"Mama, si tu kwa sababu ni kaka yangu bali ni mtu ninayemfahamu kuwa akisema kitu yuko tayari kuupindua ulimwengu wote akipate kile anachotaka!" Derrick akamtetea kaka yake. Ni damu moja.
"Una uhakika na hisia za kaka yako kwa binti yangu?" Mama akamuuliza
"Sina shaka nazo mama, na sina wasi wasi na Retha kuwa anaweza kumpenda Edrian.."
Mama akashusha pumzi,
"Kwa hiyo ile picha ulimpelekea kaka yako?"
"Ndio mama, na aliweza kugundua, japokuwa nilijaribu kumkwepa...natamani kuamini hawa watu wanapendana!" Derrick akajibu....
"Sawa mwanangu, nitajua cha kufanya, ila nakuomba tena usijali kuficha chochote kuhusu wewe au kaka yako" mama alimsisitiza
"Sawa mama, asante kunielewa na kunisamehe." Derrick akaonesha unyenyekevu baada ya kuyaona makosa yake.
Mama alipokata simu akaguna mwenyewe...
"Wote wanapendana lakini hakuna aliye na uthubutu wa kusema... ngoja tuwasaidie" akajisemea mama wa watu na kuinuka kuelekea katika majukumu yake ya bustanini...
****************
Ed alipoondoka kwao Aretha, akapokea simu kutoka kwa Captain... na safari yake haikuelekea tena nyumbani bali alielekea The Base kwa ajili ya kuonana na 4D.
"Hiyo gari uliyoiona imesajiliwa kwa jina la Matheo Teshau, na ni kweli kabisa ndio ile ile ilikupita usiku wa jana. Tofauti ni kuwa ulipotoka ofisini haikukufuatilia. Nimejaribu kufuatilia nyendo zake zilipotea ghafla na sina uhakika ni kwa nini CCTV eneo hili la Lavender hazikuwa zikifanya kazi" Captain akamweleza Ed ambaye alikuwa amesimama akitazama nje kupitia kioo ndani ya ofisi hii!"
"Mmmmm" Ed aliguna
"Bro nimejaribu ku-zoom lakini sura bado hazijakaa vyema... usiwe na wasi wasi! Ndani ya siku mbili kila kitu kitakaa vizuri" Captain akampoza Ed maana anajua anapokuwa hajafurahishwa na kitu...
"Vipi kuhusu huyo mdukuaji?" Akauliza Ed taratibu
"Nimepata IP namba ya kompyuta iliyotumika.. na kesho kila kitu kitakuwa wazi. Kwa sasa kuweni makini na wasikubali kufungua kitu wasichokuwa na uelewa nacho. Chumba namba 307 ndimo kazi ilifanyika" Captain aliendelea kutoa taarifa
"Sawa, Captain...naomba unisaidie kufuatilia simu ya Joselyn, najua nachofanya ni kuingilia maisha ya mtu. Nina wasi wasi na ujasiri alionao Lyn. She might be hiding something from me"
"Kesho nitakuwa na ukaguzi ground zetu zote, naweza nikawa hapa Alhamisi, kuna mtu nataka nikuombe wewe specifically umweke katika uangalizi wako"
"Hakuna neno brother. ..nitafanya kile naweza kufanya...."
"Nitakutumia details zote once nikimaliza kuziandaa"
Edrian alipomalizana na Captain akaondoka kuelekea nyumbani huku njiani alikuwa akiwasiliana na Allan kujua kama amejiandaa kwa safari na kupata uthibitisho wa kutoka kwa Loy. . Akaangalia tiketi aliyotumiwa na Loy kwenye barua pepe yake..
Moyo wake ukashtuka....si kawaida ya Lyn kunyamaza kimya bila kumtafuta pale ambapo yeye hatamtafuta....
Akaangalia simu yake lakini akawa mzito kutoa amri simu impigie... " nataka kupumzika sina mood ya kusikiliza malalamiko" Ed akajisemea..
****************************
Oparesheni za SGC katika miji minne zilikuwa katika ukaguzi wa kina uliofanywa na wasimamizi wa operasheni pamoja na Mkurugenzi Mkuu Edrian na meneja operasheni Allan....
Waligundua uzembe wa hapa na pale katika baadhi ya idara, bado walikuwa na mengi ya kuboresha ili kuweza kuepuka rungu ambalo lilionekana kuwatafuta ili kuwasagia mbali na biashara hii ya madini..
Edrian ilibidi alale G-Town ambako ndiko kulipokea onyo kutoka Taasisi ya Kuhifadhi Mazingira. Baada ya kupitia taarifa mbali mbali na nini kilisababisha. ..akashusha pumzi na kuegama kwenye kochi lililokuwa ndani ya chumba hiki cha hoteli aliyofikia..
Akainua simu yake na kupiga kwa Allan ambaye yeye alilala K-Town..
"Brother bado hujapumzika?" Ilikuwa saa saba kasoro usiku na Ed alikuwa macho huku pembeni kikombe cha kahawa kilionesha wazi anayekunywa hana mpango wa kulala.
"Allan nahitaji kuwa na mazungumzo na wanasheria, kuna mikataba ya watu itatakiwa kusitishwa, am afraid this was a set up, kuna mtu aliandaa mazingira yale"