Chereads / Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 28 - SUPRISE (4)

Chapter 28 - SUPRISE (4)

"Mama usimlazimishe sana, nina sehemu nyingine nataka anisindikize siku ya jumatatu." Derrick akatumia tena fursa hiyo ambayo alikuwa na hakika Aretha hatoweza kuikataa

"Hamna shida Derrick, jumatatu yaweza kuwa rahisi kwangu iwe tu haijaingiliana na ratiba ya chuo.." alijibu Aretha ambaye wakati huu alikuwa akila tufaa.

"Uwhhhh huyu binti yangu sijui ni wa aina gani. Haya hiyo jumatatu msindikize mwenzio" mama Aretha alizungumza huku akiinuka kuelekea jikoni.

"Mama jamani" Aretha alishusha pumzi akikerwa na neno "mwenzio" alilotumia mama yake...

Derrick alikuwa na tabasamu jepesi usoni,

"Twende unioneshe picha zako unazochora, sitakusumbua tena hadi jumatatu"

"Aaaah mmmhh sina picha nyingi." Alijibu Aretha

Derrick akamwangalia kisha akaweka mgomo

"Kama hunioneshi picha na mie nitashinda hapa hapa......tena ngoja nimpigie ndugu yangu kuwa leo tusikutane...." Aretha alimkatiza Derrick aliyekuwa akishika simu yake kama anayetaka kupiga

"Aah... basi... nitakuonesha chache... nifuate?" Aretha alisema huku akiinuka kuelekea mlango uliowatoa nje

Walipokuwa nje waliingia kwenye nyumba ndogo iliyokuwa pembeni ambayo ulionekana kuwa maalum kwa ajili ya wageni. Baada ya kufungua, sebule ndogo iliwapokea na Aretha alimpa ishara Derrick afumbe macho. Akainua zuria na kuchukua ufunguo kisha akafungua mlango mmoja na kumwambia Derrick afumbue macho.

Derrick baada ya kuingia kwenye chumba kile, uso wake ulibeba mshangao na akayarudisha macho yake kwa Aretha..

"You are a painter Retha... oooh my God"

Akapita kwenye picha zilizokuwa kwenye mbao za kuegemeza picha... Derrick aligundua kila picha ilibeba tukio fulani na kwa namna ziliwekwa haikuwa ngumu kwake kufahamu.

"Haya matukio uliyochora ni kumbukumbu ya mambo uliyoyaona eeeh" aliuliza Derrick

Aretha aliitikia kwa kichwa huku mkono wake ukipapasa picha ambayo ilikuwa karibu na meza iliyokuwa kati kati ya chumba.

Derrick alipeleka macho kuona picha hiyo, alipoangalia kwa makini, macho yalimtoka na akapiga hatua kwa haraka kitendo kilichomshtua Aretha.

Derrick aliichunguza how picha akagundua ni mandhari ya ofisini kwa Ed. Tabasamu lilimtoka Derrick na kumfanya Aretha kumuuliza

"Vipi mbona umeshtuka?"

"Hahaha hapana nimeipenda hii picha, naweza kuinunua" aliuliza Derrick

"Mmmh sijawahi kuuza picha" alijibu Aretha kwa aibu

"Aaaaaah, hauna meneja au mtu anayehusika na hizi picha zako?" Aliuliza kwa mshangao Derrick maana aliamini kabisa picha zile zinaweza kuwa biashara kwa Aretha.

"Hapana"

"Okay, basi mimi nitaanza kununua hii, na naomba niwe meneja wako" maneno haya yalimfanya Aretha kushangaa to asijue cha kujibu

"Aretha please, niamini hii itakupa pesa hope nafasi nikusaidie" Derrick alimsihi Aretha

"Nitakuuzia nyingine lakini sio hii.... kuwa meneja sijui inakuwaje na utafanya nini, nitauliza halafu nitakwambia" Aretha alijibu na kukaa kwenye stuli iliyokuwa mbele ya picha moja.

Derrick akawaza nini afanye ili aipate ile picha.

"Retha, nitainunua hii picha kwa gharama yoyote, utachora nyingine bila shaka. Nakuomba"

"Kwa nini hii?" Aliuliza Aretha..

"Aaargh..... Retha nimeipenda ni hivyo tu, imekaa kiume"

"Hapana Derrick" Aretha aliweka msimamo wake sawa.

"Basi sawa. Nipe hiyo ya machweo ya jua" Derrick aliamua kuchukua nyingine.

Baada ya Aretha kuitoa na kuizungusha safi kwenye mbao yake akamkabidhi Derrick.

Sauti ya mama yake Aretha iliwashtua akimuita Derrick na mwanae.

Akaingia ndani na kuwaambia anataka kutoka Derrick nae akatumia mwanya huo kuaga. Lakini kabla ya kutoka mama yake Aretha akamtoa Aretha na kwenda nae nje akitaka kumpa maagizo kwa kuwa angechelewa kurudi. Derrick akatumia mwanya huo kubadilisha picha na kuzungusha picha ile nyingine kwenye mbao. Akatoka nje ambapo alikutana na Aretha na mama yake,

"Mama nikusogeze mbele kama hutojali nimekuja na piki piki yangu na hapa natakiwa sehemu muda hii " alisema Derrick

"Ooooh mwanangu asante, na umri huu siwezi, nitaita tu gari" mama Aretha alijibu..

"Aaaaah basi sawa ngoja nikimbie mara moja.."

"Haya mwanangu... uje tena hapa ni nyumbani"

"Asante  mama" Derrick alijibu na kufungua geti dogo tayari kuondoka.

"Msindikize mwenzio" mama Aretha alimsukuma binti yake ambaye alilalamika kwa nini mama yake anamuita Derrick mwenzie.

Alipofika nje Derrick alikuwa tayari ameshawasha piki piki yake na alipogeuka na kumuona Aretha akaachia tabasamu kisha akampa ishara amsogelee..

"Naomba namba ya mama" Derrick alimuomba Aretha ambaye alimwangalia usoni akishangaa kwa muda mchache Derrick amekuwa karibu na mama yake hata kumpita yeye..

Baada  ya kumtajia, Derrick akamuaga Aretha na kuondoka. Akafanikiwa kuondoka na ile picha iliyochorwa mandhari ya ofisi ya Ed. Alielekea hadi mahali ambapo aliiweka ile picha kwenye flemu na kuifunga katika namna ya zawadi. Akiwa pale alimpigia mama yake Aretha, na baada ya kujitambulisha na namna alivyoipata namba yake, akaendelea

"Mama naomba unisamehe, nahitaji msaada wako" Derrick alisihi kwa sauti ya upole

"Niambie mwanangu kwani umenikosea  nini?" Aliuliza mama Aretha kwa mshangao

"Mama, kuna picha ya Retha nimeichukua bila yeye kuniruhusu, lakini ni kwa wema mama. Nataka kumsaidia auze picha zake sasa yeye hakutaka hiyo picha kuiuza. Now naamini atachora nyingine kama hiyo."

Alijieleza kwa unyenyekevu hata kumfanya mama Aretha kumsikiliza pasipo hata kutilia mashaka kitendo hicho. .

"Oooh kwa hiyo nitakusaidiaje hapo mwanangu, binti yangu hupendi kabisa kushika picha zake bila ruksa yake"

"Najua mama, ndio maana naomba umwambie uliichukua. Ila nakuahidi mama mambo yatakuwa mazuri baada ya huo picha" ilikuwa ni kazi ya Derrick kumhakikishia mama huyu usalama na mafanikio ya binti yake...

Kimya kifupi kilipita kisha mama yule akasema

"Derrick mwanangu nakuomba usifanye chochote kikamuumiza Retha. Najua mwanangu hajui mambo mengi kijamii lakini ana akili ya kupambanua vitu. Nitakulinda na usiniangushe kuhusu kumsaidia"

Derrick alijawa na furaha na akamhakikishia mama yake Aretha kabla ya kukata simu. Baada ya hapo alielekea kwake kujiandaa kusubiri muda wa kuonana  na kaka yake.

*******************************