Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 121 - NIKO NAWE

Chapter 121 - NIKO NAWE

Alfajiri ya siku iliyofuata Edrian aliamshwa na mlio wa simu yake ikiwa ni mapema, alipoangalia ilikuwa ni namba ya Lyn kwenye kioo.

Hakupokea, akaamua kuinuka kitandani na kuelekea kwenye ofisi yake, ambapo alifungua kompyuta yake na kuanza kuangalia barua pepe kwenye akaunti yake ya Google.

Akasoma taarifa chache ambazo zilitumwa kutoka kwa wasimamizi wa migodi ya SGC. Ilipofika muda wa kufanya mazoezi akainuka na kuelekea kwenye chumba cha mazoezi. Bado Lyn aliendelea kupiga hata kumkera Ed ambaye aliamua kuizima simu na kuendelea na mazoezi. Akajuta kwa nini alimpa Lyn namba yake binafsi anayoitumia kuwasiliana na watu wake karibu

Baada ya kujiandaa vyema akatoka na kuelekea. Alipoingia kwenye gari akawasha simu na kisha akaenda moja kwa moja kwenye kuzuia simu zote za Lyn. Alipomaliza akampigia Aretha, na wakati huo akawasha gari na kutoka. Akiwa njiani simu ikaendelea kuita kwa muda hatimaye ikapokelewa na sauti ya mtu aliyekuwa usingizini

"Hello Rian" Ed alisikia sauti yenye mkwaruzo ikitoka kwa Aretha

"Retha, bado umelala princess?" Akauliza kwa upole

"Hapana, niko macho Rian" Aretha akajitahidi kusikika kama alikuwa macho lakini hakuweza sababu bado sauti ilitoa mikwaruzo kwa kutoongea muda mrefu!

"Okay, amka basi princess, ulichelewa kulala?" Ed akauliza

"Aaahm"

"Retha umechelewa kulala, ulikuwa unafanya nini?" Maswali yakaendelea

"Aaah. .aah___" akapata na kigugumizi

"Ulikuwa unachora Retha" Ed akamkamatia kwenye ukweli

"Rian_" Ed akamkatisha

"Ni sawa princess, lakini kumbuka kulala mapema bado mwili wako unahitaji mapumziko".

"Sawa nimekusikia"

"Asante kwa picha nzuri Retha, umeweka kumbukumbu kubwa kwangu"

"Aah sawa Rian"

"Najua ni zawadi, nataka niinunue kwa kuwa in___"

"NO...no Rian, usiseme hivyo, naomba uchukue ni zawadi yangu kwako kwa kunipenda" Aretha alisema taratibu huku sauti yake ikiishiria aliposema neno hilo la mwisho

"Eeeehm, wewe ndio unastahili zawadi princess kunikubali na kunipokea"

"Rian, nimekupa hiyo picha, hesabu nimekupa moyo wangu, huwezi kuununua, si ndio hivyo eeeh?"

Ed akashusha pumzi, "sawa princess. Nashukuru sana."

"Asante kuelewa"

"Princess" akaita Ed

"Aahmm" akaitika Aretha

"Sitaki kuendelea na ule mpango wa mama, nimechoka" Ed aliongea na kudhihirisha uchovu wote alikuwa nao

"Kumetokea nini Rian" akauliza Aretha ambaye ilikuwa wazi alishtushwa na kile Ed alimwambia

"Retha, siwezi kujizuia ikiwa Lyn ataendelea kuingilia maisha yangu. Nitaingia kwenye shida ikiwa nitamuumiza"

"Kwa nini umuumize Rian, kumbuka kutoruhusu mambo ya__"

"No Retha, siwezi. Siwezi kuwa mbali nawe" Ed akamkatisha Aretha kwa msisitizo katika sauti yake

"Uhmmm" Aretha akaguna

"Sheesh siwezi Retha.. anaingilia uhuru wangu sana. Nimeona nikwambie ili atakachofanya chochote kuanzia sasa jiandae kisaikolojia. Najua nakupa mzigo mkubwa princess, ila naamini ni maamuzi sahihi kwangu"

"Na huwazi taswira yako itakuwaje?" Nikikisa na mashaka ya wazi kwenye sauti ya Aretha

"Retha, acha wafikirie wanachotaka kufikiri. Najua baada ya muda ukweli utajulikana" Ed alijibu kwa uthabiti kabisa.

"Na mama umemwambia?" Akauliza Aretha

"Nikifika ofisini nitaongea nae, nimeona nikwambie lakini kama nilivyosema jana, uwe mwangalifu. Naamini uko smart katika hili, Joselyn ni msumbufu atajaribu kukuingia akutishe lakini nakuomba mpuuzie"

Aretha akanyamaza kwa muda, kimya kikatawala kati yao kwa sekunde kadhaa

"Retha" Edrian akaita

"Rian, uwe mwangalifu pia. Taswira yako ni taswira ya kampuni pia. Mimi naweza vumi_"

"NO, hayo ndio maamuzi yangu Retha. Nitashughulika na taswira yangu na ya kampuni nikijua sihitaji kukuficha au kuigiza. I can't Retha" kwa haraka Edrian alimkatisha Aretha.

"Ooooh sawa, niko nawe Rian" Aretha akajibu, japokuwa aliyaogopa maamuzi hayo lakini alijitia moyo na kumkubalia Ed

"Asante Retha. I love you princess" maneno ya furaha yakamtoka Edrian

Walipomaliza kuongea Edrian alikuwa tayari kafika Ashante Tower kwenye maegesho maalum. Akaachia tabasamu na kuchukua vitu alivyokuwa navyo kwenye gari, akashuka tayari kuelekea ofisini.