Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 79 - UNAMPENDA?

Chapter 79 - UNAMPENDA?

"Aretha, unadhani kaka alikuwa anajua kama Lyn yupo hapa?"

"Mmmh?"

"Alikuwa hajui ndio maana alimuuliza yuko wapi." Coletha akajaribu kumliwaza Aretha ambaye alihisi amemkatia simu kaka yake. Mara Ed alipompigia na kumuulizia Aretha, akajua ile simu iliyoita na haikupokelewa ilikuwa ya kaka yake.

"Coletha, aa unaweza kumuuliza mama kama anaweza kuwa na mbolea kidogo aliyoozesha niweke kabla sijaondoka" Aretha akainuka na kumwambia Coletha ambaye alipomuangalia alishangaa maana hakuweza kuona usoni kwake hisia yoyote ya kukerwa au kuhuzunishwa. Aretha aliendelea kutabasamu huku akimwangalia

"Coletha" Aretha akamuita tena Coletha ambaye alikuwa akimshangaa msichana huyu, akashtuka alipo

"Aaah sawa ngoja nikamuulize. Unaonaje unawe mikono ili nikuletee glovu kama utashika mbolea?"

"Aa..hapana, labda kijembe kidogo tu kitasaidia. Ni sehemu kidogo tu!" Aretha akamwambia kisha akaendelea kuyatazama maua aking'oa majani yaliyokauka.

Coletha akaelekea ndani ambapo mama yake waliendelea na maongezi na Lyn ambaye alionekana kumfurahia mama yake. Akamuuliza kuhusu mbolea

"Coletha, binti wa watu atachoka mwambie aache tutafanya na kina Ann."

Lyn naye akaona aseme "kama anapenda maua sio mbaya akiomba kazi ya kuyahudumia wakati huo atakuwa anajiingizia kipato na mama utapunguza kazi, unahitaji muda wa kupumzika"

Coletha akamwangalia "nadhani kaka Ed atafurahi akiyahudumia maana anavyopenda maua atampa chochote ayatunze"

"Coletha" mama akamuita na kumuangalia

"Mama kwani nini, ulisema kaka Ed anapenda maua tangu akiwa mdogo au nimek____" mlio wa simu ukamkatisha Coletha akaangalia, alipoona ni Ed akapokea huku alielekea jikoni. Kabla ya kusema chochote akasikia sauti ya mama yake

"Coletha, nisaidie Aretha asiondoke. Nakuja usimwambie"

"Okay Bro, fanya upesi anamalizana na maua sasa hivi" Coletha akanong'ona kwa kuwa hakutaka hasa Lyn asikie

Akaelekea nje kwa kupitia mlango wa nyuma, akazunguka hadi bustanini. Akamuona Aretha amekaa kwenye msingi wa bustani akiwa anachora chini kwa kijiti. Aliposogea Aretha akainua uso na pasipo kuondoka tabasamu lake akamwangalia Coletha

"Aretha mama amesema imetosha atamalizia kesho. Upumzike"

"Haaaa lakini haikuwa shida, basi ngoja ninawe mikono nikamuage" Aretha akamwangalia Coletha akiwa na maana wapi akasafishe mikono yake..

"Usiondoke haraka jamani, tupige kidogo stori"

"Hmmm' nitachelewa nyumbani maana huku usafiri sijui naupataje bora niondoke mapema" Aretha akamwambia huku akinawa kwenye karo

Coletha aliposikia hivyo akahisi Aretha hajui kama Ed anakuja kumpeleka au itakuwa hataki ampeleke..

"Aretha kwani Ed hakusema kuwa atakuja kukuchukua"

"Haaa. .aam sitaki kumchosha sana walau apumzike wikiendi" Aretha alisema na akaingiza mkono kwenye mfuko wa gauni akatoa kitambaa na kujifuta

Coletha aliposikia hivyo akajua Aretha hataki Ed amrudishe..

"Aretha unajua kaka atajisikia vibaya kama atafika halafu umeondoka"

"Hmmm" Aretha akaitika kisha akamwangalia Coletha akaanza kuelekea ndani kumuaga mama...

"Aretha, please, usiondoke kama kaka alisema atakuja kukuchukua, sahau upuuzi wa huyu mwanamke" akaamua kumsihi Aretha akageuka na kusimama

"Coletha....aa..n..naomba usimwambie..R Ria..Edrian chochote na wala tusimwongelee kwa sasa. Please" macho ya Aretha ambayo yalibeba upole wote yakamfanya Coletha ashushe pumzi kwa nguvu..

"Okay Aretha. Ila naomba unijibu hili" Coletha akamshika mkono kisha akaendelea

"Unampenda bro?"

Aretha macho yake yalionesha mshtuko na akayakwepesha yasimuangalie Coletha ambaye alitaka apate ukweli

"Aretha please" akamsihi

"I..aa. .Coletha..sijui nijibu nini sababu na____" kabla ya kumaliza alichotaka kusema sauti ya geti lililokuwa lilifunguliwa iliwashtua, macho yao wakayaelekeza getini ili kuona nani alikuwa akiingia. Mioyo yao ilibeba hisia mbili tofauti, Aretha aliomba moyoni asiwe Ed na wakati Coletha alitaka sana awe kaka yake..

Geti lilipofunguliwa gari ikaingia kuelekea sehemu ya maegesho. Kwa kuona gari ile wakajua nani atakayeshuka, Aretha akapiga hatua kuingia ndani hata kabla mlango haujafunguliwa....