Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 30 - UTAUJUA UKWELI

Chapter 30 - UTAUJUA UKWELI

Sauti ya mlango ukigongwa taratibu ilimshtua Ed aliyekuwa amepitiwa na usingizi mwepesi wa alasiri.

"Nakuja" aliitika Ed wakati akijiinua kitandani na kuelekea mlangoni,

"Oooh sorry kukuamsha bro" maneno haya yaliambatana na tabasamu zuri kutoka kwa Derrick.

"Usijali D. Tukaongelee huko ofisini" Ed alifunga mlango wa chumbani kwake na wakafuatana na Derrick hadi kwenye chumba chake cha kujisomea ambacho kiko ghorofa sawa na chumba chake cha kulala.

"Kabla ya kuongea bro nina peace offering yangu kwa ajili yako" Derrick alisema maneno haya kabla ya kukaa

"Ahaa....' peace offering' hatuna ugomvi mdogo wangu" Ed alisema akimtupia jicho la utani Derrick

"Ha ha ha kweli bro, let's say ni zawadi yangu kwako" Derrick alisema na kunyoosha ile zawadi akimkabidhi

"Ooooh asante sana, you are mysterious Derrick" Ed aliipokea huku akiitupia jicho la uchunguzi, lakini kabla ya kuifungua Derrick akamuwahi

"Bro wala hakuna siri, ni picha tu nilimuomba rafiki yangu achore. Nataka ujue you are my precious brother nakujali sana."

"Asante D, am sorry, nilikuonesha udhalimu na kusahau wewe ni ndugu yangu. Nilipaswa kukusikiliza kwanza. Niliacha hasira inipofushe" Ed aliyasema haya maneno akiwa ameegemea kwenye meza, na wakati huo Derrick naye alikuwa amesimama

Ed alihisi kushusha mzigo mzito, aliiweka ila picha mezani na kumsikiliza Derrick ambaye alimsogelea na kumpa kumbato la kiume.

"Bro hili limepita, nisamehe pia sikukutafuta tuongee. Let's put it behind us"

Walipoachana, Derrick alienda kukaa kwenye kochi na Ed akarudi kuegama kwenye meza.

"Thank you D.. sitaki kujua mlikwazana wapi na Lyn au nini kilitokea lakini nimechagua kuliacha hili kama misunderstandings." Aliendelea Ed huku akimuangalia Derrick ambaye wakati huu sura yake ilionesha kumfuatilia kaka yake kile alichosema

"Sawa kaka, na mimi nashukuru kama hutataka kujua lakini niamini sikunyanyua hata mkono wangu kumgusa. Yamepita hayo. Nami najua ipo siku sote tutaujua ukweli na hasa wewe. Sitaacha kusema Lyn sio huyo unayemfahamu." Derrick akatoa na yeye duku duku lake...

Kimya kifupi kikapita, Ed alirudisha akili kwenye ile alama iliyokuwa shingoni kwa Joselyn. Kweli alitamani sana kujua aliipata wapi lakini hakutaka kujua kutoka kwa Derrick...

"Sio Derrick, ni nini Joselyn alitaka kitokee kwa kusema vile" moyo wake uliongea. Alishtuliwa na Derrick

"Ammhh.. kwa kuwa hili limeisha basi undugu wetu umeimarika zaidi."

"Oh kweli." Ed alikubaliana na Derrick kisha akachukua zawadi ambayo alipewa na ndugu yake..

"Ngoja niangalie my gift, sijui but nahisi unataka kunishangaza"

"He he he he una wasi wasi tu, but you will like it." Derrick alimtania kaka yake akijua kuwa mara macho yake yatakapoona kazi ile ya sanaa atashangaa.

Baada ya karatasi ya juu iliyofunga fremu ya picha kuondolewa macho ya Ed yalikutana na muonekano wa picha uliomuacha mdomo wazi,

"Hey D, hii picha inaonekana kama halisi kabisa, the setting exactly like my office... wow this is amazing?" Ed akarudisha macho kwa Derrick ambaye alirudisha tabasamu jepesi usoni.

"Umeipenda?" Derrick aliuliza

"Nimeipenda.. asante brother" Ed akayarudisha macho tena kwenye picha. Na kila mara hii aliona kitu cha tofauti kwenye picha. Picha ilimuonesha akiwa amesimama kwenye meza akichukua mfuko na pembeni alionekana mtu amekaa kwenye kochi na miguu tu ndio ilionekana kuchorwa.

Ed akashtuka, alipouona mfuko ulikuwa ni sawa na ule aliomkabidhi Aretha siku alipokuja ofisini. Akajaribu kukumbuka nguo aliyovaa siku ya mkutano wake na Aretha.. oooh exactly zile zile nguo..

Wakati Ed akizidi kuchanganyikiwa na kile alichokiona, Derrick alikuwa akitabasamu mfululizo.

"Hey D, nani aliyechora hii picha?" Ed aliuliza huku macho yake yakiwa bado yapo kwenye ile picha...

"Rafiki yangu, kwani vipi bro?" Derrick aliuliza huku akiinuka na kumsogelea kaka yake..

"Nothing! Nashangaa aliipataje hii scenario? D... una spy ofisini kwangu?" Sura ya Ed ilijaa u-serious hata Derrick hakutegemea, lakini alijua kaka yake hana akili nzito kushindwa kuelewa upekee wa picha ile hasa kwa scenario ile.