Download Chereads APP
Chereads App StoreGoogle Play
Chereads

WEWE NI CHAGUO LANGU

🇹🇿Doris_Benas
--
chs / week
--
NOT RATINGS
5.6k
Views

Table of contents

VIEW MORE

Chapter 1 - Sehemu ya kwanza

(by benasdoris@gmail.com)

Baada ya kumaliza Elimu yangu ya Sheria katika Shule ya Sheria iliyopo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), nilirudi nyumbani Arusha ambapo ndipo nilipozaliwa, ninaishi na Mama yangu pekee, kwani Baba yangu mzazi alifariki nikiwa na umri wa miaka sita tu, Mama yangu Bi Rose, ni aina ya Mama mchapakazi na anayrpenda sana raha, yani kwa kusema hivyo namaanisha kwamba, anajali sana Biashara yake ya Nguo za kike, anapenda sana kula vizuri, Kupendeza, kufurahi, na anapenda sana Mimi niwe na furaha na kufata kile anachonifundisha.

Jina langu naitwa Tracy Benson Lawison, ni binti mwenye miaka 24, baada ya kukaa nyumbani kwa Muda wa miezi kadhaa, siku moja nilipokea ujumbe katika Email yangu kwamba ninahitajika kwenye Interview katika Kampuni moja kubwa Maarufu jijini Dar es Salaam, binafsi nilifurahi sana kupata ujumbe huo, nilimpa mama taarifa, yeye pia alifurahi sana, Mama aliniandalia kiasi cha pesa ambacho kinanitosha kukamilisha zoezi hilo pindi nitakapokuwa huko, hiyo ni pamoja na nauli pamoja na pesa ya Malazi na Chakula.

Tarehe 21 January 2021, nilipanda ndege kuelekea Dar es Salaam, kwa ajili ya kujiandaa na Interview itakayofanyika Alhamisi ya Tarehe 24 January, nikiwa ndani ya ndege nilikua nina shauku ya kupata kazi katika kampuni hiyo na nikawa nina mawazo ya mbele zaidi kwamba mara tu baada ya kupata kazi nitafanya hiki na kile, kiukweli sikuwa na wazo la kukosa kazi au kufeli Interview hiyo, Matumaini na ujasiri niliokuwa nao ulizidi kunitia moyo kikamilifu, Kwamba kwa uwezo wa Mungu lazima tu nitapata kazi.

Masaa machache baadae, ndege ilitua katika Uwanja wa ndege wa Taifa wa Mwl JK Nyerere jijini Dar es Salaam, nilimshukuru Mungu kwa kuniongoza na kuisimamia safari yangu mpka nikafika salama, Kwakuwa sikuwa mgeni jijini Dar, nilipakia mizigo yangu katika Troli maalum, moja kwa moja kwenda kutafuta usafiri ili niende Hotelini kwa ajili ya mapumziko ya siku hiyo.

Nikiwa nasukuma mizigo yangu kwenye Troli, Ghafla nilimwona mzee mmoja aliyekua mbele yangu akiwa anakohoa kwa tabu mpka akaanguka chini, nilikimbia na kuiacha mizigo yangu nyuma ili nimsaidie mzee yule, alianguka mpaka chini huku akionekana kubanwa kifua, sikuwa na uzoefu wala ujuzi wa kitabibu wa kumsaidia mzee huyo, hivyo nilianza kupaza sauti kuomba msaada wa karibu, Nikiwa nimechuchumaa chini nikihangaika kumtikisa babu yule na kumpa pole, Alikuja kaka mmoja ambaye alinifanya niache kufanya nilichokua ninakifanya na kuanza kumuangalia yeye alikua ni Kijana mzuri sana, mrefu pia mwenye mvuto, alivyofika pale alitoa baadhi ya vifaa ambavyo nilipoviona nilijua wazi ya kuwa huenda akawa Daktari au Nesi, alianza kumuhudumia kwa haraka na uku akiandika baadhi ya vitu kwenye Notebook, Kiukweli muonekano wa yule kaka ulinifanya nisahau kabisa ya kwamba nilipaswa niweke umakini kwa Mzee yule mgonjwa.

Baada ya dakika kadhaa yule kaka alinigeukia na kuniomba niwapigie Ambulance, Alioneka kujali zaidi juu ya Afya ya yule mzee, hakuonyesha kupata shauku yoyote ya kunifahamu, nikiwa bado namtazama Usoni mwake alionyesha kunisisitiza niite Ambulance, Niliwapigia Ambulance, haikuchukua muda Gari la wagonjwa lilifika na kumbeba Mgonjwa yule, Yule kaka aliwapa karatasi ya Maelezo ya mgonjwa huyo baada ya kuchukua vipimo vya huduma ya kwanza, walitushukuru sana na waliondoka na yule Kaka ambaye hakuonyesha kujali wala kuwa na msukumo wowote wa kuonyesha kuhitaji kunifahamu, hakunisemesha neno lolote tofauti ya kuniambia niwapigie Ambulance, nilijiona mjinga baada ya fikra zangu kuanza kuvutiwa na mtu ambaye simjui, Ilihali si kitu kilichonileta Dar.

Nilichukua mizigo yangu na kuchukua usafiri ambao ulinipeleka mpka Hotelini kwaajili ya mapumziko ya siku hiyo, kichwani mwangu nilifuta kabisa mawazo ya yule kaka na sikutaka kuendelea kufikiria juu ya kitu kilichotokea, nilipotezea na niliendelea kufikiria juu ya Interview ya mbele yangu, Niliomba sana Mungu anisaidie nipate kazi ili malengo yangu yatimie, Jioni ilipofika nilipata chakula cha jioni na nikaingia katika chumba nilichopata kwa ajili ya mapumziko.

Majira ya saa tatu usiku Mama yangu alinipigia Video call kwa lengo la kutaka kuniona kama kweli nimefika na kujua usalama wa Afya yangu, Mama alifurahi sana baada ya kuniona bintiye nikiwa ninatabasamu kwa furaha, mimi pia nilifurahi sana kuongea na mama yangu, Nilimshukuru sana Mungu kunipa mama anayejali na kunipenda kiasi kile.

Asubuhi iliyofuata niliamka mapema nikachukua laptop yangu na kuanza kuangalia Website ya Kampuni hiyo pamoja na Kazi kuu ya Kampuni ili inipe mwanga wa kukisia baadhi ya maswali ambayo naweza kuulizwa mimi ambaye nilisomea Sheria, nilipitia baadhi ya Sheria na vitabu mbalimbali ili nipate uelewa wa kujibu maswali kwenye Interview hiyo, Niligusia kila sehemu ya Muhimu ambayo huenda ningeweza kuulizwa kwenye Interview hiyo.

Baada ya masaa kadhaa simu yangu ya mkononi iliita na nilipoangalia ilikua ni namba ngeni na baada ya kupokea ilisikika sauti ya Mwanamke;

"Hello unaongea na Vicky, Secretary wa Reef Company, nadhani ninaongea na Tracy Benson?"

Nilimjibu kuonesha ukubali kuwa mimi ndiye Tracy, alinipa maelekezo kwamba Siku ya Interview natakiwa niwahi mapema sana na nijiandae kikamilifu, na pia alinitakia maandalizi mema, Nilimshukuru na nikaendelea kufanya maandalizi kwa ajili ya Interview ambayo imebaki siku moja tuu ili niifanye.

Kwakua ilibaki siku moja tuu kabla ya Interview, kesho yake ilinibidi niende maeneo ya Kampuni ili nione kwa karibu mazingira yake na muonekano wake, ikiwezekana nipate mtu nitakaezungumza nae ambae ni Mfanyakazi pale, nilianza kutembea kwani hapakua mbali sana na Hotelini ninapoishi mimi,, Kabla sijafika nilipita sehemu ambayo niliona jengo kubwa lililojengwa kisasa zaidi, sikutilia mkazo sana niliendelea kutembea, nikiwa natembea nilimuona Kaka mmoja aliyekua anaongea na simu pembeni, nilipomuangalia vizuri niligundua ni yule kaka niliekutana nae Airport,, nilifurahi sana nikamfuta pale alipokua amesimama…

Je Tracy atafanikiwa kuongea na Kijana ambaye hapo awali hakuonyesha kujali kumfahamu????