"Rian, mliongea nini na mama?" Aretha akauliza huku akivuta mikono yake kwenye mifuko ya sweta alilokuwa amevaa,
"Nothing much, alitaka kujua kama nitakurudisha leo au ukalale kwangu" Edrian akamtania
"Rian" Aretha akashtuka aliposikia maneno yale akageukia dirishani
"Kuna shida kwani princess?, kwangu kuna vyumba vya wageni, utakuwa mgen_"
"Rian please" Aretha ambaye sasa alijaa aibu, hakutaka kugeuka kumwangalia Ed
Edrian akaguna huku tabasamu likiendelea kuwepo usoni kwake!
"Oookay princess, wewe unadhani mimi naweza kuongea nini na mama eeeh?" Akauliza kwa utani
"Aaaahm...sijui lakini alisisitiza sana nikadhani kuna kitu mmeongea nae" Aretha akajitetea akijaribu kutokuonesha wasi wasi. Maongezi yake na mama siku chache zilizopita bado yalimuweka njia panda, akihisi huenda mama yake alimwambia Edrian maadui ambao anawafahamu.
"Kawaida tu princess, mama mwenye mapenzi na mwanae hataacha kumlinda, na yeyote yule aliye karibu na binti yake atapata maonyo ya kumlinda kila siku" Edrian akamwambia huku akiachia tabasamu
"Aaaaah basi sawa" Aretha akaridhika
Wakaendelea na safari hadi walipofika Southern Pole, usiku ulikuwa umeenda japokuwa mwanga wa taa ulifanya barabara na baadhi ya mitaa kuonekana kana kwamba bado ulikuwa mchana.
Kabla ya kushuka kuingia ndani, Edrian akamwambia Aretha ampigie Beruya kujua kama ameshawasili. Beruya akawajulisha kuwa alikuwepo na akawakaribisha, nao wakashuka na kuelekea kwenye mlango wa kuingia ndani. Edrian akabeba picha mkononi huku akimkatalia kabisa Aretha kubeba zile picha
Mara Edrian alipowakaribia wale walinzi wakamsalimia kwa heshima, akajua wamemfahamu. Usiku huu hakukuwa na watu waliokaa pale kwenye ukumbi wa mapokezi. Wakaelekea kwenye lifti kuelekea kwenye ukumbi ambao onesho litafanyika. Hata huku bado hakukuwa na mtu hata mmoja. Ndani ya lifti Edrian akasema mzigo ule wa picha pembeni. Akabaki akimuangalia Aretha ambaye alisimama karibu na yeye, moyoni akatamani amvute karibu zaidi nae. Zile nguo aliyovaa zilimfanya avutie zaidi.
"Nini kinanivutia wakati mtu kavaa sweta aaah" akajiuliza Ed huku kicheko chepesi kikimtoka na kumfanya Aretha amwangalie...
Mlango wa lifti ukafunguka Aretha akawa wa kwanza kupiga hatua kutoka lakini kabla yakufanya hivyo, Ed akauwahi mkono wake na kumrudisha kwenye lifti na akabonyeza kitufe cha kufunga mlango.
Aretha akashtuka na kumwangalia Edrian akisubiri amwambie kwa nini alifanya hivyo...
"I want to kiss you" Edrian akamwambia Aretha huku macho yake yakimwangalia pasipo kupepesa
Mabega ya Aretha yakashuka kutoka kwenye hamaki ya kuvutwa ghafla, akainama kwa aibu kisha akainua uso wake na kumwangalia Edrian, ambaye alitambua amepewa ruhusa. Akainama taratibu na midomo yake ikakutana na ile laini ya Aretha akambusu lakini alipotaka kuendelea zaidi akasikia sauti ikimuita, akaacha na kuinuka
"Rian tuko kwenye lifti" Aretha akasema taratibu huku akiinua macho kumwangalia usoni japo hakuendelea akayakwepesha pembeni..
"Aaah okay" akabonyeza kitufe cha kufungua mlango
"Nitaendelea nilipoishia tukitoka" Edrian akasema kwa sauti ya chini huku akichukua mzigo ule wa picha. Aretha akaitika kutaka kujua nini amesema lakini Edrian akatabasamu, wakatoka na mara walipopiga hatua sauti ya Beruya ikasikika nyuma yao
"Aretha karibuni" akawakaribisha huku akiweka vyema mzigo mdogo wa picha uliokuwa mkononi mwake..
"Naomba nikusaidie " Aretha akamwambia huku akipiga hatua kurudi nyuma
"Habari Edrian" Beruya akamsalimia huku akimpa mzigo kiasi Aretha amsaidie.
"Salama Beruya" Edrian akamuitikia.
Wakaelekea ndani ya ukumbi ili kuanza zoezi zima la uwekaji wa picha. Beruya alimuangalia Edrian aliyetembea bila wasi wasi akiwa amebeba picha za Aretha..
"Kama Edrian mwenyewe amemchagua na anamfurahia mimi siwezi kufanya chochote kuwatenganisha, ona alivyo na furaha" Beruya akawaza..
Walipofika kwenye meza kubwa iliyokuwa pale ukumbini wakaweka picha pale
Mle ukumbini kulikuwa na watu wachache sana ambao waliendelea na uwekaji wa picha huku mmoja alikuwa akimaliza kuweka mapambo sehemu ya jukwaa dogo.
Ukumbi ulivutia sana.