Chereads / MAHAMENI Nyumbani Kwetu Pa Zamani / Chapter 1 - Nyumbani Kwetu Pa Zamani.

MAHAMENI Nyumbani Kwetu Pa Zamani

John_Raphael_8794
  • --
    chs / week
  • --
    NOT RATINGS
  • 4.2k
    Views
Synopsis

Chapter 1 - Nyumbani Kwetu Pa Zamani.

Basi huko nilikokuwa hakukuwa maskani, hakukuwa nyumbani kwangu. Ukweli ni kwamba nilikua nakuskia tu japo niliwahi kupita lakini nilipelekwa rasmi nilipoanza kidato cha kwanza.

Hapo ndipo nikajikuta kama mzamiaji niliyeingia taifa la watu bila karatasi yeyote ya kunitambulisha.

Nilizidi kutabiri ugumu wa maisha nitakayoyaishi pale ila sikujali, mwalimu wetu alituambia tuongee ngeli tu!!!, ndiyo ni kiingereza tu, bila hivyo, mtu hatoruhusiwa hata kwenda mariwato,

Nilipelekwa nchi ambayo nilitamani kufika tangu nikiwa shule ya awali, lakini kwa sababu hapo nilikuwa mbumbumbu kabisa, basi yule mwalimu wetu alipokuwa akiongea kiingereza nilikuwa simuelewi, ikanibidi nimtizame usoni na mwendo wa lipsi zake kisha natafsiri taswira yake kwa lugha ya kiswahili.

Sio mimi tu, hata marafiki zangu vipanga waliambulia mapichapicha. Mwaka mmoja, miaka miwili, mitatu hadi ikakamilika miaka minne, mimi na washkaji zangu wachache tukachaguliwa kwenda kujiunga na hatua iliyofuata sehemu nyingine tu lakini ni jamii yenye utamaduni uleule na lugha ni ileile, kikristo, japo kule ni kikristo kile kilichokomaa zaidi sio kama huku nilikotoka.

kule nilikopelekwa nilikuta wakufunzi wengi alafu wao wanapiga ngeli, ile mbaya. Sikuhtaji tena kujifundisha kutamka maneno ya lugha ile maana tayari nilisha jifundisha ndani ya ile miaka minne, hivyo, sikudata hata kwa ile ngeli konki aliyokuwa akiiongea yule mkuu wa pale amabye hakuwa muingereza.

Sista Morin alikuwa mfilipino, basi hata akiongea kiingereza ni kama anaongea lugha nyingine aliyoitunga mwenyewe, lugha nyingine ngumu, au kama ni kiingereza, basi ni klie kilichoota manyoya.

Miongoni mwa vitu tulivyofundishwa ni pamoja na kuukataa ukoloni, tusiwe watumwa wa wazungu, tuupende utamaduni wetu, nahisi nachelea kusema tulifundishwa kuwa wazalendo.

Mimi niliyashika mafunzo mapema, basi nilikuwa nikiwafundisha na wenzangu wayashike kama mimi, lakini, nilitumia lugha ya kiingereza niliyoifahamu vizuri kabisa na kuiongea utazani na mimi ni wa hukohuko.

Nilipiga ngeli kwa deko huku nikipindua sentensi huku na huku , sentensi zilizodamshi kwa maneno yangu konki ambayo mengine niliyashika mwanzo kabisa "characteristics" pamoja na nomino za majina ya watu na mahali "Arnold Schwarzenegger" na "Szechoslovakia".

Niliishi hapo kwa miaka miwili tu, mbele kidogo na maisha yale, mbele kidogo na eneo lile kulikuwa na kituo kingine ambacho nilijikuta nimebwagwa pale, kulikuwa na watu wengine ninao wafahamu, akina stela, agnes, lito na kaka stivu aliyefika pale mwaka mmoja kabla yetu.

Lakini!!!, nilishangaa kuona sehemu ile tupo huru kidogo, tulikuwa tunachati kwa lugha ya kiswahili na kiingereza ,lakini pale!!!, kiswahili hakikupigwa vita kama kule nilikotoka.

Ni nchi gani hyo?, tulipofika nchi ile, kiingereza kikabaki tu kwenye makabrashi tuliyoyasoma au kuyaandika .

Nilikuwa na fraha lakini sikujua kama nina fraha, fraha iliyotokana na nisichokijua pia, lakini nilifrahi kuona silazimishwi kuongea kiingereza nikitaka huduma. Fraha yangu ilizidi nilipojua kuwa baada ya mda flani, sio kitambo, tutaruhusiwa kurudi uswahilini, uswazi, nilifrahi maana nchi ile ndiko waliko ndugu zangu.

Japo ilichukua mda mrefu lakini nilirudi nyumbani, nyumbani uswazi.

Nilipomaliza shahada yangu ya kwanza nikarejea mtaani, mtaani ambako walio wengi wanaongea kiswahili na vilugha tu, yaani, lugha zao za asili, kiyao na kimwera, kizigua na kindengeleko.

Kumbe, kuongea kiingereza kwangu ilikua ni kama nipo nchi nyingine ya mbali, nchi ya watu, ni uingereza, au marekani, au kanada lakini kumbe skuwa huko, skuwai hata kukanyaga.

Fraha yangu ilirejea baada ya kuhitimu masomo kisha kurejea mtaani na kuanza kukiongea tena kiswahili ambacho nilikisusa miaka mingi, lugha ambayo nimeinyonyea toka kwenye maziwa ya mama yangu, basi ndani ya kiswahili nyumbani kwetu pa zamani kuna protini zote.

Nilifrahi nilipofika uswahilini, ni kama baba aliyetoka safari ya mbali au msafiri aliyerejea maskani yake baada ya kitambo. Nilifrahi kuona vile marafiki zangu wanaongea lugha tamu, lugha ambayo imebeba lugha zingine nyingi, lugha ambayo, kama nisingekuwa makini nisingejua kuwa ni kiswahili.

Nilikuta lugha yetu imekua na kubadilika, kiasi cha kwamba, kama tukiwaamsha waliokufa miaka ya themanini alafu tuongee nao kiswahili cha sasa basi tusingeelewana kabisa. Nilikuta rafiki yangu Jose anaita Dingi akimaanisha baba na bimdashi akimaanisha mama.

Na mimi nikaanza kutema ile lugha ambayo hata hivo ina maneno mawili matatu ya kiingereza hata lipsi zangu zisipate shida kuyatamka.

Yale maneno magumu ya kiingereza sikuyatumia tena maana hata pale nilipo mwambia mtu "little prick" Rascal" little brat" hawakunielewaa!!! basi ni kama najiambia tu mwenyewe.

Wiki, mwezi, miezi, hadi mwisho nikaweza kuongea kiswahili dakika stini bila kutaja neno lolote la kiingereza.

Na sasa, Ninayo fraha kuskia lugha niliyo inyonyea toka kwenye maziwa ya mama yangu inafundishwa nchi zingine.

Nimerudi MAHAMENI.