuko tu. Ameshaamka" Dr Ivan akamfuata na kumwambia Ed huku akimshika begani na kuondoka naye

Walipovuta pazia, Ed akamuona Aretha aliyelala kitandani huku mkono ukiwa umechomekwa sindano ilipitisha maji kutoka kwenye dripu iliyotundikwa kwenye chuma.

Dokta Brianna akamwambia Aretha, "una mgeni anataka kukuona", uso wa Aretha ukabadilika alipomuona Ed machozi yakaonekana pembeni ya macho yake kisha akasema kwa sauti ya chini

"Niitie mama yangu"

Dokta Brianna aliposikia akatabasamu na kukubali huku akitikisa kichwa. Akainuka na kumwambia Ed watoke kidogo. Akamfuta hadi pembeni

"Anataka kumuona Mama yake, wajulishe waje. Utamuona baadae, mpe myda. Lakini nitahitaji kufahamu nini kilitokea maana ana uchungu moyoni"

Edrian aliposikia akashusha pumzi kwa nguvu, "Sawa Brianna". Akatoa simu yake na kumpigia Linus mdogo wake ili amfuate mama.