Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 77 - ATANICHUKIA

Chapter 77 - ATANICHUKIA

Baada ya kumshusha Aretha, Edrian alielekea kumuona Brian ambaye alimwambia yuko nyumbani na mkewe Rose. Akapita sokoni kuchukua matunda kwa ajili ya Rose ambaye kwa maelezo ya rafiki yake alikuwa katika miezi ya mwanzo ya ujauzito.

Akaingia kwenye gari akiweka mfuko ule wa matunda pembeni, akatabasamu alifikiria siku moja na yeye atafanya hivi kwa mkewe. Picha iliyomuijia kichwani ni ya Aretha akiwa amekaa pembeni akila tufaa huku tumbo likiwa kubwa..

"Hahaha naweza nini mimi hata sijui kama Retha ananipenda" akaondoa gari kuelekea kwa Brian.

Mwendo wa nusu saa alifika Bentford Bay mahali ambapo Brian aliishi. Akapokelewa na rafiki yake wakaingia ndani,

"Bri siku hizi unapika?" Ed akamuuliza rafiki yake baada ya kumuona na eproni iliyofungwa tumboni..

"Hahaha acha tu rafiki yangu!" Brian akasema wakati wakielekea kukaa jikoni ambako alikuwa na mapishi yakiendelea.

Walipoingia jikoni Brian akaweka matunda kwenye karo la vyombo, kisha akasogea kwenye kabati na kutoa eproni nyingine na kumkabidhi Ed ambaye aliingalia

"Hey Bri unataka nipike au?" Ed akauliza akimshangaa

"Hahahhaa osha hayo matunda, namalizia kupika hapa" akamwekea eproni kifuani na yeye akaelekea kwenye jiko la kuokea..

"Bri, umesahau mimi ni 'pro' kwenye kupika, unaniambia kuosha matunda!!" Ed akavaa eproni na kuelekea kwenye karo huku wakitaniana na rafiki yake...

"Najua, ila mpishi mzuri ni muoshaji mzuri he he he" Bri akamtania

"Rose yuko wapi si uliniambia yupo nyumbani?" Ed akauliza wakati akiendelea kuosha matunda

"Yuko chumbani, kapewa mapumziko mpaka 'first trimester' iishe. Maliza hapo ukate ukamsalimie"

"Ah! Haya mambo kumbe yana changamoto, kwa hiyo hatakiwi kutoka?" Ed akauliza..

"Anainuka pale tu anaposikia uwezo kufanya hivyo.. mara nyingi anakuwa na maumivu ya kiuno akilazimisha. Ed bro anateseka kuna wakati najisikia vibaya sana" Bri akazungumza bila kuficha huzuni yake

Ed akasogea na kumgusa begani, "Be strong Bri, atakuwa vizuri tu"

"Yeah, naamini hivyo" Bri akaitikia

"Nani analeta huzuni nyumbani kwangu" sauti ikawashtua na wote wakageuka kuangalia mlango wa kuingia jikoni

"Rose" wote wawili wakaita kwa sauti...

"Aishhh kelele, mnaniumiza masikio, Ed leo umeonekana ndio maana nashangaa nguvu zimetoka wapi ghafla" akaongea Rose ambaye sauti yake ilionesha udhaifu...

Bri akamsogelea mkewe, "Rose you shouldn't move, remember what the Dr sa___"

"I know Bri, aishhh nimechoka kulala, Ed njoo tuketi sebuleni mwachie huyu father house aendelee" akageuka Rose kuelekea sebuleni huku Brian akimshika kumsaidia

Ed akamuangalia Bri na kutabasamu kisha akasema kwa sauti ya chini "namsikiliza mother house Bri. Fanya kama alivyosema"

"Bri akampa ishara ya kujisalimisha kwa kunyanyua mkono juu!"

Baada ya muda mfupi Bri aliungana na wengine sebuleni huku wakishiriki nyama choma, matunda ambayo alikula hasa Rose, na mvinyo.

Mazungumzo yaliendelea kati yao, wakikumbushana mambo ya chuoni. Walionekana kufurahi sana, japokuwa Rose akijitahidi kuwa kawaida kama daktari alivyomshauri.

Kati kati ya maongezi simu ya Ed ikaita,

"Captain" Ed akaitikia

"Bro, uko Insta na Joselyn, check it bro, akaunti GNews"

Alipomaliza kusema hivyo Ed akakata na kufungua simu yake huku akishindwa kujibu swali la Bri lililomuuliza kama yuko sawa...

Dakika mbili zilizofuata Ed alisimama na simu akiongea na Captain kufuatilia chanzo kile cha habari.

"Ed please come down, it's just a news" Bri akamwambia

"Bri, huyu mwanamke kavuka mpaka"

"Mpigie ujue kama anahusika, inawezekana hajui"

Ed akafanya kama alivyoambiwa na Bri, Lyn alipopokea simu swali la kwanza Ed alimuuliza

"Uko wapi?"

"Niko nyumbani na mama, Coletha na____" aliposikia hivyo Ed akakata simu na muda huo kitu kikapita kwenye fikra zake, "Aretha" akajikuta akitamka kwa sauti

"Ed, kuna nini tena, Aretha amefanya nini?" Brian alimuuliza Ed

"Aretha yuko nyumbani, Lyn ameenda huko wakati nilimwambia hatakuwepo, Bri she will hate me" Uchungu ulikuwa wazi machoni kwa Ed

Bri akampa ishara atulie kwanza, "Sweetheart nikurudishe chumbani mara moja upumzike tushughulikie hili"