Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 75 - ALINIDANGANYA

Chapter 75 - ALINIDANGANYA

"Karibu huku mwanangu" mama akamkaribisha huku akigeuka kuelekea jikoni..

Lyn akamfuata, Coletha akiwa kwa nyuma alisonya taratibu na haikupita bila kusikika masikioni kwa Lyn ambaye aligeuka na kumwangalia kisha akatabasamu.

Muda wote Aretha alikuwa ameinama akiangalia simu yake hadi aliposikia mama akimkaribisha mgeni, akainua macho yake kumwangalia. Mara tu macho yake yalipokutana na yale ya Joselyn aliganda kama barafu.."Rian si alisema hatakuja au alinidanganya" akawaza Aretha lakini maneno ya Lyn yaliyofuata yakamfanya ajisikie vibaya zaidi..

"Retha tumeonana tena, naona umewahi sana, leo usafiri ulikuwa hauna usumbufu eeh?"

Kabla Aretha hajajibu tayari Coletha aliyekuwa akiweka sahani mezani akimsaidia "Bro Ed kamleta mwenyewe ili asisumbuke na huo usafiri"

What!! Aretha akajua Coletha kaamsha vitu ambavyo vilimpa hofu kukutana na Lyn. Hakupenda kuonekana kama anashindana nae kwa kuwa alishamuona siku ya birthday ya mama kuwa ni mtu anayemdharau na kumuona hapaswi kuwa karibu na familia hii.

Lyn wakati huu alimeza funda la mate lililomkaba kooni, lakini kama kawaida yake akaweka uso wa tabasamu huku akiketi

"Unamaanisha Ed alikuja nawe mwanangu?" Mama akamuuliza Aretha

"Eh..aah. .ndio mama" Aretha akajibu kwa sauti ya chini huku macho yake yakibaki kuangalia mikono yake...

"Oooh huyu kijana wangu anakuja hata kuniona mama yake hataki aaasssssh! Kuzaa sio kupata" alilalama mama huyu

"Mama mbona anakuja mara nyingi bro unamsingi___" maneno ya Coletha yalikatishwa na mama yake

"Aassssh unamtetea sasa kaka yako, hebu leta na juisi humo tule haya mapishi yako" mama akamzima Coletha ambaye alimaliza kuandaa na kuiweka juisi tayari kula.

Lyn akamwangalia Aretha kisha akayarudisha macho yake kwenye simu akawa akiandika kitu halafu akatabasamu na kuiweka simu mezani.

Habari yako" Aretha akajitahidi kumsalimia Lyn maana hawakuwa wamesalimiana zaidi ya kusikia malumbano ya mama na Coletha..

Lyn akaitikia kwa sauti ya chini kama mtu ambaye hakutaka kupokea salamu..

Mama aliangalia yote haya akielewa kabisa Coletha hakuwa vizuri baada ya kumuona Lyn. Hakujua kwa nini, akachagua kuangalia hadi mwisho ni nini kinaendelea kati yao. Lakini aligundua pia Aretha kuna namna alikosa utulivu kama aliokuwa nao mwanzo.

Wakaendelea kula chakula ambacho aliandaa Coletha, kuku ambao walikaangwa vyema baada ya kuchanganywa na maziwa mgando, ngano na mayai. Coletha aliandaa ndizi za kukaanga na juisi ya embe.

Walikula taratibu huku mara nyingi kimya kikitanda kati yao, lakini usoni kwa Lyn tabasamu fulani lilikuwa wazi. Walipomaliza kula wakaelekea kukaa sebuleni, wamuacha Ann binti aliyesaidia kazi hapo nyumbani akimaliza kuondoa vyombo.

Aretha akawa akiangalia simu yake, lakini alitamani kumtumia meseji Ed, moyo wake ulisita sababu alijua akija Ed wataongozana na Lyn nae hakutaka kuwa gari moja na mwanamke wake. Mawazo yake yakampeleka kuwa huenda Ed alipomfikisha alimfuata Lyn akamleta.

"Aretha, unajisikia vibaya mbona umefumba macho" Coletha akamshtua

"Aah" akashtuka. . Kabla ya kujibu simu ya Lyn ikaita..

Baada ya kupokea walisikia tu Lyn akisema "ngoja niangalie" kisha akakata simu. Akaanza kuangalia tena simu yake, "aaaargh jamani paparazzi hawa" akalalamika Lyn.

"Kwani vipi mwanangu" mama akauliza kwa kujali, huku macho ya Aretha na Coletha yakimwelekea Lyn

"Sorry mama, kuna watu wametuma picha hizi kwenye mitandao sasa wananitafuta" akajibu Lyn huku akisogea kumuonesha mama picha. Kitendo hiki kikamfanya Coletha ainuke na kusogea alipokuwa mama yake..

Coletha alipoinama aliona kwenye simu ya Lyn picha tatu zilizoonesha Ed akiwa amembeba Lyn kutoka hoteli, ya pili akiwa anamuingiza kwenye gari na ya mwisho akiwa hospitali amemkumbatia Lyn. Kichwa cha habari kiliandikwa "Senior Bachelor na mchumba wake hadharani" wanatarajia mtoto au?

Macho ya Coletha yalimtazama Lyn na kisha Aretha ambaye aliendelea kukaa kimya asielewe nini kinachoangaliwa.

"Ulikuwa unaumwa binti yangu, mbona Ed hakusema" mama akamuuliza Lyn ambaye aliinuka na kurejea alipokuwa amekaa

"Niliugua ghafla tu tulipotoka hoteli na Ed"