"No.. bro sina spy, am sorry ni vile siku picha inachorwa nilimuomba Bro Li anitumie picha yako na akanitumia hiyo." Derrick alimua kuficha ukweli, Ed naye hakumuacha kwa wepesi
"Kwa hiyo Li nae alihusika?" Ed aliuliza huku mikono yake ikiendelea kupapasa picha ile
"Noo Bro! Nilimuomba anitumie sababu nilikukumbuka sana" akaweka na tabasamu lake kumlainisha Ed, ambaye sasa aliinua macho na kumwangalia Derrick kisha akatabasamu na kuuliza
"Naweza kumuona huyo aliyechora?" Ed bado alikuwa na shaka kwa kuwa mtu pekee ambaye aliona kitendo cha yeye kuchukua ule mfuko pale mezani ni Aretha.
"Nitaongea nae, nitakujulisha atakapokuwa tayari" Derrick akamhakikishia
Wakati hayo yanaendelea kwenye chumba cha kusomea, nje ya mlango, masikio ya Coletha yalibanwa hasa kutaka kusikia yanayoongelewa na ndugu zake. Mara alipohisi wamemaliza maongezi alinyata taratibu akirudi sebuleni. Akaanza kumtafuta Linus ambaye wakati huu alikuwa amekaa barazani.
"Bro Li, wewe unanificha mambo yako na D sana" Coletha alimvamia Li ambaye wakati huu alikuwa akisoma riwaya ya "The righteous Killer".
"Coletha hivi unajua kushinda nyumbani na wewe ni kazi sana?" Li alisema kuonesha dhahiri alikerwa na dada yake, ambaye sasa alikaa kwenye mkono wa kochi alilolikalia
"Kaka jamani" Coletha akajibu kwa kubembeleza
"Haya sema nakusikiliza" akasema Li na kuacha kusoma kitabu
"Ulimtumia picha D?"
"Hapana" alijibu Li kisha akarudisha kitabu lakini kabla hajaanza
"Mbona D kasema...." kabla Coletha hajamaliza Derrick na Ed walikuwa wamefika pale barazani. Coletha akaachia tabasamu la wasi wasi alipohisi Derrick alimsikia
Derrick akainama na kumnong'oneza sikioni,
"Punguza umbea" halafu tabasamu likafuata usoni kwa Derrick na kumfanya Coletha amwangalie kwa sura ya dhihaka.. akamgeukia Ed ambaye muda huu akili yake ilikuwa bado kwenye picha. Alitamani kumuuliza Derrick kama hiyo picha haina uhusiano na Aretha bado ilikuwa haiingii akilini kwa nini mazingira ya siku hiyo yalikuwa halisi sana kwenye ile picha.
Wote kwa pamoja wakaa kwenye viti vilivyokuwa mahali pale. Wakaongea kwa furaha wakijadili mambo mbali mbali, likiwemo la 'birthday' ya mama yao ambayo ni jumatatu. Wakakubaliana kuonana pale nyumbani mida ya jioni. Na kwa kuwa mama yao hakutaka sherehe kubwa Coletha aliwahakikishia watakuwa na wakati mzuri wa chakula cha pamoja.
"Great, ukiwaalika watu wengi, tayari itakuwa sherehe, weka list yako ndogo" Derrick akamwambia dada yake
"Hey huniamini nini, namjali mama bhana" Coletha alijitetea
"Mmeanza aaahhhh" Li aliwashtua.
Ndugu hawa walikaa kwa muda mpaka Ed alipopata simu iliyomfanya atoke nyumbani mida ya jioni...
"Derrick unarudi lini?" Coletha akamuuliza
"Baby sisy bado, kule Heaven ni mbinguni kweli" alitania Derrick.
"Hey D, umefanya vyema kuja" Li akampongeza kisha akaendelea... "na nini kile ulibeba maana hukutaka Coletha apokee he he"
"Ha ha ha a suprise for Bro" Derrick akajibu
"Mmmh.... suprise ya picha uliyomtumia ndio hataki tuione" maneno ya Coletha yakamfanya Li ainue jicho la kuhoji kwa Derrick..
"Hey Coletha gossip is bad, ammhh.. achana nae bro hajui chochote alikuwa anachungulia...umbea wake tu.. hata haelewi alichosikia" Derrick akajaribu kulipoteza wazo ambalo Coletha alikuwa anajaribu kulipanda kwenye kichwa cha Li. Akaamua kuaga..
"Mie naenda, nina mambo machache ya kuandaa kwa ajili ya zawadi ya mom" Derrick akainuka
"D... I know you, usiniumbie kesi nitakayoijibu aisee" Li akamjibu huku jicho lake likionesha anajua kuwa anamficha kitu
"Aaah ha ha ha.... hamna kitu bro"
Wakaachana, Coletha akaenda ndani na Li akatoka kutembea nje wakati akimtoa Derrick.
*************************
"Aretha" Ed alisema taratibu wakati akitafakari kile alichokiona kwenye picha aliyopewa na mdogo wake.
Kuna namna hii picha ilikamata mawazo ya Ed, aliamini kuna namna mkono wa Aretha utakuwa umehusika. Akakusudia kumuuliza Derrick ikiwa anamfahamu Aretha
"Au kuna namna Loy atakuwa alimpa vidokezo." Aliwaza Ed..Kufikiri kuwa Derrick nae anahusika kumsogeza karibu na Aretha haikuingia akilini kwake kabisa.