Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 34 - ONYO AU VITISHO

Chapter 34 - ONYO AU VITISHO

Ed alitangulia kwenye gari akimsubiri Joselyn ambaye alielekea maliwatoni. Akatoa simu yake na kupiga

"Hello Captain" akasema baada ya simu kupokelea

"Ooooh good, Asante sana." Akamshukuru na kukata simu.

Kitu ambacho Joselyn hakujua ni kuwa wakati Ed anaenda chooni, hakika hakwenda, bali ilikuwa ni mtego ambao waliuandaa kumnasa. Captain alikuwa yuko hapo na aliwahudumia bila Lyn kujua. Walikuwa wameweka mtego pasipo shaka wakitarajia nini ambacho Lyn angefanya baada ya kupata taarifa ile. Wakafaulu katika jaribio lao

Ed alitabasamu na kuangalia simu yake ambayo ilikuwa na ujumbe ulioingia, kisha akasema taratibu

"Well"

Joselyn pasipo kujua aliingia kwenye gari na wakaondoka eneo lile. Njiani akili ya Ed ilikuwa ikihama hapa na pale barabarani hadi kumfanya Lyn kumshtukia

"Babe, uko mbali sana, unawaza nini?"

Huku macho yakiwa barabarani akamjibu

"Niko okay". Jibu lile halikumridhisha Lyn akaamua kusema alichohisi

"Ed, nitamuuliza baba kuhusu huo ushahidi, please usiwe hivyo unanitisha" Lyn akalalamika

"Mmmmmm" Ed alikunja uso na kuguna baada ya kusikia Lyn akimzungumzia baba yake. Akatamani kumwambia kile alichoona kule walipotoka, lakini akasita akijua sio wakati muafaka.. akashusha pumzi na kuendelea kuangalia barabarani

"Halafu mbona huongelei pete tena, kuna kitu kinaendelea eeeh" akauliza Lyn ambaye kuna namna alianza kuwa na mashaka badala ya kupata jibu aliambulia mguno. Alijua ni ishara ya kwamba Ed hataki kuongelea suala hilo...

"Unaonaje tukiacha huu mjadala Lyn, let us not spoil our evening " Ed alijibu na kumtupia macho makali ya kutotaka kuendelea

"Ed, usinifanyie hivyo, please usiniache njia panda, kuna nini kinaendelea?"

"Mmmmm"

Lyn hakutaka kuendelea akaamua kunyamaza na kufanya safari iendelee kwa ukimya kati yao. Wakati Ed akiwa makini na usukani Lyn akaweka umakini wake kwenye simu. Mpaka alipofika nyumbani kwa kina Lyn na kupiga honi ili mlinzi amfungulie geti.

"Edrian, usijaribu kunichezea akili yangu, let us talk another time... usiku mwema" Lyn akashuka kwenye gari baada ya geti kufunguliwa na mlinzi alisimama nje akisubiri Lyn aingie.

Macho ya Ed yalimwangalia Lyn alipoelekea getini ndani yake akiyashangaa maneno yale aliyoyasikia mdomoni kwa binti huyu, akajiuliza ni onyo au vitisho. Akaachia tabasamu la pembeni kisha akaondoka baada ya geti kufungwa...

Akiwa njiani akakumbuka hakuwasiliana na Aretha, akaangalia simu yake na kwa mfumo aliotumia ilikuwa rahisi sana, akaimbia

"Call Aretha"

Simu ikapiga mara hiyo, naye akiwa na vipaza sauti masikioni akasubiri simu ipokelewe. Sekunde kumi na tano zilipita simu haijapokelewa, akakata tamaa na kutaka kuikata simu mara ikapokelewa

"Helloo" ilikuwa sauti iliyobeba mawimbi yaliyodhihirisha alikuwa amekimbia kuiwahi simu

Ed akatabasamu kisha akaitikia, "Hello Aretha" akanyamaza kumsikiliza lakini aliishia kusikia kikohozi laini

"Am sorry, muda utakuwa si sahihi nadha...."

"No no no aaah it's okay, nimeshtuka tu kujua ni wewe unaye..aaah nipigia" Aretha alimkatisha Ed ili asiendelee kuomba msamaha. Ed hakujua kuwa mara baada ya kuona simu Aretha alisita kupokea akijiuliza ataongea nini..

"Oooh asante" akashukuru Ed na kisha akamuuliza

"Umepata chakula cha jioni?"

"Yes...aaah no.. hapana?" Hakuweza kudanganya, mara nyingi hupitiwa kula kwa muda unaotakiwa.

Upande wa pili Ed aliposikia hivyo, akaangalia saa akataka kuondoa mashaka yake kwa kuuliza 'kwa nini'. Lakini kabla ya kufanya hivyo, Aretha aliwahi kujieleza

"Nitakula sasa hivi, nili ....aaah.... nilisahaulishwa na kusoma kitabu"

"Oooh....ni vizuri ule on time hasa usiku" Ushauri ambao Ed aliutoa kwa dhati maana ndivyo naye alishauriwa na daktari wake..

"Sawa, asante.. amhhh nitakula mara tukimaliza..."

Ed akaachia tabasamu, kimya cha sekunde kadhaa kilipita japokuwa aliweza kusikia kuhema kwa Aretha kutoka upande wa pili.. akaamua kuanzisha mazungumzo huku akiwa amesimama kwenye taa za magari..

"Ulikuwa unasoma kitabu gani?"

Kama angepata kuuona uso wa Aretha wakati huu angetabasamu maana alifanana na binti mdogo aliyeona watu kwa mara ya kwanza.