" wewe ni nani?" Tulya anasikia sauti hiyo na Kila kiungo Cha mwili wake kina sisimka akili yake ina mtuma kukimbia nyumbani kwake akajifiche chini ya uvungu wa kitanda mpaka mtu huyu atakapoondoka.
Dunila anaendelea kumwangalia mschana huyu mrembo anajaribu kuvuta pumzi kama atapata zile hisia alizoambiwa na harufu nzuri ya ardhi pasipo mafanikio.tangu aingie kijijini hapa hajasikia harufu yeyote na hata Sasa baada ya kumsogekea mschana huyu aliyekuwa anamvutia tangu amuone anachonusa ni harufu nyingi mchanganyiko inayozidi zaidi ikiwa ni harufu ya kitu kinachoungua kama ngozi ya mnyama inayo chomwa.
Anakumbuka maneno ya mtemi Lukomo " harufu ya mmiliki wa ardhi haifichiki hata ukiwa mbali unaisikia na kwa Sababu wamemfunga ndio maana hatuwezi kuisikia lakini kwa Sasa lazima itakuwa ina sikika vizuri ukiwa eneo Moja na yeye,kumbuka ni harufu nzuri ya ardhi iliyopata mvua baada ya mda mrefu ikichanganyika na harufu ya maua ya miti inayochipua na ukimuona ni lazima utavutwa kwake"
Tangu aingie Kijiji Cha Ntungu Dunila amekuwa akivuta pumzi kwa nguvu endapo ataisikia hiyo harufu lakini pasipo mafanikio.
Baada ya watu kukusanyika amekuwa amesimama kwa mda mrefu akiwa amefumba macho yake akivuta pumzi na kuvuta hisia pasipo mafanikio.
Anafumbua macho yake na kuangalia kama Kuna mschana atakayemvutia asimuone.
Alichoona ni watu wakiwa wameinamisha
vichwa vyao kwa heshima lakini hakuwa kwenye Hali ya kupokea heshima kwa sasa.
Hisia zake yote zilikuwa zina mtuma kuwa yule mschana atakuwa Kijiji hiki lakini sasa anahisi kuchanganyikiwa na kujiuliza kama alikosea na kwa mara ya kwanza anaanza kuzitilia mashaka hisia zake kali ambazo hazijawahi kumwangusha hapo awali.
Baada ya mda anasikia mtu akisogeza miguu yake.Anaangalia katikati ya watu wanaomzunguka asione mtu anayetembea.
Anaangalia kwa makini na kumuona mschana mmoja akitikisika hapo ndipo alipogundua kuwa amewaweka watu namna hiyo kwa mda mrefu pasipo kuwaambia wasimame na watakuwa wamechoka.
Anataka kuwaambia wasimame lakini anaacha baada ya kumuona mschana huyo akinyanyua miguu yake na kukanyaga Ili miguu yake itoe sauti kama mtu anayetembea .
' anafanya nini?!' anajiuliza na kubaki amesimama akimwangalia kwa makini.Anamuona anageuza kichwa chake huku na kule kama kuangalia watu wa pembeni yake kama wako sawa na kurudi kukaa kama awali pasipo kunyanyua kichwa.
Anamuona akinyanyua tena miguu yake." usiniambie anajaribu kunipa ishara Mimi kama wamechoka?" anajiuliza na baada ya kukubaliana na akili yake anaamua kuendelea kumwangalia aone atafanya nini.
Mschana huyo anaendelea na mchezo wake kwa mda mrefu pasipo mafanikio na anamuona akinyanyua kichwa chake kumwangalia macho yao yalipogongana anarudisha kichwa chake chini haraka.
Dunila anajikuta akipiga hatua kuelekea alipo simama mschana na baada ya kuwaambia watu wasimame mschana anaendelea kuinamisha kichwa chini.
Anaamua kumpa amri ya kusimama,anasimama na anashangaa kumuona akimwangalia machoni.
kwanza macho yake yalikuwa na woga na baadaye woga huo ukabadilika kuwa wa kihoro.
'atakuwa anagopa kuwa nitamuadhibu namana hiyo?' anajiuliza lakini Kuna kitu kinamvutia,macho yake.
Mschana aliyeko mbele yake ana macho mazuri hajawahi kuona anashangaa mapigo ya moyo wake yakianza kuongezeka.
" we ni nani?" anamuuliza anajishangaa tu anataka kusikia sauti yake na kujua jina lake.
Mkita aliyekuwa maeneo Yale anaona namna Dunila anavyo mwangalia Tulya sio yeye tu hata Wana Kijiji wengine waliliona Hilo lakini wengi walijiuliza kwa nini anataka kumjua.
Kabla Tulya hajamjibu wanasikia sauti nyuma ya Dunila.
" mwana wa mtemi" anasogea karibu Yao mmoja kati ya wazee wakubwa pale kijijini kwao mzee Matalu.
" karibu kijijini kwetu" Dunila anageuka na kumwangalia mzee huyo.
" Asante,hakuna haja ya kuendelea kuweka Wana Kijiji, wanaweza kuendelea na kazi zao" Dunila anasema na wanakijiji wanaanza kusambaa akibaki yeye na walinzi wake na baadhi ya wazee.
Tulya aliyekuwa ameganda mda wote huo kama kamwagiwa barafu kauli ya Dunila ilikuwa kama moto uliyo myeyusha.
Anageuka haraka haraka na kuanza kuondoka akimvuta mkono Sia.
Dunila anageuka ili kuendeleza mazungumzo yake na Tulya lakini anamuona huyo akiondoka anataka kumwita lakini anaacha baada ya kuona shanga kiunoni mwake.
" ameolewa?!" anaongea kwa sauti ya chini lakini mzee Matalu anamsikia na watu waliokuwa karibu akiwemo Mkita.
Mzee Matalu anaangalia alikoelekea Tulya na kumwangalia tena Dunila.
" ndio,imekuwa ni miezi mitatu Sasa au na zaidi tangu aolewe" anajibu mzee Matalu akijua aliulizwa yeye swali kumbe mwenzake alikuwa anaongea mwenyewe baada ya mshtuko.
pasipo hata mzee Matalu kujibu ushahidi kuwa Tulya kaolewa ulikuwa mbele yake kwani Kila mwanamke mwenye shanga kiunoni anaashiria kuwa ameolewa.Dunila analijua Hilo na Kila mtu pia.
" nilikuwa napita tu Nina safari zangu Haina haja ya kunikarimu ninaondoka" Dunila anamwambia mzee Matalu akiwapatia ishara walinzi wake wanaanza kuondoka macho yake yakienda kwa Tulya anayezuga kiuno chake kutembea haraka haraka kuondoka mahali pale.
" kwa nini asikimbie tu?" anaongea Dunila kwa sauti ya chini akiendelea kumwangalia Tulya na pasipokujua anajikuta akitabasamu baada ya kumuona kapotea anaendelea na safari zake kwani hapa kijijini imekuwa kazi bure.
" shemeji yangu yupo kama maua na nyuki" anaongea Mkita akitabasamu.
" Ninaenda mtoni kuoga" anawaaga wenzake na kuondoka uso wake ukiwa na tabasamu la kuokota embe dodo kwenye mpera na anajua mbele ya safari atalifaidi zaidi.
" tutembee pole pole Tulya" Sia anasimama baada ya kuchoka kuburuzwa na Tulya.
Tulya anamwachia " mbona unatembea kama unakimbizwa?" Sia anauliza.
" aaam,Nina haraka tu kidogo nataka niende nyumbani kwa mjomba nikachukue mboga nikapike haraka mume wangu atakuwa na njaa" anamjibu akianza kutembea.
Sia nae anamfuata akiamini uongo wake.
" uuuuh, hiyo ilikuwa inatisha" mwili unamsisimka baada ya kukumbuka namana Dunila alivyo msogelea na jinsi alimwangalia hajui ni kwa nini aliogopa au kwa Sababu alikosa na kujua ata adhibiwa.
" siku moja utakuja kufa kwa kihere here chako Tulya na leo ni mfano unaotakiwa kuuweka akilini shukuru miguu yako imekuwa myepesi kukutoa pale" anaendelea kuongea kwa nguvu asijue mawazo yake anayatoa njee.
" kwa nini ufe?" anasikia sauti ikimuuliza,anamwangalia Sia na kutikisa kichwa." Amna kitu twende zetu"
Upande wa pili mtoni Nzagamba akiwa amekaa kwenye jiwe karibu na mto anapowindia ndege akili yake ikiwa imevurugika baada ya purukushani lake na mnelela anakumbuka namana alivyomkamata na kumuuliza kwa nini anamfuatilia majibu aliuompa bado hayaelewi.
" wewe ni nani na kwa nini umekuwa ukinifuatlia?" anamuuliza mnelela baada ya kumuwekea kisu shingoni kwake.
"Huuu?!" Mnelela anashtuka kwani hakutegemea."nimekuuliza wewe ni nani?" anarudia tena Nzagamba.
" tafadhali usiniue Mimi nimetumwa tu kukulinda sio mtu mbaya" anajitetea Mnelela jasho likimtoka.
" kunilinda? kunilinda na nini? na nani kakutuma,sema" Nzagamba anauliza kwa ukali akisogeza kisu karibu na koromea.
" aaah,sio kukulinda hiyo ni kazi ya mtu mwingine Mimi ni mzim nimetumwa kukuangalia kama umepata nguvu zako"
Nzagamba anashangaa alikuwa anajua huyu sio mtu wa kawaida lakini kukubali kuwa yeye ni mzimu inamshtua zaidi.
Wakati anajaribu kurudisha akili mnelela anatumia nafasi hiyo kuyeyuko na kupotea Ili kuokoa maisha yake kama sio uhai wake wa mara ya pili.
Kwa Sasa Nzagamba akiwa amekaa anaangalia mkono wake ambao bado umeshikilia kisu asiamini kama kamshika mzimu na kuutishia na ulikuwa unamaana gani uliposema kuwa ulikuwa una mwangalia kama amepata nguvu zake
" nguvu gani?" anajiuliza.
Anavuta pumzi ndefu na kutoa macho yake yakienda mtoni kwenye maji " kwanini maisha yangu yamepinda namna hii Sasa nafatiliwa mpaka na mizimu?!" anajiuliza na kujikuta akicheka kidogo.
Anageuka baada ya kusikia sauti za watu wakiongea na hatua zao zikisogea anamuona Mkita,Lingo na Ntula.Anafumba macho akijua utulivu wake umekwisha kuvurugwa.
" Nzagamba umeskia " anaongea Ntula akikaa karibu yake Lingo nae akilala kwenye jiwe na kuangalia mti juu akisema " Mkita ana habari nzuri na mbaya kwako"
Nzagamba anamwangalia Mkita aliyesimama mbele yake akimwangalia kwa tabasamu analolijua vizuri.
" ongea haraka ,kama huongei toka mbele yangu siko kwenye Hali ya kucheza na wewe"
Mkita anachukulia hiyo kama ruhusa na kuanza kuongea kwa bashasha.
" ni kweli Nina habari nzuri na mbaya kwako kama alivyosema Lingo"
" nimesema kama huongei uondoke hapa" Nzagamba anamjibu.
" tulia Sasa nikwambie,habari nzuri ni kuwa mkeo ni mzuri sana tena kupindukia"
" toka hapa" Nzagamba anaongea akimnyoshea kisu chake mkononi Mkita anasogea kukikwepa.
"si nimekwambia siko kwenye Hali ya kucheza na wewe Leo?"
" ohh, pole pole na kisu Nzagamba,siogopi kufa kwenye mikono ya rafiki yangu kipenzi lakini familia yangu inanitegemea na mke wangu bado mdogo mno kuwa mjane na kumwachia mtu mwingine aanze kufaidi itaniuma sana kiasi Cha kugeuka mzimu na kukuwinda wewe na mkeo msifanye kitu chochote iwe usiku au mchana hiyo itakuwa ni adhabu yako Nzagamba"
" msikilize Nzagamba la sivyo utajuta" Ntula anamshika bega Nzagamba kumpoza naye anatuli.
" sema"
Mkita anatoa ulimi wake na kuramba mdomo wake wa chini kama anakombeleza asali aliyoiiba kwenye kibuyu Cha Babu.
" ongea" Nzagamba anaonekana kukereka zaidi na tabia ya mkita.baada ya kupata mwonekano aliokuwa anataka kutoka kwa Nzagamba Mkita anaendelea.
" na habari mbaya ni kuwa mwana wa mtemi amekuja kijijini leo kamuona na kampenda"
****usisahau comment yako*****