Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 33 - MARAFIKI MAADUI

Chapter 33 - MARAFIKI MAADUI

"Siku ile hukutaka nikumalizie lakini ni kweli alinikaba shingoni baada ya kubishana nae aliponikatalia nisiingie chumbani kwako, uliona alama ya vidole vyake haikuwa love bite Ed."

"What" Ed akashtuka

"Babe ulipanick na mimi nikaogopa, isingekuwa rahisi kuongea chochote ukanielewa" Joselyn alijitetea huku akipapasa mkono wa Ed uliokuwa mezani!

"Okay Lyn, na kwa nini ulipoona nimetulia haukutafuta kunieleza yote yaliyotokea?" Sauti ya Ed ilikuwa ya chini na taratibu, hizi kwake ni dalili za kukerwa.

"Ed, sikuwa na ujasiri wa kutibua yaliyolala. Halafu sikutaka kukuchonganisha wewe na ndugu yako" Lyn aliongea pasipo kupepesa macho..

Kimya kifupi kilipita, Ed macho yake yalikaza kutazama ziwani yakionesha wazi alikuwa kwenye dimbwi la mawazo..

"Okay Lyn. Let's us not discuss it anymore" muonekano wa Ed sasa ulianza kurudi na kumfanya Joselyn afurahi na kutabasamu huku akijilaza begani kwake.

"Thank you babe"

Wakati wakiendelea kusubiri oda ya chakula, Ed akaona ni wakati muafaka kuhoji nini Lyn anafahamu kuhusu baba yake..

"Lyn" aliita Ed ambaye wakati huu alipitisha mkono wake kichwani kwa binti huyu alikarudisha nywele zake zilizokuwa zimesimama sababu ya kiupepo kilichovuma kutokea ziwani hapo..

"Abee" Lyn aliitikia kwa kudeka huku masikio yakiwasha kujua jambo gani jingine Ed amegundua. Alihisi leo watakuwa na mazungumzo mazito kuelekea uchumba.

"Najua unanipenda, au nakosea?" Ed aliuliza huku akimwangalia machoni Lyn kitu ambacho kiliamsha hisia za tofauti kwa aliyeulizwa..

"Bila shaka kabisa" Lyn alijibu na kumwangalia Ed machoni,

"Basi naomba uniambie ukweli kuhusu mambo ambayo baba yako anafanya kwa kampuni yangu?"

Lyn akainua macho kwa mshangao na kuuliza "mambo yapi Ed?"

Akamwangalia usoni na kumjibu, "Baba yako anafanya njama za kuharibu kila 'proposal' ya SGC inapoenda Boric" akashusha pumzi na kuendelea

"Nimefuatilia na nina taarifa zenye ushahidi, unadhani ni kwa nini anifanyie hivyo?"

Lyn akajiweka vyema kwenye kiti kisha akamshika Ed mkono ambao ulikuwa huu ya meza na kusema.."Mambo ya baba yangu siyajui, na sijui kwa hakika anahusika au la! Lakini babe kwa nini unaamini ana njama mbaya?"

"Kwa nini nisiamini Lyn?, biashara zina maadui wengi wenye sura ya urafiki, lakini anguko langu ni kuinuka kwa mwingine" Ed alijibu na kisha akatoa simu yake na kutafuta picha kisha akamuonesha Lyn.

Lyn aliangalia kwenye kioo cha simu ya Ed, na macho yake yalibeba mshangao, kisha akasema, "Edrian.. sijui chochote na huu ushahidi unaonionesha waweza kutengenezwa....sio mimi wala baba tunaokuharibia"

Ed alimwangalia usoni Lyn halafu akachukua simu yake na kuiweka pembeni. Akashika mikono ya Lyn kwa pamoja na kusema, "kama hujui sitakulazimisha Lyn, na kama ushahidi huu ni bandia nitaendelea kumtafuta aliye nyuma ya ushahidi huu. Let's enjoy the moment"

Lyn akaachia tabasamu la furaha na kumbusu Ed shavuni.. "Asante kunielewa babe"

Wakati huu mhudumu alisogea na oda yao ya chakula. Baada ya kuviweka mezani na kuwakaribisha, Ed akamuomba Lyn aendelee wakati yeye akiinuka kuelekea maliwatoni.

Ed alipopotelea kwenye mlango uliomtoa kuelekea vyooni, Lyn alitoa simu yake na akaandika kitu kwa haraka kwenye simu yake. Baada ya kufanya hivyo akarudisha simu kwenye meza akageuza kuona kama kuna mtu alimuona, alipohakikisha hakuna akajiweka vyema na kuanza kula.

Ed aliporudi, akajumuika na Lyn kuendelea kufurahia chakula kwa pamoja huku mazungumzo mepesi ya hapa na pale yakipita kati yao. Walipomaliza, mhudumu alitoa vyombo vilivyokuwa mezani na wakaendelea kuangalia machweo ya jua yaliyofanya mandhari ya hotel kuvutia zaidi.

"Babe, inakuwaje Jumatatu?" Aliuliza Lyn.

Huku akiwa ameegama kwenye kiti chake akajibu, "Nitatoka saa kumi, niambie wapi nikupitie?"

"Nipitie nyumbani"

"Kwa nini nisikukute dukani kwako maana ndio karibu na njia ya Estate?" Ed akauliza maana nyumbani kwa kina Lyn na njia ya kwenda kwa mama yake Ed wangetumia dakika 30 kuepukana na foleni.

"Sitaki kwenda bila maandalizi Ed. Please" Lyn alimsihi

"Mmmmm" Ed aliguna

"Babe, please"

"Okay" hakutaka kubishana Ed akakubali