Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 29 - MISSION YA SIRI

Chapter 29 - MISSION YA SIRI

Geti la nyumba hii lilifunga taratibu baada ya Ed kuingia ndani, moja kwa moja aliingiza gari lake sehemu ya maegesho. Baada ya kuhakikisha ameegesha vyema, akazima injini ya gari na kisha akachukua baadhi ya mafaili yaliyokuwa kwenye kiti cha nyuma na kushuka nayo chini. Akaelekea ndani, huku sauti ya Coletha na Linus zikisikika mara tu alipoingia sebuleni.

"Ooooh afadhali bro kaja, njoo unisaidie kumshinda Li!!" Coletha akapepesa macho akimsihi kaka yake ambaye alitupia macho kwenye kioo cha TV kuona mchezo waliocheza..

Akaachia tabasamu la upande, "Cheza tu baby sisy, nina njaa" huku akiangaza macho Ed aliita "Zena"

"Ha ha ha baby sisy huna wa kukusaidia, haki sawa ndio hii" Li alimdhihaki Coletha baada ya Ed kutoa udhuru wa kujiunga nao. Mchezo walioucheza uliitwa "the warrior" ambapo wachezaji walipewa silaha kupambana na maadui na kila adui alibeba point zake.

"Bro vipi" Li alitoa salam huku macho yake yakiwa sawia kwenye Tv.

Ed wakati huo alikuwa tayari kasimama kwenye meza ya chakula,

"Poa" alijibu

Zena aliingia mikono yake ikionesha dhahiri alikuwa akifua nguo,

" Abeee kaka"

"Kuna chakula kilicho tayari huko jikoni?" Aliuliza Ed, akikumbuka sana chakula cha nyumbani na leo amechagua kutokula nje.

"Mboga ipo, nipe dakika chache nikuandalie hata usiende juu" Zena alijibu na kugeuka wakati huo huo kuelekea jikoni.

Mambo mengi yaliyajaza kichwa cha Ed lakini alioona vyema kukaa na nduguze wakati akisubiri chakula.

"Afadhali bro umekuja, Li imekula kwako" Coletha alimdhihaki Li baada ya kuona Ed kachukua mashine yake kumsaidia, akakaa pembeni akiangalia

"Aaaaah wewe huniwezi, na kwenye hili game bro namtoa" Li alijitapa mbele ya kaka yake..

"Una uhakika Li?" Akauliza Ed wakati akifungua vifungo viwili vya shati yake...

"I will beat you bro" Li akamjibu

"Oooh, let's do it" Ed akaachia tabasamu kisha wakaanza kucheza.

Zena aliporudi kumkaribisha Ed, aliishia kusimama kwa mshangao kumuona Ed akicheza na Li, hakuweza hata kumshtua kwa namna alivyokuwa ameweka umakini kucheza.

Ed aliweka mashine mezani na kuinuka huku Coletha akimzodoa Li baada ya kushindwa.

"Respect bro, sikujua una ujanja mwingi huku nako" Li akampongeza kaka yake na kukubali kuwa ameshindwa.

"Ha ha ha kwa hili nina rekodi ambayo bado haijavunjwa... jaribu game tofauti na hili" Ed alijibu na kuelekea mezani kupata chakula.

Alipomaliza kula Ed aliinuka kuelekea chumbani kwake...

"Li, Derrick akifika mtaniamsha nahitaji kupumzika kidogo kwa sasa."

"D anakuja leo?" Coletha aliuliza, wakati huo Ed aliamua kuwaacha akijua mdogo wao anavyopenda kulalamika

"Aaaaargh... yaani sio wewe wala D mwenyewe kuniambia" alilalamika Coletha

"Eeeh anakuja.... acha basi malalamiko dada yetu." Li akamtania

"Am so happy.... anarudi kabisa?" Aliuliza kwa hamasa

"Hahaha Coletha.... wewe na D ni mapacha kwa nini hajakwambia?" Li akaendelea kumtania

"Toka aende Heaven kawa kama mgeni, tunakutana chuo tu, tena ananipungia mkono kwa mbali... nahisi ana mission ya siri sijaijua bado?" Coletha akalalama

"Hahaha mchunguze akija leo" Li alimaliza kisha akainuka na kuelekea jikoni huku akirudi na glasi ya maji akakaa na kuendelea kutekenya kompyuta mpakato.

Ed alipofika chumbani aliingia bafuni kujimwagia maji na baada ya hapo alichukua kompyuta mpakato na kukaa nayo kitandani akiangalia mambo machache aliyotoka nayo The Base.

Kumuuliza Joselyn ndio mpango mkuu aliokuwa nao akilini. Akachukua simu na kumpigia Lyn, akaamua kuongea nae pasipo kuonesha hasira yoyote japokuwa kitendo cha kujua Martinez anahusika kilimpa hasira.

'Kweli anayekuchekea si wakati wote anakuwazia mema' alisema moyoni Ed.

Baada ya kuongea na Lyn walikubaliana aonane nae kesho yake, kitu ambacho kilimfanya Lyn aone Ed yuko sawa.

"Let's wait and see your reaction darlin... natamani uwe hujui lolote" maneno yalimtoka Ed baada ya kuwa amehamisha picha kadhaa kwenye simu yake na akasukuma pembeni kompyuta na kujinyoosha kitandani.

Akaunganisha matukio tofauti ya namna alivyokutana na Joselyn hadi walipofikia, akajaribu kutafuta ujanja wowote lakini hakuweza uona.