Lyn akamwangalia Ed, kisha akainuka tena alipokuwa amekaa, akaweka mikono kiunoni...
"Ni kwa sababu ya huyo Anitha eeh, unatafuta sababu za kuwa mbali na mimi, unamsingizia baba anakuharibia deal za kampuni...Edrian unataka kuniacha?" Lyn akamwangalia usoni kwa hasira
Ed hakujibu chochote...akamwangalia Lyn na kujiuliza ni nini kinaendelea ndani ya huyu binti. Alikuwa akibembeleza mara ghafla amekasirika..
"Babe...hujui kwa kiasi gani unaniumiza moyo wangu! Huyo Anitha ana nini hata amekubadili hivyo uwe kinyume na mimi. Hutaki nikuguse, hutaki tuwe pamoja, unashtumu kwa mambo ambayo sijafanya... kwa nini lakini" akajitupia kwenye kochi na kuweka kichwa chake kati ya magoti huku akilia tena...
Ed ambaye alisimama pale dhamiri yake ikiwa njia panda... akili yake ikitaka awajibike kwa kuzichezea hisia za binti huyu, uungwana wake ameutupa wapi, lakini moyo wake ulimwambia vingine.
Akashusha pumzi na kumsogelea Lyn akakaa pembeni yake... mkono wake ambao ulikuwa na mgomo kumgusa Lyn, hatimaye ukampapasa taratibu mgongoni.
"Usilie Lyn...hakuna aliye nibadilisha moyo." Ed alipomaliza kusema hivi dhamiri yake ikamsuta " una hakika moyo wako haujabadilika"? Akajikaza na kuendelea
"Lyn hebu tulia kwanza tuongee, kuna mambo ya kuweka sawa..?"
Lyn akainua kichwa, macho yake yalianza kuvimba na wekundu uliosababishwa na kulia ulionekana...
"Mambo yapi Ed...uliniahidi wiki hii utanivisha pete...sasa hivi huongelei tena. Unanifokea mara zote na sijui unawaza nini?"
Kabla Ed hajajibu...mlango ukagongwa na wote wakashtuka kuelekeza macho mlangoni.
Ed akainuka kwenda mlangoni, alipofungua akakutana na Li
"Za asubuhi bro" akasalimia
"Salama" Ed akajibu huku akipikicha macho yake kuonesha alikuwa amechoka..
"Vipi ulitoka nje maana nimegundua mlango uko wazi?"
"Oooh ndio, nilit...."
"Li umeamkaje" Lyn akasimama nyuma na kusalimia huku mikono yake akiipitisha kiunoni kwa Ed ambaye alikakamaa mwili ghafla
Li ambaye alisimama nje ya mlango alipoona hivyo akameza mate na kuitikia salamu...."Salama Lyn, karibu"
"Asante shemeji" Lyn ambaye kama Ed au Li wangepata kumuona, alikuwa na tabasamu la kejeli kwa Li
Ed ambaye uso wake sasa ulionesha wazi kukaribia kupasuka kwa hasira ulimfanya Li ambaye alisimama pale mlangoni kuaga
"Bro niko gym baadae"
"Mmmmm" mguno ulimtoka Ed ambaye aligeuka kwa kuwa Lyn alimwachia baada ha kusikia Li ameaga..
Akarudi ndani, hakukaa tena kwenye kochi akaelekea mpaka kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya meza akajitupia, akachukua chupa ya maji iliyokuwa juu ya meza. Ed akanywa maji yote pasipo kupumzika. Macho yake yalikuwa mekundu
Lyn ambaye sasa alikaa kwa upande juu ya meza alimwangalia Ed akijua wazi kabisa kitendo kile kilimkwaza..
"Babe una. .."
"Lyn unaweza kuniambia nini makusudi ya ujio wako asubuhi hii, nina kazi za kufanya" mtetemo wa sauti ya Ed ulionesha kukwazwa na Lyn
"Ed...kuna shida kukimbilia kwako ikiwa mimi na baba tumetofautiana?" Akauliza Lyn huku akiinama kumuelekea Ed..
"Uko hapa kwa muda gani" Ed akauliza
"Kwani wewe unatakaje babe" Lyn akamuuliza
Tik tik. .
Meseji kwenye simu ya Ed ikaingia, akaitoa simu iliyokuwa mfukoni mwa pajama yake na kuangalia
Meseji ya Aretha....uso wa Ed ukang'aa ghafla kitendo ambacho hakikuweza kumpita Lyn pasipo kuona...
Kabla Ed hajajibu, Lyn akaichukua simu kwa ghafla mkononi mwake kitendo ambacho kilimfanya Ed kuinuka kwa hasira
Lyn alipoangalia hakufanya chochote akataka kujibu lakini mkono wa Ed ulimkamata kwa nguvu na kusababisha simu kuanguka mezani... akiwa ameushika mkono wa Lyn,
"If you ever do that again Lyn consider me your greatest enemy...read again my profile" akamwachia mkono na kuchukua simu hakumwangalia tena akapiga hatua na kutoka ofisini...
"Naomba uondoke" akageuka na kumwambia kisha akaendelea pasipo kugeuka nyuma...
Lyn hakusema lolote akaachia tabasamu laini...
"We shall see Ed, mimi ni Joselyn Martinez"
Akajitupia kwenye kochi huku miguu akiinyoosha pembeni na kufumba macho. Akashusha pumzi. ..
"Oooh kumbe ni Retha na sio Anitha... nina shauku ya fair play na wewe. Game on" akatabasamu