Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 35 - ANA KWA ANA

Chapter 35 - ANA KWA ANA

Muda uliwadia ambao uliandaliwa kwa ajili ya sherehe fupi ya kumpongeza Mrs Simunge ambaye ni mama wa Edrian katika siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake. Watu wachache walikuwa tayari wameketi katika viti vilivyoandaliwa nje kwenye bustani ya maua iliyokuwa pembeni mwa nyumba. Hakukuwa na nakshi nyingi lakini muonekano wake ulivutia. Viti viliwekwa katika umbo la nusu duara, mbele paliwekwa kiti ambacho kilionesha wazi ni kwa mhusika wa ile sherehe. Kwa jumla ya viti kwa haraka havikuzidi ishirini.

Edrian akiongozana na Joselyn, Linus, Coletha na watu wengine wachache walishawasili. Baada ya kufika Ed alielekea ndani kumsalimia mama yake ambaye wakati huo alikuwa na mtu wa urembo aliyeandaliwa kumtengeneza jioni ile. Japokuwa Ed alimuomba Lyn amsubiri nje, hakukubali na akafuatana naye hadi ndani.

Walipofika kwenye chumba cha mama yake, Ed aligonga mlango kuomba ruhusa ya kuingia.

"Nani tena jamani?" Sauti ya mama yake iliuliza kuonesha hakutaka mtu aingie.

"Ni mimi mama, naweza kuja kukusalimia?" Alijibu Edrian

"Baadae, anamalizia" alijibu mama yake..

"Sawa mama" aligeuka na kumpa ishara Lyn warudi lakini hakuonekana kutaka kufanya hivyo. Ghafla bila kutarajia Joselyn akagonga mlango wakati akisema

"Mama naweza kuja kusaidia chochote?"

Ed alimwangalia na kuachia mguno wake kama kawaida..

"Mmmmm"

Joselyn akatabasamu kwa ushindi na wakati huo mlango ulifunguliwa na akatoka mwanamke ambaye muonekano wako ulionesha kuwa ndie mpambaji wa mama, akampa ishara aingie huku akimsalimia Ed ambaye alisimama pembeni.

Baada ya Lyn kuingia ndani, mikunjo laini ilionekana kwenye uso wa Ed na kisha akapiga hatua kwenda bustanini kukaa. Alipofika nje hakuamini macho yake, ni Derrick mdogo wake ambaye alikuwa akiingia huku ameongozana na Aretha ambaye ni wazi aliona aibu akijaribu kuyaepuka macho yake na watu.

Akaanza kupiga hatua taratibu kuelekea alipo Linus ili kumuuliza nini kinaendelea, lakini kabla ya kufanya hivyo Mshereheshaji (Mc) akawaomba watu waketi kwenye viti vyao. Ed akaelekea mahali palipoandaliwa kukaa macho yake yakagongana na Linus ambaye nae alionesha wazi wazi kushtushwa na uwepo wa Aretha.

Derrick akawaona na kuwasalimia kwa furaha huku akibeba tabasamu lake murua.. Mshangao sasa ulikuwa mkubwa kwa Aretha maana hakuamini kama, Edrian alikuwa mbele yake, ikasababisha mkazo wa mkono wake kuzidi katika ule wa Derrick aliyemshika.

"Retha, meet my elder brothers, Edrian na Linus Simunge" Derrick alitambulisha ndugu zake kwa Aretha huku akiliona jicho la Edrian kwake lilikuwa kama moto na alionesha wazi kutaka majibu ya maswali yaliyopita kichwani kwake.

Kwa tabasamu la ajabu usoni Aretha akatoa salamu kwa ndugu hawa,

"Hello"

"Tumeonana tena Aretha, karibu sana nyumbani" Li aliamua kuvunja ukimya maana Ed hakuweza hata kujibu ile salamu macho yake yalimtazama kwa mshangao Aretha.

"Ooooh kweli, nashukuru" Aretha akajibu na kurudisha macho chini maana macho ya Ed yalitulia kwake bila kusema chochote..

Li akamshtua "Bro umesalimiwa"

Ed akayarudisha macho yake kwa Derrick na akajibu huku akimtazama "Njoo mara moja, sorry Aretha nakuja sasa hivi"

Derrick akaachia tabasamu na kumuaga Aretha huku akimkabidhi Linus..lakini kabla hajaondoka na kumfuata Ed ambaye alisimama akimsubiri, Coletha akawajia kwa haraka..

"Bro mbona mmesimama wakati tunaanza, mama kasema tukichelewa anaenda kulala" alipomaliza aligeuka na kugundua uwepo wa Aretha ambaye muda huu alikuwa na Linus.. Coletha akamsalimia huku akimwangalia Li kuonesha kufurahishwa na uwepo wa Aretha akidhani ni mgeni wake.

"Karibu sana dear, naitwa Coletha dada yake Linus"

"Heehee dada yangu?" Li akamtupia jicho la kumtania

"Naitwa Aretha" walau kwa Coletha alionesha kupunguza aibu .

"Twendeni tukakae jamani mama anakuja sasa hivi, we Derrick unachakujibu tukimaliza" Coletha akawaambia huku akiukamata mkono wa Aretha na kuwafanya wote wamfuate.

Akamuongoza kwenye kiti akiamini Li angefuata, akashangaa Derrick ndie aliyekaa mkono wa kushoto wa Aretha. Li akakaa pembeni ya Derrick.

Ed aliyekuwa amesimama akabaki njia panda asijue wapi akae.