Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 126 - SHEM DERRICK

Chapter 126 - SHEM DERRICK

Mkutano kati ya Aretha na wachoraji hawa mahiri uliendelea vizuri ikionesha wazi kabisa waliikubali kazi yake. Mara kwa mara Ed aliuliza maswali muhimu ya namna ya kutengeneza kipato kutokana na picha. Moja ya mambo ya msingi ambayo waligundua kuhusu uchoraji wa Aretha ni uwezo wa kuficha jambo katika picha. Ilichukua muda kwa Ed na Derrick kuona picha ya kipepeo aliyekuwa katikati ya picha yote ya mawio ya jua.

Baada ya mazungumzo yao kukamilika walikubaliana kuwa Aretha atapeleka baadhi ya picha zake kwenye onesho la Beruya ambalo lingefanyika wiki moja mbele. Aretha alishukuru sana kwa kuweza kupata nafasi hiyo. Kwa muda mchache alikaa na wachoraji hawa alimzoea sana Beruya, mara zote ndie alimtia moyo kujiamini, hakuishia hapo alikubali kumfunza kwa karibu huku akimkaribisha kwenye maandalizi yote.

Edrian aliwashukuru sana na akaahidi kuzungumza na Idara ya Habari Mawasiliano ya SGC kuona kama wanaweza kuwa na udhamini katika onesho la Beruya. Wakaagana wakiwaacha wachoraji wale wakitumia usafiri wao binafsi.

"Umeona ilivyokuwa rahisi Retha!" Derrick alimwambia Aretha wakati huu alikaa nyuma na Aretha alikuwa pembeni ya Edrian aliyekuwa akiendesha

"Aaaah wewe ndio unaona rahisi lakini kwangu hapana" alijibu Aretha

"Hahaha wakati wewe ndio umeongea kwa sehemu kubwa!" Derrick akaendelea kumtania

Aretha akageuza shingo na kumwangalia Edrian ambaye alikuwa kimya akiendesha

"Rian ndie aliyeongea kwa sehemu kubwa..Asante" akaongea kwa sauti yake ya upole akimshukuru Edrian. Ni kweli kabisa sehemu kubwa ya mazungumzo ilibebwa na Edrian ambaye aliuliza maswali ya muhimu. Kutokea hapo Aretha alipata ujasiri wa kujieleza na yale yote aliyahofia juu ya picha anazochora.

"Umefanya vizuri Retha" Edrian alijibu huku macho yake yakiendelea kubaki barabarani..

Derrick akakohoa kidogo kumrudisha Aretha ambaye macho yake yaliganda usoni kwa Edrian. Aretha akashtuka huku akiinama kwa aibu

Akili ya Edrian ilikuwa imezama katika kutafakari mambo ya msingi ambayo Aretha alitakiwa kuwa nayo kabla ya onesho la pamoja na Beruya.

"Derrick unaweza kuwa Meneja wake kwa muda kabla ya kupata Meneja rasmi eeh?" Aliuliza Edrian

"Bro unaniomba tena eeeh?" Derrick akauliza kwa mshangao

"Ndio nakuomba, una majukumu yako siwezi kuyaingilia ndio maana nakuomba!"

"Retha unakubali niwe Meneja wako? Derrick akamuuliza

Aretha ambaye hakutegemea kuulizwa hilo swali akashtuka "aaahm"

Macho ya Derrick na Edrian yakamwangalia kwa pamoja yakionesha shauku ya kujua maoni yake.

"Sawa tu Derrick. Nakubaliana na Rian"

Edrian akaachia tabasamu wakati huo macho yake yakarudi barabarani.

"Retha, kuanzia sasa mimi ni Meneja wako, hauruhusiwi kugawa picha bila ruhusa yangu sawa eeeh!"

"Aaaah" wakashtuka kwa pamoja huku Aretha akigeuza shingo na kumwangalia Derrick

"Ndio hivyo, ukimgawia mtu picha na kumbe ingeweza kutuingizia pesa ndefu, tutakuwa tumepoteza" Derrick akajifanya kumaanisha kile alichokizungumza.

Wakati huo Edrian alimuangalia Derrick kwa kutumia kioo kile cha ndani huku akitabasamu kwa utani ule,

"Kwani kuna mtu alimgawia picha?" Edrian akauliza macho yakimtazama Derrick..

"Retha ulimgawia nani picha eeeh" Derrick akalirudisha swali kwa Aretha

"Mmmmh" Aretha akaguna na kumwangalia Edrian

"Umeona umemgawia picha m_" kabla Derrick kuendelea Aretha akamuwahi

"Hata wewe nilikugawia halafu ukaibadilisha na ukachukua nyingine"

"Mimi ni Meneja wako naruhus___? Edrian akaingilia

"Meneja ukipewa bila kununua unatupa hasara. Lipia kwanza ile uliyochukua halafu masharti yako yatafuatwa. Au sio Retha?

"Aaaeehm ni sawa, ila picha nikiamua kumpatia mtu si vibaya Derrick?"

Derrick aliyekuwa anamuangalia Aretha akamuonesha kwa midomo yake "Shem Derrick"

"Eeeehm" Aretha akashangaa huku akiinama kosa ambalo lilimfanya Ed wangalia alipo Derrick akishangaa Derrick alijaribu kuongea nini na Aretha.

"Hamna kitu bro, ameshtuka kuona Meneja wake nimekubali anaweza kukupatia picha" Derrick akajificha alipoona macho makali yakimwangalia

"Aaahm" Aretha akazidi kushangaa kwa jinsi Derrick alivyohamisha mada...

Derrick akamkonyeza