Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 55 - HAYANA KANUNI

Chapter 55 - HAYANA KANUNI

Edrian aliyekuwa ameinama akashusha pumzi.....akageuka na kumwangalia mama yake....

"Baba hakukosea kukuoa mama, asante" akamshukuru mama yake...kisha akainuka na kumuaga

"Mbona hata hatujamaliza kuongea mambo ya kampuni umeinuka tayari?" Mama akalalamika...

"Mama haya ni ya msingi... ya ofisini utapewa ripoti kwenye kikao cha bodi hivi karibuni." Edrian akaendelea kupiga hatua taratibu akimuacha mama yake akiendelea kulalama

"Huyu mtoto na kanuni zake aishhhh" mama huyu alijua ambavyo mwanae hapendi kabisa kuleta mambo ya ofisini nyumbani labda iwe dharura ambayo ingehitaji suluhu ya wakati huo

Edrian alipoingia garini akachukua simu...

"Hellow Lyn" kwa sauti tulivu nzito Ed alisalimia

"Umerudi tayari?" Lyn aliuliza huku shauku yake ikiwa wazi...

"Ndio nimerudi..." kabla hajaendelea

"Uko wapi Ed nina hamu ya kukuona" Lyn akaongea kwa kudeka

"Niko kwa mama...Lyn tunaweza kuonana kesho jioni?" akamuuliza kwa taratibu...

"Hakuna shida babe.... are you okay" Lyn akauliza kwa kujali

"Yes...am okay. Jioni njema Lyn" akaaga lakini kabla ya kukata

"Edrian....you are so cold to me these days!..una-date na yule Anitha?" Sauti ya Lyn ilionesha kabisa kukerwa na namna ambavyo Edrian alimchukulia

"Lyn..see you tomorrow" akakata simu na kushusha pumzi...

Kabla ya kuondoa gari akampigia Derrick....

"Utarudi nyumbani lini" akamuuliza

Brother kuna shida ndani? Akauliza Derrick ambaye aliweza kuisoma sauti ya kaka yake

"Hapana D, nimekukumbuka...by the way, kwa nini unaamini Lyn so mtu mzuri kwangu?"

"Bro tunaweza ongea hili wakati mwingine?" Derrick aliomba alijua tayari kaka yake hakuwa kwenye hali nzuri

"Mmmmmm" Ed akaguna

"Bro nitakuja kesho tuongee, najua ninastahili kukwambia sababu gani inanipa kusema hivyo"

"Okay bro, muda wa mchana utafaa. Tuna busy ratiba ofisini."

"Sawa Big Bro, take care" Derrick akamjibu

"Okay. Thanks." Akakata simu na kuanza kuondoa gari ndani ya geti tayari kuelekea nyumbani....

Akiwa barabarani alianza kufikiria kama Derrick alikuwa hakubaliani na Lyn ni nini alikifahamu ambacho yeye hakuwa anakifahamu....Lyn ni mzuri, uzuri ambao hata hata yeye anakubali ulimvuta hasa mara zote walipokutana accidentally... lakini bado hakuwa na hakika na msukumo wa Lyn kwake.... "aaah hata hivyo sijui wa Aretha pia". ..akajisahihisha

"Na kwa nini navutiwa na binti wa kawaida tu ambaye hata hatuko kwenye arena moja ya biashara...aaaargh.....ndio maana I prefer business mapenzi hayana kanuni... what if Aretha nae anatumiwa na mama yake... mama yake anataka niwe karibu na mwanae...Why!

akashusha pumzi na kuelekea nyumbani akidhamiria kufanyia kazi hekima za mama yake..

"Nitaongea na Lyn na nitakuwa karibu na Aretha kwa lengo ambalo mama yake ameniomba." Edrian aliamua moyoni...

Meseji ikaingia kwenye simu..... akakusudia kutoiangalia hadi atakapofika nyumbani...

*********************

"Sorry Retha nilikuwa naendesha" akaandika Edrian baada kufika nyumbani akiwa ameegesha gari akaamua kuangalia simu yake!

Alisikitika maana hakujua kama ni Aretha ndie alimtumia meseji... akasubiri akiwa ameegamisha kichwa kwenye kiti huku macho yamefumbwa....

Dakika kumi zikapita huku Ed akipitiwa usingizi, akashtuka na kuangalia simu hakukuwa na mrejesho wa ujumbe wake kwa Aretha..... akaandika

"Usiku mwema Retha"

Akashuka na kuelekea ndani, alipotoka bafuni haikuchukua muda kupitiwa na usingizi.

******************

Simu ilimuamsha usingizini..... alipoangalia alikuwa ni Lyn...saa ya ukutani iliyafanya macho yake yafumbuke kwa nguvu maana ilikuwa alfajiri ya saa kumi na nusu. ..

"Hello babe"..sauti ya Lyn ilisikika baada ya Ed kupokea simu

"Lyn what is..." sauti ya Ed iliyojaa mikwaruzo ya usingizi ilikatishwa

"Ed I want to see you niko nje ya geti" Lyn akasema kwa upole

Ed aliyekuwa bado amelala akainuka taratibu na kupikicha macho kuhakikisha alikuwa hayuko ndotoni...

"Kuna shida gani Lyn?" Akauliza

"Nashuka kwenye gari mwambie mlinzi anifungulie maana simuoni huku nje na sitaki kugonga" Lyn akaongea kwa ujasiri

Edrian alishusha pumzi na kuingia kitandani...

*********************

Unaposoma usisahau ku-like, ku-comment na ku-vote... tuwezeshe webnovel kuona lugha ya kiswahili ni lugha kubwa na ina watumiaji wengi