Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 91 - USIOMBE MSAMAHA

Chapter 91 - USIOMBE MSAMAHA

"Renee, hakikisha napata taarifa za ndani kuhusu SGC, nje ya hapo makubaliano yetu yatavunjwa na sitakwambia wapi mama yako yupo" Sauti ya mwanaume ambaye sura yake haikuonekana wazi ilisika na kwa kuwa giza lilifunika karibu nusu ya chumba hiki usingeweza mtambua, lakini sauti yake ilibeba harufu ya mtu mwenye madaraka makubwa.

Renatha aliyekuwa amekaa kwenye kochi mkononi akiwa na glasi yenye mvinyo aliuangalia kabla ya kuutikisa kidogo kabla ya kuunywa wote.

"I will do it daddy. Jumatatu ninaanza kazi kama barua waliyonitumia inavyonielekeza. Naomba nikimaliza kazi hii utimize ahadi yako la sivyo nitaondoka" Akamjibu mtu huyu halafu akainuka na kuondoka.

Ndani ya chumba kile akaingia mwanaume mwingine aliyevaa vazi la kiofisi, mtanashati na mwenye kutembea kwa madaha.

"Bon hakikisha unamfuatilia. Simuamini sana. Nimemuona anaangalia faili la Simunge uso wake ni kama umekuwa tofauti na binti yangu ninayemjua."

Aliongea mwanaume yule ambaye aliuficha uso wake usionekane

"Yes TM" akajibu yule mwanaume aliyeitwa kwa jina la Bon kisha akageuka na kuondoka.

****************************

Safari ya Edrian na Aretha iliishia Ashanti Tower, mahali zilipo ofisi za Simunge Mining!

Aretha alimuangalia Ed kwa mshangao baada ya kushuka, lakini kabla ya kusema chochote, Edrian akamshika mkono na wakaelekea kwenye lifti maalumu iliyowapeleka mpaka juu kabisa ya jengo hili lililobeba ghorofa 15

Baada ya kushuka kwenye lifti, Ed akapitisha mkono wake mabegani kwa Aretha na wakatembea kuelekea kwenye kibaraza kilichowekewa turuba juu na ndani yake paliwekwa viti viwili, meza na pembeni kuliwekwa meza nyingine ndogo iliyobeba kontena ndogo ambalo lilionesha kubeba vinywaji.

Edrian akavuta kiti akamkaribisha Aretha aweze kukaa. Kisha nae akarudi kuketi. Ilikuwa ni mida ya machweo ya jua. Kulikuwa na rangi ya dhahabu iliyonakshi mandhari ya eneo lote. Palivutia sana. Uso wa Aretha ulijaa furaha alipoona mandhari ile..

"Umepapenda Retha?" Ed akamuuliza

"Ooooh Rian, ulijuaje napenda sana machweo ya jua! Thank you" akasema Aretha huku mikono yake akiiweka kifuani.

"Nashukuru umefurahi, wakati wowote unaweza kuja kuyaangalia machweo"

"Asante sana Rian.. aaah na mahali hapa ni pazuri kuchora."

"Haha tena nafikiri unichore mimi, maana nimeona ile picha asilimia 99 mtu akiiona atajua ni mimi. ... ooooh what a talent Retha," Ed akacheka akifurahi huenda akapata nafasi ya kuchorwa na Aretha.

Aretha akainama kwa aibu, lakini mkono wa Ed sasa uliwekwa juu ya mkono wake na akamsugua huku akimuangalia usoni..akainuka na kwenda kwenye meza iliyobeba kontena la vinywaji...

"Retha utakunywa nini?" Akamuuliza...

"Chochote tu Rian"

Edrian akatoa vinywaji chupa mbili na kuviweka mezani kisha akarudi kukaa. Simu ya Ed ikaita na alimuangalia Aretha usoni kabla ya kupokea.... akaisukuma pembeni huku uso wake ukionesha aliyepiga hakutakiwa kupiga.

"Rian am sorry lakini pokea ili aache kukusumbua" Maneno ya Aretha yalimfanya Ed amwangalie usoni na kuharibu kutabasamu.

Joselyn ndie alipiga simu muda huu wakati Ed hakutaka kabisa kuipokea simu. Akaipokea kama Aretha alivyoshauri na kuiweka sikioni pasipo kuongea lolote

"Ed, umeamua kunidharirisha eeeh?" Sauti ya Lyn ilisikika.

'Mmmmmmm" Ed akaguna pasipo kuongeza neno lolote

"Kweli Ed unaniacha sababu ya huyo msichana? Nakuhakikishia kama utamuoa Anitha...aaah Retha sijui labda nikiwa nimepoteza ufahamu na____"

"Unataka kushindana nami Lyn, then try me"

Baada ya kusema maneno haya Ed akakata simu na alipoweka mkono juu meza Aretha akaweka mkono wake juu ya ule wa Ed. Akampapasa vidole akijaribu kutuliza hasira zilizokuwa wazi usoni kwa Ed.

"Retha..am sorry! " Rian akaomba msamaha lakini majibu ya Aretha yalimshangaza

"Mimi ndie nilikuruhusu upokee Rian, usiombe msamaha. Jaribu kumuelewa na usiruhusu akufanye mtu wa hasira wakati hauko hivyo"

Ed akaangalia mikono ya Aretha iliyomshika, akageuza viganja vya mikono yake akamshika Aretha " Asante 'princess'.I love you Retha. Nitajitahidi kufanya hivyo ulivyosema. Nawe nakuomba usiuachie mkono wangu hata kwenye dhoruba "